Thursday, August 05, 2010

Anguilla Festival 2010


Mshindi akijiandaa kuimba wimbo wake kuhusu umoja wa visiwa vya Caribbean.
Mshindi akiimba wimbo wake.
"YAH MAN! Anguilla kuzuri!"
Mashindano ya Calypson ya Vijana kwenye TV. Huyo binti hakuwa na sauti nzuri lakini nilipenda hiyo nguo aliyovaa ya kuwakilisha Anguilla.
Waziri Mkuu (Chief Minister) wa Anguilla Hubert Hughes

Wadau, jana jioni nilienda kwenye mashindano ya Calypso hapa Anguilla. Ilikuwa safi sana. Walishindana wanawake wanne na wnanauma 6. Mwanamke ndiye alishinda na nyimbo yake ya kuhusu visiwa vya Caribbean kuwa na umoja.

Nyimbo nyingi zilihusu siasa za Anguilla. Nimeshangaa maneno wazi wazi hakuna maficho. Mfano walisema kuna rushwa tele, waAnguilla wanaonewa na mabenki. Hawawezi kupata mikopo. Walilamika kuwa waChina wana haki kuliko waAnguilla na sasa wana maduka makubwa ya Hardware na restaurants tele.

Mwanamke fulani aliimba nyimbo kuhusu kupujunwa uroda na mume wake. Nimempenda jamaa 'Springer' ambaye ni jirani yetu hapa Blowing Point. Aliimba wimbo ambayo ilisema aliweza kutabiri kuwa kutakuwa na amani dunia nzima siku moja.

Lakini ajabu, jamaa fulani aliimba nyimbo kuhusu uchaguzi wa hivi karibuni hapa kisiwani. Walitoa bango ya waziri mkuu na kuitumia katika wimbo! Nilishutuka, nikamwuliza mtu aliyekaa karibu na mimi ni nani huyo? Khaa! Jamani, kumbe nilikaa naye kwenye ferry kutoka Anguilla. Nilijua ni mtu wa maana jinsi watu walivyouwa wanamsalimia, lakini sikujua kamani waziri mkuu! Hakuwa na mbwembwe zile kama Bongo, mkubwa kubebewa begi, walinzi kibao, nk. Tena aliniomba kuazima kalamu kwa ajili ya kujaza fomu ya uhamiaji, lakini mtu mwingine alikuwa ameaimza. Yeye ndo alikuja kakaa na mimi na tulikuwa tunaongea, na nilitaka kumwuliza kama ana ndugu a shemeji yangu lakini sikumwuliza. Nadhani alijua mimi sikumtambua.

Habari zaidi baadaye.

Mnaweza kusoma habari za Anguilla Festival 2010 hapa:

http://www.axasummerfestival.com/results.php?eventID=24

5 comments:

Anonymous said...

Da chemi, kuuliza si ujinga. Anguilla Iko wapi?

emu-three said...

Kama visa vya Shabani Robert ehe, na uvaaji wao ukoje, kwani kama wanaongea pua kama pua basi basi hata macho hayana miwani etiiii

Chemi Che-Mponda said...

LOL! Anonymous wa 11:19Am Anguilla ni moja wa Leeward Islands. Inatawaliwa na Uingereza. Inatazama na St. Maarten, ni jirani na visiwa vya St. Kitts & Nevis, na St. Bartholomew. Kwa ujumla iko Carribean. Hata mdogo wangu aliponiambia kuwa ana boyfriend kutoka huko, ikabidi niulize iko wapi, na nitazame ramani!

Stephan said...

:))))))))

Anonymous said...

DA CHEMI NAOMBA MSAADA WAKO.
ULIWAHI KUPOST WEB SITE YA MUZIKI ILIKUWA NZURI SANA.NILLISAVE ILA NILISAFISHA COMPUTER YANGU NIKAPOTEZA KILA KITU.NAOMBA UIPOST TENA.PLZ PLZ PLZZZZZZ.