Wadau, nafurahi kuwatangazia kuwa niko katika sinema mpya, Here Comes the Boom. Stelingi wake ni mwigizaji maarufu Kevin James. Mtaniona katika scenes za darasa la Uraia. Niligiza kama moja wa wanafunzi watu wazima wanaotafuta uraia wa Marekeni. Wanasoma kwa ajili ya mthiani wa uraia.
Katika sinema hii, Kevin James anaigiza kama Mwalimu Voss ambaye anakuwa mpiganiaji wa MMA (Mixed Martial Arts) ili kutafuta hela ya kuokoa somo la muziki katika shule yake. Kwa vile bajeti ya shule inapungukiwa Mwalimu mkuu anaamua kufuta somo la muziki. Kwa maana hiyo hata mwalimu wa muziki ambaye ni rafiki yake, atakosa kazi.
Nilienda kuiangalia jana na nilifurahi sana kujiona. Yaani nimeigiza katika sinema nyingi za Hollywood na mara nyingi scene inakatwa, au unaniona sekunde! Lakini hii nimeonekana vizuri tu.
Showing posts with label Background. Show all posts
Showing posts with label Background. Show all posts
Sunday, October 14, 2012
Subscribe to:
Posts (Atom)



