Showing posts with label Here Comes the Boom. Show all posts
Showing posts with label Here Comes the Boom. Show all posts

Tuesday, January 22, 2013

Mimi Katika Sinema Here Comes the Boom

Haya wadau, katika sinema, Here Comes the Boom, niliigiza kama moja wa wanafunzi wa darasa la watu wazima wanaotafuta uraia wa Marekani. Darasa ilikuwa inafundishwa na Mr. Voss (Kevin James) ambaye anatafuta hela zaidi ya mshahara wake kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa muziki katika shule ya sekondari anayofundisha.  Mimi nilikuwa background actor, hivyo siongei. Nimefananikiwa kupata picha za scenes zangu.








Sunday, October 14, 2012

Niko katika Sinema - Here Comes the Boom

Wadau, nafurahi kuwatangazia kuwa niko katika sinema mpya, Here Comes the Boom.  Stelingi wake ni mwigizaji maarufu Kevin James.  Mtaniona katika scenes za  darasa la Uraia. Niligiza kama moja wa wanafunzi watu wazima wanaotafuta uraia wa Marekeni. Wanasoma kwa ajili ya mthiani wa uraia.

Katika sinema hii, Kevin James anaigiza kama Mwalimu Voss ambaye anakuwa mpiganiaji wa MMA (Mixed Martial Arts) ili kutafuta hela ya kuokoa somo la muziki katika shule yake. Kwa vile bajeti ya shule inapungukiwa Mwalimu mkuu anaamua kufuta somo la muziki. Kwa maana hiyo hata mwalimu wa muziki ambaye ni rafiki yake, atakosa kazi.

Nilienda kuiangalia jana na nilifurahi sana kujiona.  Yaani nimeigiza katika sinema nyingi za Hollywood na mara nyingi scene inakatwa, au unaniona sekunde! Lakini hii nimeonekana vizuri tu. 

Tuesday, March 01, 2011

Ukitaka kuigiza Katika Sinema Hii ni Nafasi Yako!

Kama unataka kuwa Extra katika sinema, 'Here Comes the Boom' jiandikishe na Boston Casting. Lazima uwe na makaratasi. Utalipwa dola $100 kwa siku au zaidi kutegemeana na masaa unaokaa kwenye set. Pia kuna chakula na vinywaji tele. Sinema inakuwa filmed Maeneo ya Quincy, MA.



UPDATE - MORE VENUES!

Here Comes the Boom- OPEN CALLS!

Open Call for the film “Here Comes the Boom” starring Kevin James. We are looking for people of ALL TYPES (ages 18+) to be extras on the film that is shooting late March- Early June.
Please feel free to come to any of our open calls- you only need to attend one! Make sure to bring a photo!


OPEN CALL SCHEDULE:

Saturday March 5th
10am- 3pm
North Quincy High School
316 Hancock Street
Quincy, MA 02171

Saturday March 12th
10am- 3pm
Quixote Studios
184 Everett Street
Boston, MA 02134

Sunday March 20th
10am- 3pm
Burlington Mall
Middlesex Turnpike #130
Burlington, MA 01803

Sunday March 20th
10am- 3pm
VFW Lowell
190 Plain Street
Lowell, MA 01852

Saturday March 26th
10am- 3pm
South Shore Casting Studio
Hanover Mall
1775 Washington Street
Hanover, MA 02339

Please do not call venues directly, all questions should be directed to Ashley at Boston Casting 617-254-1001 ext. 3