Sunday, October 14, 2012

Niko katika Sinema - Here Comes the Boom

Wadau, nafurahi kuwatangazia kuwa niko katika sinema mpya, Here Comes the Boom.  Stelingi wake ni mwigizaji maarufu Kevin James.  Mtaniona katika scenes za  darasa la Uraia. Niligiza kama moja wa wanafunzi watu wazima wanaotafuta uraia wa Marekeni. Wanasoma kwa ajili ya mthiani wa uraia.

Katika sinema hii, Kevin James anaigiza kama Mwalimu Voss ambaye anakuwa mpiganiaji wa MMA (Mixed Martial Arts) ili kutafuta hela ya kuokoa somo la muziki katika shule yake. Kwa vile bajeti ya shule inapungukiwa Mwalimu mkuu anaamua kufuta somo la muziki. Kwa maana hiyo hata mwalimu wa muziki ambaye ni rafiki yake, atakosa kazi.

Nilienda kuiangalia jana na nilifurahi sana kujiona.  Yaani nimeigiza katika sinema nyingi za Hollywood na mara nyingi scene inakatwa, au unaniona sekunde! Lakini hii nimeonekana vizuri tu. 

6 comments:

emu-three said...

Duuh, ningefurahi kuiona, tupo pamoja mpendwa

Anonymous said...

Kudos! You go girl!

Anonymous said...

Da Chemi, the next time ukija Bongo nakushauri uandae semina kwa ajili ya waigizaji wetu. Nina hakika kuna mambo mengi sana wanaweza kujifunza kutoka kwako. Nyingi ya sinema za Bongo ni vichekesho vitupu. Yaani mwanamke anaonekana anaamka asubuhi lakini usoni ana makeup, au mtu aliyekuwa tajiri sana anaonyeshwa kafilisika lakini bado anang'aa na kichwani ana wave na vidoleni pete lukuki za dhahabu. Kwa umaarufu ulionao, nadhani sponsorship haitakuwa tatizo.

Chemi Che-Mponda said...

Asante anymous wa 6:09AM. Naweza kuandaa hiyo semina. Ni kweli ujuzi ninayo. Je, watasiliza? Kuna wakati nilitoa ushauri kwa Staa fulani nikaambiwa eti nina wivu! (Mbavu sina). Pia Bongo Supastaa's watakuwa tayari kusikiliza maana naona wengi wanajiona kuwa wamefika. Wakati hapa Hollywood ni learning process, hata kama ukifika ni lazima uendelee kujifunza. Mfano Will Smith na mke wake walienda Uingereza kushiriki katika michezo ya kuigiza ingawa ni Superstars hasa.

Mimi kama mwanachama wa SAG-AFTRA, inabidi nioneyeshe kwenye resume kuwa nimeshirki katika michezo ya kuigiza, nimesoma darasa. Siyo nakaa nasema oh nimefika! Mfano mwaka huu niliamua kusomea mambo ya kuigiza katika matangazo. Hapa hakuna kufika.

Anonymous said...

Da Chemi hebu wapashe! Kuna supastaa fulani aliringa kweli siku ya kushuti filamu fulani. Gari ilifika nyumbani kwake saa 1 asubuhi kumchukua lakini hakutoka hadi saa 3 na nusu. Kasema yeye ni supastaa na anafanya kazi kwa taimu yake!

Anonymous said...

Chemi, mimi si mpenzi wa filamu za Bongo na sijawahi hata siku moja kununua DVD ya sinema ya Kibongo. Hata hivyo, kuna siku nililazimika kuangalia filamu mbili za Kibongo mwanzo hadi mwisho. Sikua na jinsi kwa kuwa sinema hizo zilikuwa zinaonyeshwa katika basi nililokuwa nasafiria kutoka Arusha kwenda Dar. Kwa kweli nilichikiona kilinikatisha tamaa kabisa na ninashangaa unaposema kuwa waigizaji wa filamu za Bongo hawataki kujifunza kwa kuwa wanajiona ni ma-celebrity