Showing posts with label Detroit. Show all posts
Showing posts with label Detroit. Show all posts

Sunday, December 27, 2009

MNigeria Mgaidi!


Bila shaka mmesikia habari za kijana wa KiNigeria, Umar Farouk Abdulmutallab, aliyejaribu kulipua ndege ikitua Detroit siku ya Krismasi. Kama angefanikiwa ingekuwa pigo kubwa.

WaNigeria na familia ya jamaa wanasema wanaona haya na jamaa amechafua jina la Nigeria! Mimi nasema kachafua jina la Afrika kwa ujumla! Lakini jamani, huyo kijana ni mtoto wa tajiri, millionea. baba yake alikuwa mkuu wa benki. Sidhani kama katika maisha yake amekuwa na uhaba wa pesa au njaa. Akitaka ananunuliwa, tena mtoto wa kiume! Lazima familia yake walimwoanesha upendeleo fulani. Halafu anaamua kufanya kitendo cha kigaidi. Kwenye taarifa ya habari wanasema Nigeria imejaa maskini na huyo kijana kweli alikuwa na maisha ya kifahari.

Inasikitisha. Ubaya zaidi kitendo chake kitafanya waNigeria na waafrika kwa ujumla kupata shida zaidi wakati wa kuomba visa za kuja Marekani. Pia watachunguzwa zaidi wakisafiri kwenye ndege.

Habari zinasema kuwa baba yake mzazi Umar, Al Haj Umaru Mutallab, alipeleka taarifa kwenye ubalozi wa Marekani huko Lagos, kuwa alikuwa na hofu kuwa mwanae ameingia kwenye kikundi cha kigaidi. Naona baba yake ni shujaa ingawa waMarekai walizembea. Lazima kilimwuma kuona mwanae anafanya maajabu, lakini aliona umuhimu wa kulinda maisha ya wengine.

Na mimi sasa nachukia kuwa kusafiri kwa ndege itazidi kuwa shida sasa. Utakaguliwa kila kona mpaka chooni sasa! Mwisho itabidi uvue mpaka chupi!

Kwa habari zaidi someni:

Wednesday, July 02, 2008

Bongoland II itaonyeshwa Zanzibar, Detroit na Chicago


Wadau, nimepata habari kuwa sinema Bongoland II itaonyeshwa hivi karibuni kwenye tamasha la sinema huko Zanzibar. Tarehe kamili sijajua.

Pia itaonyeshwa hapa Marekani kwenye miji ya Detroit (Agosti) na Chicago.

Nitawapa updates nikipata.