Showing posts with label Eve Ensler. Show all posts
Showing posts with label Eve Ensler. Show all posts

Tuesday, March 15, 2011

Mimi katika Mchezo- 'The Vagina Monologues'

Washiriki wa Boston Community Production of The Vagina Monologues 2011

Wikiendi iliyopita nilishiriki katika Mchezo wa Kuigiza, The Vagina Monologues (Maongezi ya Uke ..nishahishe kama nimekosea kutafsiri).

Kila mwaka vikundi vya wanawake hapa Marekani na nchi nyingi duniani wanasoma na kuigiza huo mchezo mwezi Machi. Hela wanazopata kutoka kwenye viingilio na mauzo ya chakula zinakwenda kusaidia vyama, mashirika yanayosaidia akina mama. Machi ni mwezi ya Wanawake duniani.

The Vagina Monologues ni hadithi fupi mbalimbali zinazotokana na mahojiano aliyofanya Bi Eve Ensler na wanawake kadhaa kuhusu nyeti zao. Kulikuwa na maongezi ya Bi Kizee, Shoga, Mke, Uke uliyokasirika, Mwanamke aliyedhani kapoteza kiharage chake, Kubalehe, Kubakwa, Kutairiwa, na mengine.

Kwa kweli nimetokea kufurahia huo mchezo na hata wanaume niliyowaalika waliyoenda wameipenda sana. Imewafanya wafikirie haki za akina mama na pia jinsi akina mama wanavyoona maswala kama uke zao, ngono, kunyanyyawa kijinisia.

Tanzania kuna hadithi nyingi sana ambazo zinaweza kuingizwa katika huo mchezo.

Mnauliza niliongelea nini? Nililionogelea uzazi, jinsi mwanamke anavyokuwa na uchungu katika uzazi na jinsi uke unavyofunguka ili mtoto atoke.