Tuesday, March 15, 2011

Mimi katika Mchezo- 'The Vagina Monologues'

Washiriki wa Boston Community Production of The Vagina Monologues 2011

Wikiendi iliyopita nilishiriki katika Mchezo wa Kuigiza, The Vagina Monologues (Maongezi ya Uke ..nishahishe kama nimekosea kutafsiri).

Kila mwaka vikundi vya wanawake hapa Marekani na nchi nyingi duniani wanasoma na kuigiza huo mchezo mwezi Machi. Hela wanazopata kutoka kwenye viingilio na mauzo ya chakula zinakwenda kusaidia vyama, mashirika yanayosaidia akina mama. Machi ni mwezi ya Wanawake duniani.

The Vagina Monologues ni hadithi fupi mbalimbali zinazotokana na mahojiano aliyofanya Bi Eve Ensler na wanawake kadhaa kuhusu nyeti zao. Kulikuwa na maongezi ya Bi Kizee, Shoga, Mke, Uke uliyokasirika, Mwanamke aliyedhani kapoteza kiharage chake, Kubalehe, Kubakwa, Kutairiwa, na mengine.

Kwa kweli nimetokea kufurahia huo mchezo na hata wanaume niliyowaalika waliyoenda wameipenda sana. Imewafanya wafikirie haki za akina mama na pia jinsi akina mama wanavyoona maswala kama uke zao, ngono, kunyanyyawa kijinisia.

Tanzania kuna hadithi nyingi sana ambazo zinaweza kuingizwa katika huo mchezo.

Mnauliza niliongelea nini? Nililionogelea uzazi, jinsi mwanamke anavyokuwa na uchungu katika uzazi na jinsi uke unavyofunguka ili mtoto atoke.

5 comments:

Anonymous said...

niliwahi kuhudhuria mchezo kama huu hapa tanzania, nadhani katika tamasha la jinsia pale TGNP, 2009. Ilikuwa ni nzuri sana, ila bado kuna nafasi ya kuzifanya onyesho kama hizi hapa kwetu, dada na wadau hilo haliwezekani? na sisi tunahitaji kitu kama hiki kwa mwingi..

godfather said...

Hongera Da Chemi! Nami nilienda kwenye mchezo New York. Ingekuwa vizuri na Tanzania wawe na Monologues kutoka kila mkoa.

Anonymous said...

Mtapigwa mawe Bongo!

Anonymous said...

dada nimefurahi sana kama nawe ni mshiriki katika michezo hiyo kweli wewe ni mwanaharakati. Ukeketaji unamaliza, ndoa za utotoni na mimba za utotoni zinamaliza watoto wa kabali za wafugaji nchini. Tunaomba mikanda hiyo kama inagusia ukatili huo iwe na tafsiri ya kiswahili

Chemi Che-Mponda said...

Anony wa 10:51PM, asante. Kulikoni kutafsiri nadhani ingekuwa vema tuandike tu za Tanzania. Hizi za hapa zinafaa utamaduni wa Marekani. Ila waliweka moja kuhusu vita vya Bosnia na nikasema wanawake wa Congo wana hadithi hiyo hiyo ya kuharibiwa uke zao kwa kutiwa bunduki.