Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbogwe, (kulia), Elias Kayandabila, akizungumza na waandishi wa habari, walioongozana na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) pamoja na Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) waliopo mkoani Geita kwa ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani.
Showing posts with label Geita. Show all posts
Showing posts with label Geita. Show all posts
Saturday, May 27, 2017
Ucheleweshaji wa Pembejeo Umetajkwa Kuporomosha Kilimo Mkoani Geita
UCHELEWESHAJI WA PEMBEJEO UMETAJWA KUPOROMOSHA KILIMO CHA PAMBA WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA
Saturday, June 28, 2014
Ujambazi Geita
Nimepokea taarifa hizi kwa Email:
Taarifa kutoka kwa mdau S.A.
June 24, 2014
Taarifa kutoka kwa mdau S.A.
June 24, 2014
Wadau,
Jioni ya leo majambazi
wamempiga risasi mbili kifuani na tumboni mfanyabiashara maarufu kwa
jina la Warwa na inasemekana amefariki dunia papo hapo kwenye duka lake
la uwakala wa mitandao ya kutuma na kupokea pesa maarufu kama mpesa,
airtel money na tigo pesa lililopo soko kuu kwenye barabara ielekeayo
kwenye benki za nmb, nbc na posta.
Mpaka sasa mji wa Geita
umekumbwa na taharuki kubwa kutokana na tukio hilo. Mpaka kufikia saa
mbili usiku huu bado kulikuwa na makundi ya watu wengi kwenye eneo la
tukio na kwenye maeneo ya hospitali kuu ya wilaya ya Geita.
Inasikitisha sana maana
inasemekana kuwa pamoja na polisi kuwa karibu na eneo hilo lakini
majambazi hao wamefanikiwa kutoroka kwa kutumia pikipiki. Vishindo vya
risasi zinazoamika kumuua ndugu Warwa vilisikika mbali kutoka kwenye
eneo hilo la tukio.
SA.
************************
June 25, 2014
Wadau,
Taarifa zilizopo Geita
zinaoonyesha kuwa majambazi hao waliuwawa jana ile ile, walipoondoka na
pikipiki, walikuwa wakifuatwa kwa nyuma kwa mbali na madreva pikipiki
ambao waliwatonya polisi uelekeo walikokuwa wanakimbilia!
Inasemekana walikuwa
wanakimbilia uelekeo wa Nyang'wale, polisi wa Geita wakawajulisha wenzao
wa Nyang'wale ambao nao wakawatangizia hao jamaa barabarani na kuwaua.
Utambuzi wa maiti za majambazi
hao wawili ulionyesha kuwa mmojawapo ni mpwa wa marehemu aliyevamiwa na
kuuwawa! Na hii ni baada ya dada wa Warwa kumtambua kijana huyo kuwa ni
mwanae!
Habari zaidi zinasema kuwa,
kabla ya kupigwa risasi zile kifuani na tumboni, marehemu Warwa
alimtambua mpwa wake huyo na kutamka kuwa, "....hata wewe .....
umejiunga na ujambazi kuja kunivamia mimi mjomba wako?", na huenda hiyo
ilikuwa sababu ya kuuwawa kule na kijana huyo!
Taarifa zilizopo hapa Geita
zinasema jana hiyo hiyo, ndani ya muda mfupi sana, kulikuwa na matukio
mawili ya ujambazi, hilo la hapo kwa marehemu Warwa na jingine kwa
mfanyabiashara wa jumla wa bia ndugu Inyasi, ambaye yeye hakukutwa
dukani bali mke wake na watu wengine. Hapo waliishia kupora fedha na
bostora iliyokuwemo kwenye droo na kukimbilia kusikojulikana.
Haijajulikana kama matukio haya
yalifanywa na watu walewale au tofauti, lakini inasemekana yana
uhusiano. Inasemekana kiasi kikubwa cha fedha kiliporwa, na wadau
wanatonya kuwa huenda pesa hiyo ilikuwa ni zaidi ya shilingi mil. 50!
SA.
Tuesday, March 08, 2011
Majita Inakuhitaji Sasa
ITIKIA WITO: MAJITA INAKUHITAJI SASA!
Tumia utaalamu na uwezo wako wa uelevu wa hali halisi ya Majita, kuihudumia Majita, kwa maslahi ya Majita!
Nani? Wewe unayetoka Majita, Musoma, popote pale ulipo – hasa uliyestaafu.
Sababu? Kuiendeleza sehemu ya Majita ukijitolea katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kupanua na kutathimini mradi-kusudiwa wa maendeleo–ambatana, ambao utakuwa ni ‘not-for-profit NGO’: Majita Integrated Rural Development Initiative.
Ujuzi? Dini, Kilimo, Komputa, Madini, Maji, Mazingira, Menejimenti, Miundombinu, Mistu, Nishati, Sheria, Takwimu, Ualimu, Uandishi/Utangazaji, Uchukuzi/Usafirishaji, Udaktari/Afya, Ufugaji, Ufundi/Ujenzi, Uhasibu, Ukarani, Upishi, Utalii, Utamaduni, Uvuvi . . . . na kadhalika.
Lini? Mara moja . . . . Sasa hivi . . . . Leo!
Wapi? Ki-jadi, walipanga, walibuni, walitekeleza, walipanua na walitathimini mikakati kama hii, wakikutana uso kwa uso wakikaa chini ya mti (orality culture). Wakati wa mashini (industrial culture), wanagawana umbali wa kusafiri na kukutana katikati ya nchi ( Canberra , Lilongwe , Rawalpindi , Brasilia, Dodoma ). Tulio na bahati ya mtandao (digital culture), tumewezeshwa kufanikiwa kukutana ‘instantaneously’, kana kwamba tumo katika ‘global village’.
E-Mail? romuinja@yahoo.com (au) MUJUNGU@unhcr.org
Omurimu ogukomera gutakorelwe!
Bhamugaire, najayo!
‘If it is to be, it is up to me.
Subscribe to:
Posts (Atom)


