Saturday, June 28, 2014

Ujambazi Geita

Nimepokea taarifa hizi kwa Email:

Taarifa kutoka kwa mdau S.A.

June 24, 2014

Wadau,
Jioni ya leo majambazi wamempiga risasi mbili kifuani na tumboni mfanyabiashara maarufu kwa jina la Warwa na inasemekana amefariki dunia papo hapo kwenye duka lake la uwakala wa mitandao ya kutuma na kupokea pesa maarufu kama mpesa, airtel money na tigo pesa lililopo soko kuu kwenye barabara ielekeayo kwenye benki za nmb, nbc na posta.
Mpaka sasa mji wa Geita umekumbwa na taharuki kubwa kutokana na tukio hilo. Mpaka kufikia saa mbili usiku huu bado kulikuwa na makundi ya watu wengi kwenye eneo la tukio na kwenye maeneo ya hospitali kuu ya wilaya ya Geita.
Inasikitisha sana maana inasemekana kuwa pamoja na polisi kuwa karibu na eneo hilo lakini majambazi hao wamefanikiwa kutoroka kwa kutumia pikipiki. Vishindo vya risasi zinazoamika kumuua ndugu Warwa vilisikika mbali kutoka kwenye eneo hilo la tukio.
SA.

************************

June 25, 2014

Wadau,
Taarifa zilizopo Geita zinaoonyesha kuwa majambazi hao waliuwawa jana ile ile, walipoondoka na pikipiki, walikuwa wakifuatwa kwa nyuma kwa mbali na madreva pikipiki ambao waliwatonya polisi uelekeo walikokuwa wanakimbilia!

Inasemekana walikuwa wanakimbilia uelekeo wa Nyang'wale, polisi wa Geita wakawajulisha wenzao wa Nyang'wale ambao nao wakawatangizia hao jamaa barabarani na kuwaua.
Utambuzi wa maiti za majambazi hao wawili ulionyesha kuwa mmojawapo ni mpwa wa marehemu aliyevamiwa na kuuwawa! Na hii ni baada ya dada wa Warwa kumtambua kijana huyo kuwa ni mwanae!

Habari zaidi zinasema kuwa, kabla ya kupigwa risasi zile kifuani na tumboni, marehemu Warwa alimtambua mpwa wake huyo na kutamka kuwa, "....hata wewe ..... umejiunga na ujambazi kuja kunivamia mimi mjomba wako?", na huenda hiyo ilikuwa sababu ya kuuwawa kule na kijana huyo!
Taarifa zilizopo hapa Geita zinasema jana hiyo hiyo, ndani ya muda mfupi sana, kulikuwa na matukio mawili ya ujambazi, hilo la hapo kwa marehemu Warwa na jingine kwa mfanyabiashara wa jumla wa bia ndugu Inyasi, ambaye yeye hakukutwa dukani bali mke wake na watu wengine. Hapo waliishia kupora fedha na bostora iliyokuwemo kwenye droo na kukimbilia kusikojulikana.
Haijajulikana kama matukio haya yalifanywa na watu walewale au tofauti, lakini inasemekana yana uhusiano. Inasemekana kiasi kikubwa cha fedha kiliporwa, na wadau wanatonya kuwa huenda pesa hiyo ilikuwa ni zaidi ya shilingi mil. 50!
SA.

1 comment:

Anonymous said...

Poleni sana Geita. This is a failed state. A dysfunctional government. A a jungle of ruthless wolves.

Ukiona wananchi wanaishi kwa hofu bila amani katika nchi yao basi ujue taifa hilo liko ukingoni kucollapse.

Jana sister kauawa mchana kweupe pale Ubungo, Dar es Salaam, lakini hakuna atakaye kamatwa, na baada ya wiki tutasahau kama vile hakijatokea kitu.

Leo Geita. Usiku huu hatuji wapi na nai atakufa. Na kesho hivyo hivyo.. Lakini hakuna anayesema neno wala kuinua sauti kusema "enough is enough"

Hakuna aliye salama isipokuwa wale wenye madarka, pesa, na wote wanoishi kama wafalme kwa kodi zetu.

Badala ya kutulinda, wanajilinda wao na familia zao. Polisi wetu si kwa ajili yetu bali kwa wajili ya wenye pesa, tena pesa zinazotokana na jasho letu.

Sisi ki vyetu na wao kivyao. Tutaendelea kuchinjwa na kutiwa vilema mmoja baada ya mwingine, huku wao wakihubiri "nchi hii ni ya 'utulivu' na 'amani'

Nani katulia?

Nani ana amani?

Ni wale wanaolindwa na polisi wetu huku wengine tukiuawa bila wahalifu kuchukua hatua! (where the culture of impunity rules, everyone is a king of lawlesness)

Halafu bado watanzania tunacheka. Tunawashangilia. Na wengine ndio kwanza wanashabikia upuuzi upuuzi wa watu wenye sare za kijani.

Tumelaaniwa?