Showing posts with label Godwin Kaduma. Show all posts
Showing posts with label Godwin Kaduma. Show all posts

Tuesday, October 02, 2007

Mazishi (Funeral) ya Mzee Godwin Kaduma Iringa









Msanii mkongwe, Mzee Godwin Kaduma, aliyefariki dunia wiki iliyopita amezikwa kwao, Itamba, Iringa.

Mungu amlaze mahali pema mbinguni. AMEN

REST IN ETERNAL PEACE.

Friday, September 28, 2007

Heshima za Mwisho - Mzee Godwin Kaduma (1938-2007)

Prof. Saida Othman (kulia) Prof. Amandina Lihamba, Prof. Penina Mlama na Mama Thecla Mjatta wakiongea kabla ya heshima za mwisho kuanza.
Wazazi wangu Dr. Aleck Che-Mponda na Rita Che-Mponda wakiongea na Prof. Penina Mlama, Prof. Saida Othman na Prof. Amandina Lihamba.
Mama Thecla Mjatta (mwenye Scarf ya pinki) akiongea na waombolezaji wengine kabla ya shughuli za kuwaga Mzee Kaduma kuanza.


Mzee Masimbi akitoa maelezo kuhusu mipango ya mazishi. Mwili wa Mzee Kaduma ulipelekwa kwanza nyumbani kwake Bagamoyo halafu ulipelekwa Iringa kwa ajili ya mazishi.


Prof. Amandina Lihamba na Prof. Penina Mlama wakipita kutoa heshima za mwisho.

Mzee Masimbi akiwafariji Mama Thecla Mjatta na Prof. Penina Mlama

Thursday, September 27, 2007

Rest in Peace Mzee Godwin Kaduma (1938-2007)

Hapa Mzee Kaduma anajadili mambo ya filamu Tanzania.


Nimepata habari za kusikitisha sana. Mzee Godwin Kaduma amefariki dunia. Nilikuwa namfahamu miaka mingi sana, alikuwa na kipaji ya ajabu katika usanii. Ninalia. Mungu Amlaze mahali pema mbinguni. AMEN.

*****************************************************************************

Dear Friends,

Mzee Godwin Zilaoneka Kaduma is no longer with us. Godwin Kaduma passed away at the Muhimbili National Hospital this afternoon the 27th September 2007 due to a severe stroke. I will update you with the funeral arrangements once I get information from relatives. May God rest him in eternal peace!

Ghonche Materego.

CEO - EATI
27th September 2007

************************************************************************
Habari za kusikitisha zilizotufikia ni kwamba gwiji la sanaa za maonyesho nchini Tanzania Mzee Godwin Zilaoneka Kaduma hatunaye tena duniani.Habari hizo zinazidi kupasha kwamba mauti imemfika Mzee Kaduma katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa ajili ya matibabu zaidi.Alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kupooza(stroke).

Msiba upo nyumbani kwake Bagamoyo jirani na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo. Heshima za mwisho kwa walio Dar-es-salaam zitatolewa kesho (Ijumaa) saa nne asubuhi habari zaidi zinasema heshima za mwisho kwa marehemu mzee Kaduma kwa walio Dar es salaam zitatolewa kesho saa nne asubuhi hospitali ya Muhimbili kabla mwili wake kusafirishwa kwenda nyumbani kwake Bagamoyo na kisha baada ya kuagwa saa nane mchana utapelekwa kijijini kwake Itamba, Iringa, kwa mazishi.

Thursday, July 26, 2007

Mjue Msanii Mkongwe wa Bongo Mzee Godwin Kaduma

Mzee Kaduma akiburudika na sigara, huko akitoa mawaidha juu ya fani ya kutengeneza filamu. Mzee Kaduma alicheza kama Sekondo, katika sinema ya Arusi ya Mariamu. (1985)
http://www.grisgrisfilms.com/html/marriage_of_mariamu.html
Mzee Kaduma ndani ya Theater anayojenga. Anasema atakuwa anafundisha kozi za usanii hapo. Kwa kweli ni jengo safi sana. Bado haijaisha lakini.

Nilivyofika kwa Mzee Kaduma, niliburudika na soda baridi. Tulikuwa na manongezi marefu sana juu ya fani ya sinema Bongo, script development, na mambo mengi ya usanii. Nilifurahi sana siku hiyo kupata ushauri kuhusu filamu kutoka kwa Mzee Kaduma. Tulikuwa tumemwomba Mzee Kaduma acheza kama 'Uncle' kama sinema ya Bongoland II, lakini alikataa kutokana na majukumu mengine.


Mzee Kaduma na mbwa wake Tommy. Utashangaa Mzee Kaduma anavyoongea na Tommy na jinsi Tommy anayotii amri.



Hii ndo View kutoka backyard ya Mzee Kaduma.

Monday, May 21, 2007

Sinema ya Arusi ya Mariamu


Umewahi kuona sinema iitwayo, ‘Arusi ya Mariamu’? Sinema hiyo ilitengenezwa 1985 nchini Tanzania na Ron Mulvihill na marehemu Nangayoma Ng’oge.

Sinema hiyo ni fupi, dakika 36. Lakini ni hadithi tamu sana. Mariamu (Amadina Lihamba) ana funga ndoa na Sekondo (Godwin Kaduma). Wanapendana sana, lakini Mariamu anaanza kuugua ugonjwa ambao madaktari wanashindwa kumtibu. Sekondo anashauriwa ampeleke kwa mganga wa kienyeji atiibiwe. Huko inakuwa balaa maana kumbe Mariamu ana waoga wa waganga wa kienyeji. Kwani alishuhudia kifo cha baba yake ambaye naye alikuwa mganga wa kienyeji. Alifariki akikusanya mitishamba kwa ajili ya kutibu wagonjwa. Je, Mariamu atapona?

Sinema hiyo inapatikana http://www.grisgrisfilms.com/html/marriage_of_mariamu.html
Ron Mulvihill alirudi Tanzania 1994 kutengeneza sinema ya Maangamizi the Ancient One.