Showing posts with label Arusi ya Mariamu. Show all posts
Showing posts with label Arusi ya Mariamu. Show all posts

Saturday, August 13, 2011

Bibi Arusi Ashikwa na Uchungu Kanisani!

Makubwa. Habari kutoka Muheza, Tanga zinasema Bibi Arusi, Mariam Shabani, kashikwa na uchungu kanisani, na kupelekwa hospitalini na shela yake na kuzaa huko! Pole zake. Mama na mwana wako salama. Wanasema alikuwa na mimba ya mieza saba.

*****************************************************************
Kutoka Gazeti la Mwananchi:


Bibi harusi ashikwa uchungu, ajifungua kanisani Muheza
Thursday, 11 August 2011 21:16

Mwandishi Wetu, Muheza

BIBI harusi aliyefahamika kwa jina la Mariam Shabani, ameshikwa na uchungu wa kujifungua kanisani wakati akifungishwa ndoa na mchumba wake, aliyefahamika kwa jina la Deo Massawe.Tukio hilo lilitokea juzi Kanisa Katoliki lililopo maeneo ya Majengo Shimoni, wilayani Muheza, huku umati wa watu ukiwa umejaa ndani ya kanisa hilo ukiisubiri kufungwa kwa ndoa hiyo.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia tukio hilo ndani ya kanisa hilo, wakati Padri Martin Kihiyo, akiendelea na misa ya kufungisha ndoa hiyo, ghafla bibi harusi akiwa amevaa vazi rasmi la harusi, alianza kupiga kelele akidai anasikia uchungu wa kujifungua.

Hata hivyo, baada ya bibi harusi huyo kupiga kelele, Padri Kihiyo alisitisha misa hiyo na Mariamu kuchukuliwa haraka na kuwekwa kwenye gari huku akiwa hajiwezi hadi Hospitali Teule Muheza.Pia, Mariamu anafahamika kwa jina la Sada Shabani, baada ya kufikishwa hospitali alipelekwa chumba cha kujifungulia huku akiwa na vazi lake la harusi.

Baada ya kuhudumiwa Mariamu, alijifungua mtoto wa kike na kulazwa wodi ya Azimio wanakolazwa wazazi.
Mmoja wa muuguzi hospitalini hapo aliyeomba asitajwe, alisema bibi harusi huyo alijifungua njiti akiwa na miezi saba.Kwa upande mwingine, kwenye ukumbi ambao ulikuwa umeandaliwa kwa sherehe ya harusi hiyo, watu walikuwa wamekaa ndani wakisubiri maharusi bila kufahamu kilichokuwa kikiendelea.

Hata hivyo, kutokana na hali hiyo bwana harusi alilazimika kufunga ndoa na msichana mwingine wa pembeni kwa niaba ya bibi harusi, ili kuhalalisha sherehe hiyo huku bibi harusi mwenyewe akiwa hospitali analea.

Inasemekana Mariamu alianza kusikia uchungu akiwa saluni na aliwaeleza baadhi ya watu, lakini walimjibu kuwa huo ni woga wa harusi.Katika hatua nyingine, mbuzi wa ndafu aliyekuwa ameandaliwa alianguka chini kwenye mchanga.

Baadhi ya Wakristo walisikitishwa na tabia ya viongozi wa dini kuendelea kuwafungisha ndoa watu ambao wake zao wana mimba kwamba, ni aibu.

Tuesday, June 26, 2007

Mjue Msanii Thecla Mjatta

Thecla Mjatta in Arusi ya Mariamu
Thecla Mjatta at a screening of the film, Tumaini
Thecla Mjatta (in baibui) with other cast of the film, Mlima Kolero
(photo from Jiachie blog)


Mama Thecla Mjatta ni mwigizaji mkongwe wa Tanzania. Huenda mnakumbuka zile michezo za kuigiza kwenye redio. Tulikuwa tunazingojea kwa hamu kila wiki, hasa kwa vile wakati huo hakuna TV miaka ya 70 na 80. Pia aliigiza katika michezo ya kuigiza kadhaa.

TV ilivyoanza alianza kuigiza kwenye michezo ya television. Mama Thecla pia ameigiza katika sinema kadhaa na kucheza kama watu ambao hamwezi kusahau.

Katika sinema ya Arusi ya Mariamu, anaigiza kama shangazi yake Mariamu, na hamtasahau anvyopagawa.

Katika sinema ya Maangamizi the Ancient One aliigiza kama mama wa mhusika mkuu, Samehe. Samehe, alishuhudia kifo cha cha kuunguzwa na moto na baba yake mzazi amabaye alikuwa ni mchungaji mwenye imani kali ya dini. Sinema ya Maangamizi iliteuliwa kama sinema ya kwanza kutoka Tanzania, katika mshindano ya Oscars mwaka 2001 (Foreign Language category).

Pia ameigiza katika sinema za Simu ya Kifo, Tumaini, Mzee Mkude, na mlima Kolero. Hivi karibuni ataigiza katika sinema ya Bongoland II, akicheza kama mama yake mhusika mkuu, Juma.

Kwa habari zaidi za sinema ya Bongoland II nenda : http://www.kibirafilms.com/bongoland/home.html

Monday, May 21, 2007

Sinema ya Arusi ya Mariamu


Umewahi kuona sinema iitwayo, ‘Arusi ya Mariamu’? Sinema hiyo ilitengenezwa 1985 nchini Tanzania na Ron Mulvihill na marehemu Nangayoma Ng’oge.

Sinema hiyo ni fupi, dakika 36. Lakini ni hadithi tamu sana. Mariamu (Amadina Lihamba) ana funga ndoa na Sekondo (Godwin Kaduma). Wanapendana sana, lakini Mariamu anaanza kuugua ugonjwa ambao madaktari wanashindwa kumtibu. Sekondo anashauriwa ampeleke kwa mganga wa kienyeji atiibiwe. Huko inakuwa balaa maana kumbe Mariamu ana waoga wa waganga wa kienyeji. Kwani alishuhudia kifo cha baba yake ambaye naye alikuwa mganga wa kienyeji. Alifariki akikusanya mitishamba kwa ajili ya kutibu wagonjwa. Je, Mariamu atapona?

Sinema hiyo inapatikana http://www.grisgrisfilms.com/html/marriage_of_mariamu.html
Ron Mulvihill alirudi Tanzania 1994 kutengeneza sinema ya Maangamizi the Ancient One.