Showing posts with label Hurricane Ike. Show all posts
Showing posts with label Hurricane Ike. Show all posts

Monday, September 29, 2008

Haiti waangamizwa na Kimbunga... nani ana jali?


Wadau, naomba niwatolee mfano hai wa jinsi wazungu Marekani walivyo wabaguzi.

Bila shaka mmesikia habari ya jinsi vimbunga vilivyopiga visiwa vya Caribbean hivi karibuni, Kisiwa kilichoathjirika zaidi ni Haiti. Nashangaa hatusikii sana habari hizo. Mamia ya watu wamekufa huko.

Hatusikii kwa sababu Haiti ni taifa la weusi! Kingekuwa kisiwa cha wazungu tungesikia kwenye matangazo maombi ya michango ya kuwapelekea walioathirika misaada. Kungekuwa na airlift ya kuleta mayatima kulelewa hapa Marekani.

Mnakumbuka Tsunami iliyopiga Indonesia? Wale walichangiwa mapesa na kupelekewa misaada kibao.

Sasa ni wiki kadhaa tangu kimbunga kifanye maafa huko Haiti mbona hatusikii kitu? Kuna habari kuwa watu wanakufa shauri ya kukosa maji ya kunywa safi na chakula. Hapa Boston kuna maHaitian wanakusanya misaada ya kupeleka huko lakini ni ndogo sana kulinganisha na kama vile wangefanya kampeni ya kuomba umati wawachangie.

Husikii hata waandishi wa habari wakitangaza habari za Haiti.

Wadau, kisiwa cha Cuba na kiswa cha Haiti si mabli na Marekani. WaCuba wameonewa na Castro (wanavyodai). Wanaruhusiwa kukaa hapa Marekani bila maswali kama wanaweza kufika Marekani. WaHaiti nao wamenyanyaswa na Papa Doc na Baby Doc na wengine. Wengi wakifika Marekani wanarudishwa bila huruma. Hao waCuba ni weupe weupe. WaHaiti ni weusi. Ukienda kwenye kambi ya wakimbizi waHaiti huko Florida kina hali duni sana kulinganisha na cha waCuba!

Wadau, tuwaombee wananchi wa Haiti walioathirika na vimbunga. Mungu awalinde wasiteseke zaidi.
Kwa habari zaidi someni:

Friday, September 12, 2008

Wadau wa Texas - Mpo Salama?


Natoa pole kwa wadau wa Texas wanaopigwa na kimbunga Ike. Kweli Ike katua na hasira kali,imebidi watu wakimbie. Wanasema kuwa Houston itaathirika vibaya.

Yaani hizi kimbunga zimezidi kuwa kali. Hii inaweza kuwa kali kama ile Hurrican Katrina.