Monday, September 29, 2008

Haiti waangamizwa na Kimbunga... nani ana jali?


Wadau, naomba niwatolee mfano hai wa jinsi wazungu Marekani walivyo wabaguzi.

Bila shaka mmesikia habari ya jinsi vimbunga vilivyopiga visiwa vya Caribbean hivi karibuni, Kisiwa kilichoathjirika zaidi ni Haiti. Nashangaa hatusikii sana habari hizo. Mamia ya watu wamekufa huko.

Hatusikii kwa sababu Haiti ni taifa la weusi! Kingekuwa kisiwa cha wazungu tungesikia kwenye matangazo maombi ya michango ya kuwapelekea walioathirika misaada. Kungekuwa na airlift ya kuleta mayatima kulelewa hapa Marekani.

Mnakumbuka Tsunami iliyopiga Indonesia? Wale walichangiwa mapesa na kupelekewa misaada kibao.

Sasa ni wiki kadhaa tangu kimbunga kifanye maafa huko Haiti mbona hatusikii kitu? Kuna habari kuwa watu wanakufa shauri ya kukosa maji ya kunywa safi na chakula. Hapa Boston kuna maHaitian wanakusanya misaada ya kupeleka huko lakini ni ndogo sana kulinganisha na kama vile wangefanya kampeni ya kuomba umati wawachangie.

Husikii hata waandishi wa habari wakitangaza habari za Haiti.

Wadau, kisiwa cha Cuba na kiswa cha Haiti si mabli na Marekani. WaCuba wameonewa na Castro (wanavyodai). Wanaruhusiwa kukaa hapa Marekani bila maswali kama wanaweza kufika Marekani. WaHaiti nao wamenyanyaswa na Papa Doc na Baby Doc na wengine. Wengi wakifika Marekani wanarudishwa bila huruma. Hao waCuba ni weupe weupe. WaHaiti ni weusi. Ukienda kwenye kambi ya wakimbizi waHaiti huko Florida kina hali duni sana kulinganisha na cha waCuba!

Wadau, tuwaombee wananchi wa Haiti walioathirika na vimbunga. Mungu awalinde wasiteseke zaidi.
Kwa habari zaidi someni:

2 comments:

Anonymous said...

dada chemi,ngoja nikueleze kidogo kuhusu haiti.
kisa cha haiti na wazungu kilianza long time,

haiti is the first black nation to be independent in the world walipata uhuru wao mwaka 1804 baada ya slaves from africa kushinda vita dhidi ya slave masters( france) vita hii ilianza mwaka 1792, ushindi huu uliwashitua sana wamarekani weupe na wakafikiri kuwa wamarekani weusi wangeweza kufanya kitu kama hicho,kwahiyo hizo habari zilifichwa

kwa kuwa france ilipoteza the most profitable colony uchumi wao ukayumba, ikabidi wauze lousiana kwa marekani,je una habari kwamba mpaka leo haiti inalipa compansation kwa france sababu ya kupoteza colony lao.
unajua nini? we nenda kanunue kitabu hiki title .UNBROKEN AGONY author.randall robinson
halafu utaelewa what is going on.

Chambi Chachage said...

Dada Chemi unayoyasema kuhusu huu ubaguzi ni ya kweli kabisa. Ila mbona Wahaiti wamejaa sana pale mjini Miami mpaka kuna kamji kanaitwa 'Little Haiti', yaani ukifika hapo utasahu kuwa uko USA. Pia wametapakaa mpaka kule juu Massachusetts tena wengine mambo yao mswano/supa. Mimi nadhani inabidi tuache kuwalilia hawa Wamarekani na tutumie 'African diasporic power', yaani nguvu ya kutapakaa kwa Waafrika duniani, kusaidia watu wa asili ya Afrika hasa wale waliopo tunakotokea. Yaani kweli inabidi tusubiri Rahisi Kichaka atupe vijisenti vya petrodola wakati Watanzania wamejaa huko Wichita, Michiana na takribani miji yote ya Kiwanja wakiujenga uchumi tete wa Yuesiei?

Wahaiti wanaadhibiwa kwa sababu ni nchi ya kwanza ya 'mtu mweusi' aliyetawaliwa na 'mtu mweupe' kufanya mapinduzi yaliyofanikiwa. Kama waliweza kufanya mapinduzi hayo zaidi ya karne 2 zilizopita kwa nini wanashindwa kufanya hivyo leo? Uhuru/ukombozi wa kwanza wa watu wenye asili ya Afrika uliletwa na muungano wa mapambano ya watu wa asili ya Afrika waliotapakaa kote duniani - kina George Padmore, CLR James, Kwame Nkrumah na wengine - na ukombozi wa pili/tatu pia utaletwa na watu wa asili ya Afrika waliotapakaa kote duniani - kina Swahili Timers, Friends of Tanzania, USA Africa Dialogue na wengineo. Aluta Continua!Hasta la victoria siempre!Vinceremos!