Rais Obama na mke wake Michelle, wakielekea makazi yao mapya, WHITE HOUSE
The Obama's & The Biden's mara baada ya kuapishwa(Picha zote kutoka CNN.Com)
Wadau, leo mchana Senator Barack Hussein Obama, ameapishwa kuwa Rais Marekani. Alitumia jina lake kamili bila aibu. Wengi walisema atatumia Barack H. Obama kwa vile waMarekani wengi hawapendi jina la Hussein kwa vile inawakumbusha Uislamu na Saddam Hussein. Pongezi kwa Obama kwa kuheshimu jina aliyopewa na wazazi wake!
Sasa anaanza kazi ngumu ya kuwa Rais Marekani. Mungu ampe nguvu na amlinde yeye na famila yake.




