Wednesday, January 14, 2009

Bibi yake Obama Atakuwepo D.C.


Bibi yake Barack Obama, wa Kenya, Sarah Obama (86) yuko njiani kuja Marekani kwenye sherehe ya kumwapisha mjukuu wake kuwa Rais wa Marekani. Sherehe za kumwapisha zitakuwa jumanne ijayo 1/20/09.

Mungu ambariki na amlinde katika safari yake. Nadhani maishani mwake hakutegemea kuwa mjukuu wake atanyakua wadhifa mkubwa hivyo.

Mnaweza kuona video hapa:


Kwa habari zaidi someni:

4 comments:

Anonymous said...

Hiyo ndo inaitwa bahati. jioni unaenda kitandani kulala asubuhi unaamka milionea. miaka 86 pengine hata basi la kwenda mbali hakuwahi kupanda leo hii alikwaa pipa kwenda kukaa kwenye kiti ambacho hata wenye madigirii hawakikalii LOL Mungu amjalie saana

Anonymous said...

Mimi natabiri kuwa huyo bibi ataishi kuona miaka yote minane ya utawala wa mjukuu wake. Ataisha mpaka ana miaka 130!

Anonymous said...

Da' Chemi,
Link ya video haihusiani na habari hii...

Anonymous said...

Kwetu huko Mara kuna methali:

"Okwibhura ni okwiyungwa"!

"Kuzaaa ni kujisikiamo"!

Kiswahili na Kiingereza - hizi lugha mbili hazina maana kamili!

Hiyo ndiyo raha ya kuzaa!

Hiyo ndiyo faida ya kuzaa!