Saturday, June 26, 2010
Saturday, December 05, 2009
James Brown Atuma Salamu za Krismasi Kutoka Mbinguni
Wednesday, August 06, 2008
Wazee Vijana
Nilishangaa kuona idadi ya wazee pale klabuni waliopanda jukwaani! Kweli hapa Marekani Uzee ni akili yako tu.


Saturday, August 04, 2007
Kumbe James Brown ana watoto wengine!
Kumbe James Brown ana watoto wengine zaidi ya hao sita aliyowatambua. Asante DNA hao watoto wamethibitisha baba yao ni nani.
James Brown alifariki siku ya Krismasi mwaka jana. Katika wosia wake alitambua watoto wake sita. Huyo ambaye alizaa na mzungu, Tomi Rae bado hajapimwa DNA, lakini James Brown alidai kuwa siyo mwanae maana kipindi hicho alikuwa na matatizo na nguvu za kiume.
Watu 12 walijitokeza wakidai kuwa ni watoto wa marehemu James Brown. Wote walifanya testi ya DNA. Kati ya hao wawili waligundilika kuwa ni kweli ni watoto wake.
Moja wa watoto hao, ni Bi LaRhonda Petitt, ambaye sasa ana miaka 45. Majibu ya DNA yanasema kuwa 99.99 percent probability kuwa yeye ni mtoto wa Brown. Petitt anashukuru kuwa baba yake amaethibitishwa ila anasema kuwa ana masikitiko sana kuwa hakutambulika mapema na maisha yake yalikuwa magumu kutokana na ukosefu wa pesa. Anasema kuwa kila James Brown akionekana kwenye TV basi mama yake angesema, "Yule ni baba yako!"
Hao watoto huenda wakawa na haki ya kudai urithi kutoka estate ya James Brown.
Na hivi karibuni, asante DNA mtoto wa Spice Girl, Melanie Brown amegundulika kuwa ni mtoto wa mcheza sinema Eddie Murphy kama alivyodai.
Sasa huko Bongo wakianza kupima DNA mbona itakuwa ngoma kwa hao wanaume wenye mchezo wa kukataa watoto wao!
Kwa habari zaidi soma :
http://www.washingtonpost.com/wp-dyn/content/article/2007/08/04/AR2007080402520.html
Tuesday, December 26, 2006
Marehemu James Brown

REST IN PEACE JAMES BROWN
1933 - 2006
Jamani nilisikitika kusikia habari ya kifo cha Godfather of Soul, James Brown! Alifariki jana asubuhi, Krismasi, akiwa anaumwa Pneumonia. Lakini jamani Ijumaa mbona alionekana mzima, ana-sign autographs na kutoa zawadi za Krismasi kwa watoto!
Ukweli, mimi ni mmoja wa washabiki wake wakuu. Yaani kila nikisimikia animba 'funk' lazima niinuke na kucheza! Nyimbo zake, 'Say it Loud, I'm Black and Proud!', 'Hot Pants, 'Sex Machine', Get Up, na zingine nyingi haziwezi kusahaulika. Sasa kwa vile ni marehemu bei ya CD's zake zitaongezeka bei.
Nisiseme habari ya jinsi nilivyokuwa nashangalia akicheza na kutia madoido ya 'splits'! Nina mpaka mDoli wa James Brown, una bonyeza mahala na anaanza kucheza na kuimba ule waimbo wake wa 'I Feel Good!' (Najisikia vizuri). Tangu mdogo yaani miaka minne hivi nakumbuka kucheza na kupiga kelele kila nikisikia anaimba, eti najaribu kumwiga!
Mungu amlaze mahali pema mbinguni. Amen.