Jana jioni nilitembelea klabu fulani hapa Boston, inaitwa Slades. Siku za Jumanne wanakuwa na kama Karaoke, lakini unaimba na bendi laivu.
Nilishangaa kuona idadi ya wazee pale klabuni waliopanda jukwaani! Kweli hapa Marekani Uzee ni akili yako tu.
Kaka Jay C. anaijiona yeye ndiye marehemu James Brown Sasa. Lazima niseme anaimba kama James Brown anacheza kama yeye na cheki hiyo 'process' ya nywele kama James Brown! Kama wanatengeza sinema juu ya maisha ya James Brown huyu anafaa kuwa James Brown!