Showing posts with label Mussa Kissoky. Show all posts
Showing posts with label Mussa Kissoky. Show all posts

Friday, November 23, 2007

Sofia Productions wataandaa Fimbo ya Mnyonge Awards


Kampuni ya Sofia Productions, inayoshugulika na mambo ya filamu na muziki Tanzania imechaguliwa kuandaa tuzo za filamu Tanzania zitakazoitwa 'Fimbo ya Mnyonge Film Awards 'kutoka Baraza la Sanaa la Taifa. Naona ndo zitakuwa Oscars zetu Tanzania!

Habari hizo zimethibitishwa na meneja mkuu wa Sofia Productions, Bwana Musa Kissoky.

Tuzo hizo wanatarajia kuzifanya mapema mwakani kati ya mwezi March na April.

Kwa kweli fani ya sinema inashamiri siku hizi Tanzania, tunangojea kwa hamu kuona washindi wa Awards!

Monday, July 30, 2007

Sofia Records

CCrew ya Bongoland II wakiburudika na Coca-Cola nje ya ofisi za Sofia Records.

Sofia Records ni kampuni inayohusika na mambo ya filamu na muziki, inayomilikiwa na Bwana Mussa Kissoky. Makao makuu ya kampuni hiyo iko Mwananyamala Komakoma, mjini Dar es Salaam. Kampuni hiyo ilitoa mchango mkubwa katika kutengeneza filamu ya Bongoland II hasa kwa masuala ya Usafiri na kutafuta sehemu za kufanya filming (locations).

Kichekesho:


Kuna siku nilipanda hiyo gari ya Sofia Records kusudi tukanunue bidhaa fulani. Nilikaa kiti cha mbele.

Basi wakati tunangojea traffic kweneye ile barabara ya Mabibo kusudi tuingie Morogoro Road kijana aka approach gari. Aliniamkia vizuri. "Shikamoo Mama Sofia!" Huko nimesahau gari imeandikwaje, kwa mshangao niliitika,"Marahaba" maana sina mtoto ambaye anaitwa Sofia.

Kijana kaanza, "Mimi nina leseni ya kuendesha gari Grade C, na pia nimesomea udereva, naomba sana unitafutie kazi."

Huko bado nashangaa nikamwambia, "Sawa nikisikia kuna kazi sehemu nitakujulisha". Jamaa kanitajia na jina na wapi pa kumpata.

Basi tukaendelea na safari, ndo watu kwenye gari wakaniuliza kama nilielewa ilikuaje. Waliambia kuwa yule kijana alidhania mimi nahusika na hiyo kampuni na alikuwa anaomba kazi. Ama kweli jet lag kitu kibaya. Maana kama ningemwelewa mara moja ningemwambia mimi ni pasenja tu kwenye hiyo gari na salamu zake ningefikisha kwa mwenye hiyo kampuni.

Kwa sasa naona kijana kaona kuwa "Mama Sofia" kamwangusha.