Monday, July 30, 2007

Sofia Records

CCrew ya Bongoland II wakiburudika na Coca-Cola nje ya ofisi za Sofia Records.

Sofia Records ni kampuni inayohusika na mambo ya filamu na muziki, inayomilikiwa na Bwana Mussa Kissoky. Makao makuu ya kampuni hiyo iko Mwananyamala Komakoma, mjini Dar es Salaam. Kampuni hiyo ilitoa mchango mkubwa katika kutengeneza filamu ya Bongoland II hasa kwa masuala ya Usafiri na kutafuta sehemu za kufanya filming (locations).

Kichekesho:


Kuna siku nilipanda hiyo gari ya Sofia Records kusudi tukanunue bidhaa fulani. Nilikaa kiti cha mbele.

Basi wakati tunangojea traffic kweneye ile barabara ya Mabibo kusudi tuingie Morogoro Road kijana aka approach gari. Aliniamkia vizuri. "Shikamoo Mama Sofia!" Huko nimesahau gari imeandikwaje, kwa mshangao niliitika,"Marahaba" maana sina mtoto ambaye anaitwa Sofia.

Kijana kaanza, "Mimi nina leseni ya kuendesha gari Grade C, na pia nimesomea udereva, naomba sana unitafutie kazi."

Huko bado nashangaa nikamwambia, "Sawa nikisikia kuna kazi sehemu nitakujulisha". Jamaa kanitajia na jina na wapi pa kumpata.

Basi tukaendelea na safari, ndo watu kwenye gari wakaniuliza kama nilielewa ilikuaje. Waliambia kuwa yule kijana alidhania mimi nahusika na hiyo kampuni na alikuwa anaomba kazi. Ama kweli jet lag kitu kibaya. Maana kama ningemwelewa mara moja ningemwambia mimi ni pasenja tu kwenye hiyo gari na salamu zake ningefikisha kwa mwenye hiyo kampuni.

Kwa sasa naona kijana kaona kuwa "Mama Sofia" kamwangusha.

1 comment:

KakaTrio said...

DaChemi sasa mie mbona nachoka bure kuja huku halafu siipati hata picha kwenye posting zako? Weka picha Dada na sie tuzifaudu manake bongo ulisema internet ziko sloo sasa na bostoni ni slow pia au ndio rivesi jet lagi bado inakusumbua?