
Kuna nini ndani ya maji ya Texas inayofanya watu wanaoiinya kufanya vituko?
Leo kuna habari kuwa huko Tyler, Texas, jamaa fulani tena mmarekani mweusi, kamwua mpenzi wake, Jana Shearaer (21). Baada ya kumwua kamkatakata vipande, kachemsha vipande hivyo, na kuweka mezani pamoja na uma na kisu tayari kwa kula.
Polisi wanasema walivyofika nyumbani kwa, Christopher Lee McCuin (25), walikuta sufuria ya supu inachemka jikoni, juu ilikuwa inaelea sikio la bindamu. Mezani kulikuwa na kipande cha nyama ya binadamu iliyopikwa na uma ilikuwa ndani tayari kwa kula! DUH! Mauji na vituko vilivyofuata alifanya nyumbani kwa mama yake.
Christopher alimwita mama yake kuja kushuhudia alivyofanya, ndo mama yake alikimbia kwenda kuita polisi.
Polisi hawajui kama alimla sehemu au la. Itabidi kinyesi chake kipimwe.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema mbinguni. Amen.
Kwa vile hayo mauji yalitokea Texas, huyo Christopher atahukumiwa adhabu ya kifo.
Kwa habari zaidi someni: