Monday, January 07, 2008

Amwua na Kumpika Mpenzi wake


Kuna nini ndani ya maji ya Texas inayofanya watu wanaoiinya kufanya vituko?

Leo kuna habari kuwa huko Tyler, Texas, jamaa fulani tena mmarekani mweusi, kamwua mpenzi wake, Jana Shearaer (21). Baada ya kumwua kamkatakata vipande, kachemsha vipande hivyo, na kuweka mezani pamoja na uma na kisu tayari kwa kula.

Polisi wanasema walivyofika nyumbani kwa, Christopher Lee McCuin (25), walikuta sufuria ya supu inachemka jikoni, juu ilikuwa inaelea sikio la bindamu. Mezani kulikuwa na kipande cha nyama ya binadamu iliyopikwa na uma ilikuwa ndani tayari kwa kula! DUH! Mauji na vituko vilivyofuata alifanya nyumbani kwa mama yake.

Christopher alimwita mama yake kuja kushuhudia alivyofanya, ndo mama yake alikimbia kwenda kuita polisi.

Polisi hawajui kama alimla sehemu au la. Itabidi kinyesi chake kipimwe.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema mbinguni. Amen.

Kwa vile hayo mauji yalitokea Texas, huyo Christopher atahukumiwa adhabu ya kifo.

Kwa habari zaidi someni:
3 comments:

Anonymous said...

Wanawake bwana! Dawa yao kuwala nyama tu. Wasumbufu sana.

Dinah said...

Anony hapo juu, mtu akikusumbua iwe mwanamke au mwanaume si unaachana nae na kuendeshamaisha yako kivyako?

Mpenzi anapatikana popota na wakati wowote ukitaka lakini uhai haupatikani namna hiyo.

Huyo bwana lazima alikuwa na matatizo ya akili au huko Marekani kuna mapepo sugu/tukutu mana'ke wamarekani weusi kwa weupe hufanya mambo ya ajabu sana kwa wanawaita "wapenzi wao".

Mara mtua toke na mkwe wake, mara atembee na baba'ke, mara apendwe namdogo mtu....maisha gani hayo?

Tukijakwenye vifo ndio sina hata la kusema, wakati naishi Ulaya nilikuwa napenda sana kuangalia kipindi cha "Crime and invetigation" na hapo nikajifunza mambo mengi sana kuhusiana na Sheria za wenzetu, ufuatiliaji wa keshi, uchunguzi na mauaji ya wa marekani(well wanazungumzia nchi nyingi) lakini US inaongoza.


I hope Bongo hatutofikia huko, japo tayari kuna mauwaji ya kikatili kwa wanaodhaniwa/tuhumiwa wachawi au wachawi.

Daima said...

mambo ya Texas hayo, mwaka jana kuna mwingine alimkata girlfriend wake kila kiungo cha mwili na kumchoma kwenye bbq Grill, it was in the news, Siiiick!!!