Showing posts with label Robert De Courcey Stringer. Show all posts
Showing posts with label Robert De Courcey Stringer. Show all posts

Thursday, August 20, 2009

Mzungu Auwawa Zanzibar

Mazishi yalifanyika huko Ireland juzi , ya Robert De Courcey Stringer (26). Alikutwa kwenye ufukwe wa Zanzibar tarehe 8/8/09 akiwa amepigwa kichwani na kuibiwa mali yake. Alikuwa Zanzibar akifanya kazi na mradi wa 'Camara' ambayo ina gawa computer zilizotumika (second hand) na teknolojia zingine kwa watu. Hivi huko Zanzibar siku hizi kuna nini? Zamani ulikuwa husikii habari ya wizi.

Mwaka jana wageni wa Cristal Resort walivamiwa na kuibiwa mali yao zaidi ya mara moja.

Na majuzi kuna wazungu waliibiwa mali yao kwenye beach Zanzibar.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.irishtimes.com/newspaper/breaking/2009/0818/breaking31.htm

http://www.rte.ie/news/2009/0808/stringerr.html

http://www.google.com/hostednews/ukpress/article/ALeqM5h8grmvaZDlHjMTifiw2jc1QFF7Gg