Showing posts with label Saratani. Show all posts
Showing posts with label Saratani. Show all posts

Sunday, August 09, 2015

Tuombe Wenye Ugonjwa wa Saratani Wapone!


Wadau, tuombe wenye ugonjwa wa saratani wapone.  Baba yangu mzazi, Dr. Aleck Che-Mponda alifariki mwezi Machi kwa ugonjwa wa Prostate Cancer (saratani).  Mfanyakazi mwenzangu hapa USA alikufa kwa kansa ya tumbo, mwingine kwa kansa ya mapafu mwaka huu.  

Tuombe haya makampuni ya madawa yanayotumia hela KUZUIA utafiti ya tiba ya saratani wabadilishe mioyo yao. Wamezidi uchu ya ya pesa! Waende Motoni wote!  Tiba ingeshapatikana lakini wanazuia kwa vile wanaogopa watashindwa kuuzwa madawa yao!

Wednesday, April 13, 2011

Ushuhuda wa Kupona Kansa Baada ya Kunywa Dawa ya Babu

Wadau, Hebu mtembelee Da Subi kusoma shuhuda za watu waliopona saratani (Kansa) baada ya kunywa dawa ya babu wa Loliondo. http://www.wavuti.com/4/post/2011/04/ushuhuda-kupona-saratani-dawa-masapile.html#axzz1JK62Bn7R

Thursday, March 26, 2009

Wagonjwa wazidi kuongezeka Ocean Road Hospital


Wagonjwa wa Saratani (Kansa) wanazidi kuongezeka Ocean Road Hospital. Ina maana kuwa ubora wa huduma huko itapungua. Wadau, nawauliza kwa nini ugonjwa wa saratani unaongezeka Tanzania? Je, watu walikuwa nayo zamani ila hatukujua ni nini, tunasema kalogwa? Je, ni kwa vile maisha yanabadilika na kuwa ya kizungu (vyakula nk.).?
*********************************************************

Kutoka ippmedia.com

Taasisi ya Saratani ya jijini Ocean Road imeanza kuzidiwa

2009-01-24 12:04:06

Na ITV Habari

Taasisi ya Saratani ya jijini Ocean Road imeanza kuzidiwa kutoa huduma za tiba hiyo kwa wagonjwa wapya kutokana na idadi ya wagonjwa hao kuongezeka kila mwaka na kufikia wagonjwa elfu arobaini wanaohitaji tiba hiyo kwa mwaka .

Wakizumgumza baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku tatu kujadili mikakati ya kuthibiti ugonjwa wa saratani uliohudhuriwa na wataalam wa tiba na madkatari wa saratani nchini baadhi ya washiriki wamesema kuna haja ya kuongeza jitihada katika kuwahamasisha wanajamii wa maeneo ya vijijini umuhimu wa kuwahi tiba ya saratani ikiwa kwenye awamu za mwanzoni wakati bado kuna matumaini ya mgonjwa huyo kupona.
SOURCE: ITV