Saturday, March 11, 2017
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utallii Yatembela Eneo lenye Mgogoro la Por Tengefu la Loliondo
Wednesday, April 04, 2012
Waliopata 'Kikombe cha Babu' Wafariki Dunia - Habari Leo
![]() |
| Mgonjwa wa UKIMWI |
| Waliopata ‘Kikombe cha Babu’ Wafariki Dunia Imeandikwa na Waandishi Wetu; Tarehe: 4th April 2012 | |||||||
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo sasa itatangaza matokeo ya utafiti wa tiba hiyo ya ‘Kikombe cha Babu’ imesema wengi ni wale wenye Ukimwi walioacha matumizi ya dawa za kurefusha maisha (ARVs). Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikuli, aliiambia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) jana Dar es Salaam, kwamba hadi sasa Serikali inafanyia utafiti watu 206 ambao walipata kikombe hicho. Utafiti unaofanywa na Wizara hiyo inataka kubaini kama kweli dawa hiyo ina uwezo wa kuponya Ukimwi, kisukari, saratani na magonjwa mengine sugu. Wanaofanyiwa utafiti huo walipata ‘kikombe’ hicho baada ya kuugua kisukari na Ukimwi. “Kwa sasa ni vigumu kusema dawa hiyo inaponya au haiponyi, tusubiri utafiti wa kitaalamu. “Baada ya miezi miwili tutatangaza matokeo kwa umma,” alisema Kikuli na kuongeza kuwa utafiti huo unafanywa katika hospitali mbalimbali nchini chini ya usimamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Utafiti huo unafanywa katika hospitali za Bugando, Mwanza; Mbeya; Mount Meru, Arusha; Hydom, Manyara na KCMC, Kilimanjaro. Hospitali hizo ziko maeneo ambayo wananchi wengi walijitokeza kupata ‘kikombe’ Loliondo. Kikuli pia alisema kwa sasa idadi ya Watanzania wanaokwenda Loliondo kupata tiba hiyo imepungua; lakini bado wananchi wa kutoka Kenya na nchi zingine wanaendelea kwenda kupata ‘kikombe’ hicho. Hata hivyo, Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Donan Mmbando, alikiri kuwa wagonjwa wengi wa Ukimwi waliokwenda kupata tiba hiyo na kuachana na ARVs wamepoteza maisha. Mbunge wa Nkasi, Ali Kessy Mohamed (CCM), aliishauri Wizara hiyo kuacha siasa badala yake iwaambie wananchi kwamba dawa ya Babu wa Loliondo haina madhara kwa binadamu, lakini pia haina uwezo wa kuponya magonjwa. “Msiogope kusema kama wanasiasa, ninyi ni wataalamu, ni kweli kuwa ile dawa haina madhara kama yalivyo maji, lakini tusidanganyane, haitibu, kwa nini mnaendelea kudanganya wananchi?” Alihoji Mbunge huyo. Makamu Mwenyekiti wa PAC, Zainab Vullu, ndiye aliyetaka Wizara itoe taarifa ya utafiti wa tiba ya ‘kikombe cha Babu’. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John Cheyo, alitaka kujua kama bado kuna idadi kubwa ya Watanzania wanaokwenda kupata tiba hiyo Loliondo. Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola, alitaka kujua kama Wizara hiyo imewasiliana na nchi zingine za Ulaya ambazo raia wake walikwenda kupata tiba ya ‘kikombe’ kama walipona magonjwa waliyokuwanayo. “Wenzetu wale Wazungu ni wepesi katika masuala haya ya utafiti, nataka kujua kama mmefanya juhudi za kuwasiliana nao?” Alihoji mbunge huyo na kujibiwa na Kaimu Mganga Mkuu kuwa kila nchi ina utaratibu wake wa utafiti. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA! *********************************************** Hii imetoka kwenye gazeti la Habari Leo. Mwaka jana saa hizi kila mtu alitaka kwenda kwa Babu. Inasikitikisha kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wamekufa. Babu yuko wapi leo hii, je, watu bado wanajazana kule Loliondo kutafuta 'Dawa ya Babu'? | |||||||
Tuesday, January 03, 2012
Babu Wa Loliondo Janga La Kitaifa 2011 - Maggid Mjengwa
![]() |
Mh. Lukuvi na Binti yake Mwalimu Nyerere wakipata 'kikombe' kutoka kwa Babu |
Babu Wa Loliondo Janga La Kitaifa 2011
“Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote”,ni wimbo unaovutia ni wimbo; unaelezea wasifu wetu wasifu wa nchi yetu Tanzania kweli jina lako ni tamu tulalapo tunakuota wewe, Ndoto wakati mwingine uashiria kitu kijacho !
Naam ndugu zangu Watanzania, tukiwa tunakaribia kumaliza mwaka nchi yetu imekumbwa na majanga kadhaa likiwepo hili la mafuriko napenda kuchukua nafasi hii kuwapa pole wote waliofikwa na mafuriko najua Mungu atasimama upande wao, janga hili ni muendelezo wa majanga mengi yaliyoikuta Tanzania yetu tunayoiota utalalapo, Ambikile Mwaisapile maarufu kama babu wa loliondo ni moja ya majanga hayo .
Inayodaiwa kuwa tiba ya Babu wa Loliondo, badala ya kuwa msaada kwa taifa, imeonyesha madhara zaidi ya kiafya, kijamii na kiuchumi. Tuliandika kutahadharisha na kushauri. Tumepuuzwa; maana, kwa wengine, tiba ya Babu ilikuwa ni mradi, na kwa kweli kugeuzwa kuwa mradi wa kitaifa.
Na kilichojikita katika kuwaacha watu wetu wakitaabika ni unafiki wetu. Tuna maradhi mabaya, na ni sugu. Ndio, miongoni mwetu kuna wenye kusumbuliwa na maradhi ya unafiki. Nitatoa mfano nilipata kukaa na wasomi wawili, tena wana digrii zao. Tukazungumzia ya Babu wa Loliondo.
Mimi na wasomi wale tulikuwa na misimamo ya kufanana, tulipinga upotoshaji unaoendelea katika jamii kuwa Babu wa Loliondo, Ambilikile Mwasapile, anatibu ukimwi, kansa, kisukari na mengineyo. Na kwa vile wote tumekwenda shule, hoja kuu ilikuwa hii; kuwa hadi sasa hakuna hata wagonjwa watatu wa ukimwi waliothibitishwa kitaalamu kuwa wamepona ukimwi kwa dawa ya Babu.
Badala yake, kuna wengi wamekufa baada ya kuacha kutumia madawa waliyoelekezwa na madaktari watalaamu waliosomea tiba.
Wakati tukiendelea kuzungumza, mara akatokea mheshimiwa fulani, naye akaingia moja kwa moja kwenye mjadala. Alimtetea Babu na kusisitiza kuwa. Babu ni lulu ya taifa, lazima aenziwe. Wasomi wale afadhali wangekaa kimya, hapana, walianza kumuunga mkono mheshimiwa kwa hoja nyepesi.
Hawakuwa wapumbavu, walijifanya tu wapumbavu wakiniacha mimi nikipambana peke yangu kuziponda hoja za mheshimiwa yule. Kwa kiasi fulani, niliogopa kuona hulka hii ya wasomi wetu. Wasomi ambao, kwa unafiki, wanashindwa kutetea na kusimamia katika hoja zao za msingi. Na hii, bila shaka, ni moja ya majibu ya swali la kwa nini Tanzania ni masikini?
Hakika, ya Babu wa Loliondo ni aibu yetu kitaifa. Katika karne hii ya 21 nchi yetu inatumia raslimali zake kufanya promosheni ya ndoto ya Mtanzania mmoja kati ya Watanzania milioni 42! Ndio, tunafanya promosheni ya jambo lisilo na uthibitisho wa kisayansi. Si tuliona, haikupita siku bila kusikia habari za Babu wa Loliondo?
Kwa sasa, tunaweza kabisa kusema, kuwa habari za huduma za Babu wa Loliondo zilitangazwa na kuufikia umma kuliko habari za Wizara yeyote ile katika Serikali ya Awamu ya Nne. Babu wa Loliondo si mchezo bwana, alikuwa na ‘maafisa habari wake’ wanaowafunika hata maafisa habari wa Wizara za Serikali.
Na katika mzaha huu wa mambo ya msingi kitaifa, tuna maelfu kwa maelfu ya Watanzania wanaotaabika na hata baadhi kufa kwa kuamini kuwa Loliondo kuna tiba, na iko Loliondo tu! , kuna Watanzania walioweka rehani mavuno yao ya mwaka mzima ili wapate nauli ya kwenda kwa Babu. Si wameambiwa, kuwa hata mawaziri wanapanga foleni ya kwenda kupata kikombe cha Babu!
Na wakishapata kikombe wanapiga picha ya ukumbusho, au labda ya kisiasa. Asubuhi yake ’maafisa habari’ wa Babu wameshatundika picha ya waziri ukurasa wa kwanza gazetini! Jimboni kwa mheshimiwa wapiga kura wake watamwona au kusikia kuwa Mheshimiwa naye anaumwa kama sisi, na amepata kikombe cha Babu!
Kikombe cha Babu ni abrakadabra, nilipata kuandika hilo. Na Watanzania, baadhi, kwa hiyari yetu, tumekubali kujifanya, wajinga na hivyo kuwapumbaza wengi wengine. Kwanini? Tulitafute jibu kwa kufikiri kwa bidii.
Hebu jiulize; wakati Shirika la Afya Duniani (WHO), Juni mwaka huu, liliadhimisha miaka 30 ya mapambano dhidi ya ukimwi, je, Tanzania, kama nchi, tulikuwa na banda la maonyesho likielezea ugunduzi wa tiba ya ukimwi iliyotokana na ndoto ya Babu?!
Labda ndio maana, magazeti yetu ya lugha ya Kiingereza hayakufanya sana promosheni ya tiba ya Babu. Maana, kama habari za Babu zingepewa uzito kama ilivyo kwenye magazeti yetu ya lugha ya Kiswahili, basi, wana jumuiya ya Kimataifa, wakiwamo wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, huenda wangeshindwa kuamini wanachokisoma.
Maana, wawakilishi wa mashirika kama PSI na FHI yenye miradi ya kupambana na ukimwi nchini na mengineyo wangejiuliza; nini hasa wanachokifanya katika nchi yetu. Na pengine wameshatafsiriwa tunachooandika juu ya Babu kwa Kiswahili chetu!
Si ajabu basi, Ubalozi wa Marekani ulikuja na tamko lake Mei 5 mwaka huu. Wamarekani hawa, kwa kuwaonea huruma Watanzania, wameshauri watu wanaotumia tiba mbadala wasiache kutumia dawa walizopewa na madakatri na vile vile waendelee kujikinga na maambukizi.
Na wakaweka msisitizo kuwa, kuacha kutumia dawa hizo za madaktari watalaamu kunafanya dawa hizo zinapotumiwa tena kushindwa kufanya kazi ipasavyo (drug resistance). Na ajabu ya habari ya tamko lile la Wamarekani ilichapishwa katika gazeti moja tu kwa lugha ya Kiingereza - The Citizen, jina la gazeti hilo lina maana ya Mwananchi; ingawa wananchi wengi hawakupata habari hiyo kwa lugha yao!
Kwa hakika, hatuhitaji kuambiwa na Wamarekani juu ya ukweli huu na wajibu wetu. Huu ni wakati kwa wizara inayohusika kufanya jitihada za dhati kutoa tamko litakaloweka bayana kuwa tiba inayodaiwa kutolewa na Babu bado haijathibitika kitalaamu kama inaponya maradhi sugu kama vile ukimwi, kansa; na kisukari.
Wakati utafiti huo ukiendelea, umma ukumbushwe kuwa, dawa zinazotambulika kitalaamu kwa sasa ni zile zinazotolewa na madaktari wetu watalaamu. Kwamba wanaokwenda kwa Babu wana ruhusa ya kufanya hivyo, lakini, kikombe cha Babu kinaweza kunywewa pamoja na dawa za hospitalini.
Tufanye hivyo sasa, na ujumbe huo usambazwe kwa nguvu zote na maafisa wa habari wa wizara husika. Ndio, maofisa habari wa Wizara ya Afya nao washindane na ‘maafisa habari’ wa kujitolea wa Babu wa Loliondo!
Watanzania tunapita kwenye kipindi kigumu sana. Na huu ni wakati wa kutafakari kwa kina. Na nimepata kumwuliza jamaa yangu swali hili; mwanadamu ; unafanyaje unapoamka na kukuta dunia unayoishi ardhi yake imeanza kumegeka na kuchotwa na bahari? Naye akanijibu; ” Huo ndio utakuwa mwisho wa dunia!”
Aliyenijibu alikuwa amechoka kufikiri. Nilidhani angetamka kuwa, angeanza kujifunza kuogelea. Maana, kwa kuogelea majini angeweza kukutana na kisiwa, au nchi kavu.
Wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndio njia mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando kuruhusu mwanga upite. Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri?
Haya ya kwa ‘Babu wa Loliondo’ ni kielelezo cha Watanzania kuamua kuacha kufikiri. Kuna umma uliojifunika vilemba vya ujinga. Umma uko gizani, ; unahitaji mwanga.
Yumkini wakatokea Watanzania wenzetu wakaoteshwa na Mungu juu ya dawa za tiba kwa mwanadamu. Na hapo wakaingiza suala la imani. Lakini, jambo hilo halituzuii wanadamu kuhoji na kudadisi. Ndio, kuuliza maswali. Na kwa Serikali, jambo hilo haliizuii kufuata taratibu zake za kawaida ikiwamo kufanyia utafiti jambo hilo na kutoa msimamo wa kiserikali.
Hata kama Watanzania watakuwa na uhuru wa kwenda kwenye tiba za imani, lakini msimamo wa Serikali uwepo. Na kwa wengi utabaki kuwa ndio mwongozo; maana, watakuwa wameufanyia utafiti. Nahitimisha.
Niwatakieni Heri ya Mwaka Mpya.
Maggid Mjengwa.
http://mjengwablog.com/
*************************
SOMA HABARI ZAIDI ZA VIFO LOLIONDO GLOBAL PUBLISHERS:
http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/loliondo-1
Tuesday, June 14, 2011
Madaktari wa Kenya Hawampendi Babu wa Loliondo!
Madaktari hao wanawaonya kuwa wasiache kutumia dawa zao maana dawa ya babu si tiba ya kudumu bali ya kifikra.
Huko Kenya, waKenya wengi wameamua kwenda kwa babu baada ya kuona maajabu. Watu ambao walikuwa wagonjwa mahututi na hata vipofu wamepona maradhi yao baada ya kwenda Loliondo kwa Babu.
************************************************************************
Doctors alarmed as patients seek Loliondo 'wonder drug'Medical practitioners in Trans Mara District have raised alarm over a worrying trend of patients withdrawing from treatment after travelling to Loliondo, Tanzania for the "wonder drug cure".
Led by the area District Medical Officer of Health, Aggrey Ouko, the medical professionals said patients undergoing treatment for HIV, tuberculosis, diabetes, hypertension, among other life threatening ailments, were stopping treatment after visiting the ‘healer’.
He said records at various health facilities have shown a sharp decline in the number of patients attending the facilities after visiting Loliondo.
The officer reported that some HIV patients had abandoned taking anti-retroviral drugs under the belief they had been cured.
Lives at stake
Addressing an HIV advocacy forum in Kilgoris, which brought together local leaders and the Provincial Administration, Ouko said several lives of patients were at stake if no immediate action was taken to address the issue. He said some of the patients who had withdrawn from hospital treatment have developed Multi-Drugs Resistance (MDR), a condition that makes it possible for a disease-causing organism to resist distinct drugs.
Separately, doctors in Nakuru say that 30 years since the first HIV/Aids case was reported, self-stigmatisation remains a major barrier in provision of medical services to those living with the disease.
Lawrence Otemba, an advisor with the International Planned Parenthood Federation, says most of those infected still avoid seeking medical services for fear of discrimination. Dr Otemba said it’s important to increase care and support for those infected and also intensify the fight against stigmatisation of those living with the virus.
"People fear that if they come out and seek medical services they will be discriminated and as a result a lot of people do not even know their status," he added. He was speaking in Nakuru during a visit by a Japanese delegation to a project run by Family Health Options Kenya (FHOK).
Infected and Affected
The delegation was on a tour to evaluate the activities carried out by FHOK aimed at improving quality of lives of people infected and affected with HIV/Aids in Nakuru.
FHOK project Coordinator Jane Adero said that the formation of support groups in the town has assisted those infected to cope and live longer.
*****************************************************************
USHUHUDA ******* WAKENYA WAPONA MAGONJWA YAO BAADA YA KUPATA 'KIKOMBE'
Trans Nzoia Residents Healed in Loliondo
Business came to a standstill in Kitale town following the return of a busload of Trans Nzoia residents, who had travelled to Loliondo to seek intervention from the famous traditional doctor Mzee Ambilikile Mwasapile. Curious residents jammed the main bus terminus to talk to the passengers about the doctor.
Most passengers looked tired from the long journey that had taken several days. Peter Kiarie, who said he has been diabetic for the last 20 years, could not hide his joy as he narrated to the Star how he is cured and is now back to his normal diet. "Immediately I took the magic drug from Mzee Mwasapile and followed his instructions strictly, I felt a strange feeling in my body, and then a sigh of relief for my 20 years of fighting with diabetes," he said.
He said the condition had almost broken his marriage and used up all his money buying expensive drugs to control his condition. Kiarie said after years of visiting several hospitals in vain in search of treatment, he is happy that God used Mzee Mwasapile to heal him. "The man is God sent and I believe very many will be healed through the process," he said.
He believes only those with a strong faith will be healed saying that not all who travelled to Loliondo village were cured. Kiarie said the drug was not allowed out of the "holy shrine" saying Mzee Mwasapile insisted that the concoction became poisonous once it left the place.
He believes that Mzee Mwasapile's shrine is a holy place that despite thousands of people jamming the small dusty village there were no scenes of immorality, theft or robbery. Kiarie also had boils on his legs and head but they disappeared after he drank the concoction.
An elderly woman who was on the trip said she had lost her sight seven years ago but could now see after drinking the concoction. "Before I went to Loliondo I could not read my Bible and was depending on my grandchildren. But I can now read my Bible. God is great," she said.
Bus conductor Stanely Mwangi said most of those who boarded two weeks ago could not walk and were literally carried into the vehicle, but he is surprised to see them walking without help and showing faces of good health. "I am equally surprised with the turn of events of the wonder drug, because when we left this place to Loliondo, I thought most of these people were going die on the way, but here they are," he said .
The patients interviewed also told the star that people close Mzee Mwasapile had hinted that the magical powers were to last till June of this year and thats why people were jamming the dusty village.
The bus company is making booming business as it makes a trip to Loliondo every Thursday. Each passenger pays Sh6,000 .The bus carries 41 passengers while the bus booking office in town has a conspicous sign post written " Loliondo hospital bus Direct". According to the director of the bus company James Wanyoike the demand for the services is growing fast and they are contemplating increasing the number of buses.
http://allafrica.com/stories/201105190143.html
Friday, May 06, 2011
Wataalam Wasema Dawa ya Babu Inafanya Kazi Kiasi
A technical report on retired pastor Ambilikile Masapila’s “miracle cure” has indicated that scientific data supports his claims to its positive effects on a number of ailments.
A report by experts from the National Institute for Medical Research (NIMR) Department of Traditional Medicine Research and Institute of Traditional Medicine, Muhimbili University of Health and Allied Sciences seen by The Guardian, says study findings have revealed that ‘Babu’s miracle cure’ prepared by boiling the roots of Carissa edulis plant is safe and has positive effects on cancer, epilepsy, herpes simplex virus, liver ailments, diabetes, blood pressure and anti-viral activity.
However, the scientists said since the remedy is being widely used by an exceedingly large number of patients, the government should advance the work of focused pre-clinical studies to establish pre-clinical efficacy and safety of the remedy.
“The dose provided by Pastor Masapila which is one cup (about 200 mls) prepared through boiling an estimated 3.0 kg of whole root material in 60 litres of water “falls within safety window and no any overdose or acute poisoning event is expected.”
The results suggested that the plant has anticonvulsant activity which supports the claim of the use of the plant in the management of epilepsy as claimed by Pastor Ambilikile Masapila.
It further indicated that the herb has antidiabetic activity which supports the claim of the use of the plant in the management of diabetes.
The herbal has blood pressure lowering activity which supports the ethnomedicinal claim of the use of the plant in the management of high blood pressure.
Research results show that the pastor’s concoction has hepatoprotective and antioxidant activity which are beneficial in the prevention of liver disorders and cancer.
“This result also reveals that Carissa edulis has potent anti-viral activity against herpes simplex viruses. Taking into consideration that, herpes simplex virus (HSV) infection is a major opportunistic infection in immunosuppressed persons, these findings supports the ethnomedicinal claim of the use of the plant in the management of HIV/Aids as claimed by Pastor Masapila,” said the report.
Drawing general conclusion, scientists said that the plant is safe and the dosage prescribed by Rev. Mwasapila is below the toxic level.
They, however, recommended that since the remedy is being widely used by an exceedingly large number of patients, focused pre-clinical studies need to be conducted to establish pre-clinical efficacy and safety of the remedy.
Scientists also recommended standardisation and formulation of “Babu’s cupful” for human use.
“MoHSW should conduct clinical trial on the prescribed remedy to establish in vivo efficacy and safety in humans and answer questions on optimum dosage, dosing schedule and duration of treatment per ailment,” stated part of the report.
It added “MoHSW should conduct clinical follow up on all patients recorded to have used the remedy for their prognosis.”
Recently, many people have been flocking Samunge village in Loliondo, Arusha, seeking the cure for chronic diseases such as diabetes, asthma, epilepsy, cancer and HIV/Aids.
According to Rev. Masapila, God instructed him through dreams since 1991 about the medication and that, it will heal people with chronic illnesses namely: diabetes, asthma, epilepsy, cancer and HIV/AIDS. The dream kept recurring to him several times since then and on August 26, 2010 he decided to obey on the instructions and started the healing work.
Earlier this month, HIV/Aids stakeholders blamed the government over its silence on HIV/Aids patients who abandon antiretroviral drugs after taking the herbal concoction being dispensed by Pastor Masapila in Loliondo.
HIV/Aids stakeholders said there was need to give correct messages to the people to avoid negative impacts in future.
SOURCE: THE GUARDIAN
Thursday, May 05, 2011
Wagonjwa wa UKIMWI Wafa Baada ya Kunywa 'Kikombe'
*****************************************************************
Kutoka The Citizen:
5 Kiteto villagers die of Aids after abandoning ARVs
Monday, 02 May 2011 22:17
By Joseph Lyimo
Kibaya. Five residents of Sunya village in Kiteto District, Manyara Region who had tested HIV positive are reported to have died after abandoning anti retroviral drugs (ARVs) in favour of a herbal concoction from a 'miracle healer' in Loliondo.
Their deaths occurred shortly after arriving back from Samunge village where the retired pastor Ambilikile Mwasapila has been dispensing liquid drink from a local herb he claims cures a range of chronic diseases, including Aids. A councillor for Sunya Ward, Mr Mussa Brighton, confirmed the deaths of the villagers, saying they had just returned back home from Loliondo where they went to seek treatment from Rev. Mwasapila.
Mr Brighton, who is the vice chairman of the Kiteto District Council, said the five had reportedly abandoned using the life-prolonging ARVs as recommended by medical doctors as one of the arsenals against killer Aids.Unconfirmed reports said the deceased had been telling people after returning from Loliondo that they had stopped using ARVs because they were feeling better after taking a cupful herbal drink from "Babu.”
The councillor warned that the trend was not good because, people who had tested positive should not abandon the ARVs dose from medical facilities. He could not disclose the names of the deceased.He argued that the sudden rush to Loliondo for herbal cure offered by the spiritual healer should not make people discard the recommended medicines.
Wednesday, April 13, 2011
Ushuhuda wa Kupona Kansa Baada ya Kunywa Dawa ya Babu
Wednesday, April 06, 2011
Kikombe cha Babu - Mjadala

pichani- Wagonjwa wakisuburi kupata 'Kikombe' huko Loliondo
Wadau, Maggid Mjengwa na John Mashaka wana moani makali kuhusu 'KIKOMBE' cha babu wa Loliodo. Lazima nami niseme nina ndugu yangu ambaye alienda huko Loliondo kupata kikombe ili apone Kisukari. Alipoipata alijisikia freshi kwa siku kadhaa sasa analalamika maumivu. Nadhani hicho kikombe haimtimbu kila mtu, lakini wako waliopona. Je, hao ambao hawakupona baada ya kunywa hawakuwa na imani, au haikuwa na dawa ya kutosha? Na ni kweli kuwa watu nje ya nje wanatucheka kuwa tuna imani kali na uchawi.
Sioni ubaya kuwa na imani ya kikombe. Ila sasa wengine copycats wanaomwiga babu wanajitokeza kila kona na vikombe. Na watu wanakimbilia kunywa! Ni fesheni nini? Pia msishangee siku moja mkisikia kuna mtu kajitokeza na kikombe' watu wakanywa kwa wingi halafu walikufa kwa wingi kwa vile ilikuwa na sumu!
Someni maoni ya Kaka Maggid na Kaka John Mashaka halafu karibuni mjadili.
Loliondo na Umma Ulio Gizani
Maggid Mjengwa Machi 23, 2011
TUNAWAPITISHA watu wetu kwenye njia yenye giza. Kwenye njia yenye matope. Kwanini?
Socrates, mwanafalsafa wa Uyunani alipata kuonekana akimulika kurunzi mchana wa jua kali. Inaandikwa, kuwa Socrates yule alizunguka sokoni na kurunzi yenye kumulika. Watu walimwuliza, kulikoni? Socrates akawajibu; ”Kwenye nuru hii , kuna walio gizani.”
Kwa Socrates lilikuwa ni tendo la kifalsafa lenye kuelezea hali halisi. Hata katika dunia hii ya kisasa, bado tuna miongoni mwetu, walio gizani mchana wa jua kali. Angalia ya kwa ’ Babu’ wa Loliondo. Ndiyo, kuna wanaohitaji kumulikiwa mwanga.
Na kuna tofauti ya ujinga na upumbavu. Marehemu Mzee Jongo alipata kutamka; ” Kusoma si kuufuta ujinga, bali ni kuupunguza”. Kila mwanadamu ana ujinga wa jambo moja au mia moja. Kuwa na ujinga wa jambo si kosa, hata profesa anaweza asijue namna ya kuchochea kuni za kuchomea mhindi mbichi ukachomeka. Kijana wa darasa la saba anaweza kuwa hodari wa jambo hilo kumshinda profesa.
Lakini upumbavu ni ile hali ya mwanadamu kufanya jambo isivyotakiwa huku akiwa na uelewa wa namna ya kufanya inavyotakiwa. Huo ndio upumbavu. Na ndiyo maana binadamu kuitwa mpumbavu ni tusi. Kuitwa mjinga si tusi, kila mmoja ana ujinga wake. Kuwa na ujinga wa jambo fulani ni kutoelewa jambo hilo. Ni nani anayeelewa kila jambo?
Na mwanadamu unafanyaje unapoamka na kukuta dunia unayoishi ardhi yake imeanza kumegeka na kuchotwa na bahari? Kuna niliyemwuliza swali hilo. Naye akanijibu; ” Huo ndio utakuwa mwisho wa dunia!” Aliyenijibu alikuwa amechoka kufikiri. Nilidhani amgetamka, kuwa angeanza kujifunza kuogelea. Maana, kwa kuogelea majini angeweza kukutana na kisiwa, au nchi kavu.
Wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndiyo njia mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando kuruhusu mwanga upite. Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri? Haya ya kwa ’ Babu’ wa Loliondo ni kielelezo cha Watanzania kuamua kuacha kufikiri. Kuna umma uliojifunika vilemba vya ujinga. Umma uko gizani, unahitaji mwanga.
Yumkini wakatokea Watanzania wenzetu, wakaoteshwa na Mungu juu ya dawa za tiba kwa mwanadamu. Na hapo wakaingiza suala la imani. Lakini, jambo hilo halituzuii wanadamu kuhoji na kudadisi. Ndiyo, kuuliza maswali. Na kwa Serikali, jambo hilo haliizuii kufuata taratibu zake za kawaida ikiwamo kufanyia utafiti jambo hilo na kutoa msimamo wa Kiserikali. Hata kama Watanzania watakuwa na uhuru wa kwenda kwenye tiba za imani, lakini msimamo wa Serikali uwepo. Na kwa wengi utabaki kuwa ndio mwongozo, maana, watakuwa wameufanyia utafiti.
Si tumemsikia yule nabii mwingine wa Tarakea, naye ni kijana wa miaka 28. Ikasemwa, kuwa naye kaoteshwa na Mungu dawa ya kutibu wagonjwa. Mpaka Serikali ilimpomzuia ili ifanye uchunguzi, tayari alikuwa na wagonjwa 100. Ndiyo, Watanzania tu wagonjwa tunaogombewa. Na viongozi wetu pia ni wagonjwa. Si tumewaona wakipanga foleni ya kikombe kwa Babu?
Katika dunia hii Serikali hupendwa na watu, lakini, si vema na busara, kwa serikali za dunia kutaka kujipendekeza kwa watu. Kuna mambo yenye kupendwa na watu, na watu wakawa na haraka ya kutaka kuyafanya. Lakini, kama serikali itahitaji kufuata taratibu ili kinachopendwa na watu kifanyike, basi, serikali haina namna nyingine, bali kufuata taratibu.
Si tuliona yale ya DECI. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisimamia taratibu, akasimamisha wimbi lile la DECI. Kuna wengi walishutumu, lakini , hao hao, leo wanaishukuru Serikali. Maana, DECI nayo ilikuwa ni Abrakadabra.
Na si juzi hapa tumemsikia Paroko wa Kigango cha Mt. Yohane wa Msalaba Parokoia ya Mbezi Luis Padri Vivian. Niweke wazi, Paroko yule amesema kile ambacho kuna wengi hawataki kukisikia. Ameusema ukweli wake. Ameifanya kwa dhati, kazi ya utumishi wa Mungu wake.
Paroko yule wa Mbezi Luis alitamka; "Sina chuki wala tatizo lolote na tiba ya Loliondo, lakini kama unataka kwenda lazima ujiulize maswali manne yafuatayo;
Kwanza, tiba inayotokana na miujiza ya Mungu lazima iwe endelevu isiwepo kwa kipindi kifupi tu.
Pili, watu wajiulize kama miujiza kutoka kwa Mungu huwa na masharti?
Tatu, wajiulize kama tiba hiyo inafanya kazi ndani ya Loliondo, kwanini isifanye kazi Dar es Salaam na kwingineko?
Nne, wajiulize kuhusu tiba hiyo ya magonjwa sugu ukiwemo ukimwi ni je, Mungu aliwaumba wanadamu na kisha kuamua kuwaangamiza? Au wanadamu wanaangamia kutokana na vitendo vyao vya ujanja ujanja?
Mwisho Paroko yule akasema; "Ukiishajiuliza maswali hayo na kujiridhisha kwa majibu utakayopata, basi, unaweza kufanya maamuzi ya kwenda Loliondo.
Ndiyo, tujiulize; katika mataizo yetu haya, tumechoka kufikiri? Tumechoka kuuliza maswali? Hapana. Tusichoke kuutafuta ukweli, hata kama umegubikwa na ukungu. Hivi ni Watanzania wangapi wamesikia au kusoma maelezo ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru Dk. Toure?
Nahofia si wengi, maana, maelezo yake yaliyopaswa kuwa habari kubwa ya ukurasa wa mbele yalipewa nafasi ndogo sana kwenye moja ya magazeti ya kila siku. Tena yaliwekwa katika ukurasa wa pili ndani ya habari nyingine. Si tunafahamu, kuwa baadhi ya wanahabari nao wanachagiza ’ Abrakadabra’ za ’ Babu’ wa Loliondo. Zinauza magazeti, na msimu ndio huu!
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Hospitali ya Mount Meru alisema, kuwa tangu tiba ya ’ Babu’ ianze, hajapata hata mgonjwa mmoja wa ukimwi aliyepata kikombe cha ’ Babu’ na kurudi hospitalini hapo kupimwa tena. Hivyo, mpaka hii leo hatuna ushuhuda wa kimaabara kwa maana ya hospitalini. Ushuhuda tunaousikia ni wa mitaani.
Ndiyo maana tiba ya ’ Babu’ itabaki kuwa ’ Abrakadabra’ mpaka hapo itakapothibitishwa vinginevyo kimaabara hospitalini na si kwenye vijiwe vya barabarani.
Halafu tunaambiwa, kuwa tiba ya ’ Babu’ inatibu kansa pia. Hivi Kliniki ya Kansa ya pale Ocean Road mpaka hii leo imeshindwa kuwapeleka kwa ’ Babu’ wagonjwa watano tu walio kwenye matibabu ya kansa. Waende huko wakapate kikombe halafu wachukuliwe vipimo tena tuone nguvu ya tiba ya ’ Babu’ katika kuwasaidia wagonjwa wa kansa.
Ndugu zangu, Mfalme Suleiman alimwambia Mola wake; ” Watu wangu wanaangamia kwa kukosa hekima”. NdiYo, Mfalme Suleiman alipoambiwa na Mola kitu cha kuchagua, basi, alichagua hekima ili aweze kuwaongoza watu wake.
Angalia leo, walio wagonjwa na kwenye hali ngumu za kiuchumi wanazidi kuwa wagonjwa na hali zao za kiuchumi zinazidi kuwa duni. Ndiyo, kuna wanaofunga safari zenye gharama kubwa kwenda Loliondo. Wanakwangua akiba zao. Kuna hata wanaokopa fedha ili waende Loliondo.
Ndiyo, wanakwenda kupata tiba isiyo na hakika katika wakati huu tunaozungumza. Kuna wagonjwa walioacha kutumia dawa zao. Wamerudi na kuanza upya. Kuna waliopoteza maisha. Inasikitisha sana. Ni nani wa kuwasaidia kuwamulikia mwanga? Naam. Kwenye nuru hii kuna walio gizani. Tuwasaidie.
===========================================================
John Mashaka anaandika....
I read with lot of interest Mr. Maggid Mujengwa’s article entitled “Ya Loliondo Na Umma Ulio gizani”, a philosophical description of a confused society. Mr. Mujengwa depicted Tanzania as a nation that is using a flashlight in a broad day light with a notion that, perhaps, it could aid her see better. Figuratively or philosophically speaking, Socrates the philosopher used this metaphor to describe a hopeless and a confused society. One question Mr. Mujengwa failed to address was the root cause of this confusion. How could Tanzanians be convinced that, flashlight is brighter than the sun? Is it because of ignorance, confusion or desperation?
Plato, one of the greatest philosophers to have ever lived, strongly advocated in favor of an examined life; An examination of one's life addresses fundamental questions such as: who am I, what do I want to do with my life, how will I know whether I have achieved my goals, what matters to me; wisdom; a feeling of accomplishment; wealth, power; social change or pleasure and how will I balance them. If you haven't asked yourself these questions, then life becomes meaningless. You become more like a boat in turbulent high seas without compass direction, going along with the tides and currents of the ocean. A boat that is destined for a clear tragic end of capsizing, Tanzania that is.
Tanzanians are not in control of their lives. Instead, they are controlled by the events of the day, and ignorantly perceiving flashlight to be more powerful than the sun, based on Socrates account on ignorance. As a nation, Tanzania has not asked itself these basic questions, because social-economic, hopelessness and despair amongst her people speak for itself. A sea of humanity flooding Loliondo, is a confirmation of the broken system. Her sick hopping from their hospital beds, carried in stretchers, just to have a sip of the wonder concoction is very troubling. This signifies the dying or non-existing healthcare system in Tanzania. Tanzania does not know where it is headed; it is a lost vessel sailing in the turbulent high seas without a direction, and only waiting to capsize
I must slightly differ with Mr. Mujengwa, based on my strong conviction, that, Babu Mwasapile’s patients are not uninformed, but rather hopeless, desperate, CONFUSED and poverty burdened men and women from all walks of life. Loliondo list of visitors is made up of the mighty and the powerful, the rich, the poor, scientists and herdsmen; famous and the little known peasants. Babu has received people who have made their way by selling their few worldly possessions, as well as the flamboyant tycoons arriving in style; in their private aircrafts, all with one goal; drinking the magical mixture, with hope ridding themselves of their excruciating illnesses. This is a national embarrassment, and depiction of Tanzania as a primitive and backward country in the eyes of the world
We are not talking about dumb, stupid, or simple-minded people; we are talking of brilliant and well educated individuals serving in the government, International, private and public agencies. We are talking of people who have been humbled by illnesses, and like anybody else, must heed the need to find treatment by standing in a long queue in the middle of nowhere; away from their posh homes, and comfort of their beds to find cure from the miraculous drink. We are talking of a hopeless and a desperate society on edge.
Desperation has no class, it has no social status or identity, it has no color or creed. It affects PhD holders and the illiterate alike. We must remember that, desperate and hopeless men do not value life; they have no shame or fear. Tell a man, who has exhausted all options to get rid of cancer, that his urine is the only cure to his excruciating illness. Even a King who desperately wants to live will heed the advice. These are the people flanking Babu of Loliondo’s compound trying to get rid themselves of terminal illnesses, endless pain, and misery.
Babu of Loliondo could not have emerged at a perfect time for the hopeless, when divine intervention is direly needed to save their souls. Babu has exposed our desperation, vulnerability and weakness as a society. He has exposed how useless education can be in the face of human despair. He has exposed how far we are lost in the turbulent high seas, and only going with the tide and flow. We are lost. Just like DECI which was a product of greed, ignorance and despair, Babu Liliondo’s purported magic cup is nothing but a tragic health and social a time bomb yet to explode!
MUNGU IBARIKI TANZANIA
John Mashaka
mashaka.john@yahoo.com
Thursday, March 31, 2011
Breaking News - Babu wa Loliondo Atatibu Wagonjwa Dar!
Wednesday, March 30, 2011
Sunday, March 27, 2011
Maoni ya Mdau Kuhusu Mjengwa Blog na Dawa za Babu
habari za kazi.
kwanza nakupongeza kwa kutumia muda wako mwingi kuelimisha umma wa watanzania ambao kwa bahati mbaya wengi wamo katika giza nene.
nimeshawishika kukuandikia mail hii baada ya kusoma makala zako kadhaa kuhusu dawa ya babu wa loliondo. niliona matusi, kubezwa na kudharauliwa unakokupata kufuatia kuwaambia watanzania ukweli, jamii ambayo kwa miaka kadhaa imezoea kuambiwa uongo, blah blah na kupumbazwa.
kimsingi nakubaliana nawe kuwa dawa ya babu ni abra kadabra. ni pumbazo ambalo limeingia katika jamii yetu kwa wakati huu na kwa bahati mbaya wasomi, wanasiasa na watu mashuhuri wamekuwa ni baadhi ya watu wanaofurika huko loliondo kupata kitu kinachoitwa kikombe.
hivi karibuni televisheni ya kenya ya ntv imetoa documentary kwa lugha ya kiswahili na lugha ya kiingereza kuelezea kile kinachoitwa maajabu ya loliondo. watu wamehojiwa wakiwemo wagonjwa, madaktari na baadhi ya wananchi wa kawaida hasa wa arusha. kuna maoni mchanganyiko kuhusu suala hili lakini ni wazi kuwa watu wamepumbazwa na maelezo kuwa mtaalamu wa dawa hiyo ni mchungaji mstaafu. kwa kuwa ni mchungaji mstaafu basi bila shaka dawa yake ni ya kweli!!!!
suala hili linaendeshwa kidini zaidi badala ya kijamii. wengi wa watu wanaodai kuponywa hisia zao wameziegemeza zaidi katika cheo au hadhi ya uchungaji wa babu. hii ni psychological treatment ambayo kwa vyovyote itaonekana kwa siku kadhaa kama sio miezi lakini baadae itaondoka na ndipo watu watakapojiona kuwa ni wapumbavu na hawakupata nafuu yoyote kutokana na kikombe cha babu.
ingekuwa mtaalamu huyu wa loliondo hakuwa mchungaji mstaafu hwenda hali ingekuwa tofauti kwa wanasiasa wetu na viongozi wa kijamii lkn hili la uchungaji ndilo linalowapumbaza watu na kujiona kuwa kumpinga babu na dawa yake ni sawa na kupinga imani jambo ambalo kwa mtazamo wangu si sahihi na ni kujipotosha wenyewe. dawa ya babu na imani ya dini hapa ni vitu viwili tofauti ambavyo vimewekwa pamoja.
kuna wengi duniani wanaotumia kivuli cha dini kwa maslahi yao na watu kupumbazika kwa kuona kuwa kinachosemwa na mtu husika hakipaswi kupingwa maana ukipinga utakuwa umepinga dini na dini inaogopwa. mtu huogopa kuwa akipinga ataonekana ameasi au atalaaniwa na dini au mungu.
maslahi ya dawa hiyo tunaambiwa yanagaiwa kwa kanisa husika, wasaidizi wake na kiasi kidogo huchukuwa yeye babu. katika hali kama hiyo iwapo kanisa linapata share fulani jee unategemea kuna kiongozi wa kanisa lake atakaemkataza? hilo haliwezekani maana kanisa litakosa mapato ambayo halikutegemea kuwa yangetokea.
mnakumbuka kufukuzwa kwa father NKWERA na waumini wake na kutengwa na kanisa lake? sababu kuu ilikuwa ni kufanya maombi na kuponyesha wagonjwa jambo ambalo lilisemwa kuwa si katika mafundisho ya kanisa. inawezekana kanisa la babu na la father NKWERA ni tofauti lakini hoja ipo pale pale. father NKWERA hakuwa ananufaisha kanisa kwa wakati ule lakini babu analiingizia kanisa fedha za kutosha hivyo watu wanafumba macho.
kwa bahati mbaya wanasiasa nao wamekumbwa na uozo huu. wakati waziri wa afya alitoa tamko awali kabisa la kupiga marufuku dawa hiyo hadi uchunguzi ufanyike, waliibuka wanasiasa uchwara ambao kwa kutaka sifa waliona tamko lile la waziri halina maana. kina SHIRIMA NA LUKUVI wakalivalia njuga jambo hilo na kudai kuwa serikali ipo pamoja na babu. waziri wa afya kwa kuepusha shari ya udini aliamua kukaa pembeni na kujinyamazia kimya.
hawa kina SHIRIMA na LUKUVI wanadai kuwa ni suala la kiimani hivyo serikali isiingilie imani za watu. wamesahau siku chache tu kabla ya uchaguzi mkuu mwaka jana mtu mmoja aliyejipa cheo cha mtabiri maafuru afrika mashariki na kati alitangaza kuwa mgombea mmoja wa uchaguzi angefariki dunia kabla ya uchaguzi mkuu na kupelekea uchaguzi kuahirishwa.
serikali hiyo hiyo wanayoisema kina LUKUVI na SHIRIMA ilitoa tamko kali la kupinga kauli hiyo na kumtaka mtabiri huyo anyamaze kimya au atachukuliwa hatua. serikali haikusema kuwa mambo yake ya utabiri ni maswala ya kiimani anayetaka aamini na asietaka aachane nae. lakini sasa tunaambiwa kuwa masuala ya imani serikali haiwezi kuingilia. hatua ile ya serikali kwa mtabiri yule ilikuwa sahihi kabisa lakini kwa sasa tunaona serikali ikiwa na kigugumizi kuhusu babu huyu.
hivi sasa kina babu wanaongezeka, wengine wakitokea mbeya. si hasha baada ya siku chache tukasikia mwengine ameibuka dar es salaam au mtwara au mwanza au hata pemba akidai nae ameoteshwa kuwa awahudumie watanzania kwa dawa ambayo formula yake haijulikani.
kwa ufupi dawa ya babu ni kanyaboya kwa hoja zifuatazo:
1. maradhi anayosema inatibu ni maradhi yanayosababishwa na vitu tofauti. baadhi husababishwa na virusi, mengine bakteria na mengine ni matatizo ya kutokuwa na uwezo wa homoni fulani mwilini. kwa vyovyote vile dawa ya matatizo haya haiwezi kuwa ni moja kwa sababu hata chanzo chake si kimoja. kwa mfano huwezi kupeleka gari gereji kwa matatizo tofauti kisha ufumbuzi wake kuwa ni huo huo mmoja. tatizo la gear box, chasis au tyre haviwezi kuondoshwa kwa aina moja ya ufumbuzi.
2. kauli za babu anapohojiwa na vyombo mbali mbali vya habari zinatofautiana. kuna sehemu anasema kuwa dawa yake inatibu maradhi matano kama alivyoambiwa na mungu. kuna sehemu anasema kinachotibu sio huo mti bali ni maombi yake na kuna sehemu anadai kuwa kinachotibu ni kikombe hivyo dawa husika isipotekwa kwa kikombe chake (kikitumika cha mtu mwengine) haitamsaidia mgonjwa. hizi ni kauli zenye mgongano. kwa mtu mwenye kutumia akili, hapa babu anajaribu kutumia ujanja wa kuzuia watu wengine wasiweze nao kujitengenezea dawa hiyo na kugawa kwa watu. anajaribu kutengeneza dominancy au monopoly katika jamii. kutakapokuwa na babu wawili au watatu bila shaka idadi ya wagonjwa wanaokuja kwake itapungua na hatimae maslahi kupungua pia.
3. kuna wakati babu hueleza kuwa dawa husika haiwezi kufanya kazi kwa mtu aliyefanya ujanja kwenye foleni kwa kuwapiku wenzake aliowakuta. hii ni njia nyengine ya ajabu kwa kuwa hakuna uhusiano wowote wa kitiba na suala la mtu kupanga foleni au kutokaa foleni.
4. kuhusu malipo ndo ujanja wa wazi kabisa. babu anadai ameambiwa na mungu kuwa atoze shs 500 tu kwa watz na dola 1 kwa wageni. hata hivyo hakusema iwapo kutakuwa na mabadiliko ya kupanda au kushuka thamani ya pesa itakuwaje? jee shs 500 au dola 1 itabakia hivyo milele? na jee binaadamu wanaotoka nchi ambazo hazitumii dola wala shs? au mungu hatambui fedha za nchi nyengine katika dunia yake zaidi ya dola na shilingi?
5. dawa husika anadai ni lazima itolewe loliondo tu. hii pia ni ujanja wa kuhakikisha kuwa hakuna babu wengine wanaoweza kufanya kazi hiyo katika mikoa mengine. ukitaka usitake ni lazima uende loliondo tu. ni kucheza na akili za watu na kwa bahati mbaya watu wamepumbazika.
6. kuhusu kulipia hapa napo pana jambo. kazi ya mungu huwa ya kujitolea lakini hakuna pahala babu anaweka utaratibu kwa watu wasio na uwezo wa hiyo shs500. jee anataka kutwambia kuwa mungu hajali watu mafukara ambao hata hiyo shs500 kwao ni kiwango kikubwa? vitabu vyote vya dini vinataja haja ya kuwahurumia mafukara na wasio na uwezo. lkn kwa hili babu yupo kimya sana. labda baada ya mfuko kujaa ndipo atakapotoa ofa kwa wasio na uwezo.
7. mwisho dawa ya babu haina dozi. hiki ni kituko chengine. kwa aliye mahututi aliye na nafuu nk wote ni kikombe kimoja tu. hili ni la kuchekesha kama sio kusikitisha. hata hao waganga wengine wa kienyeji hutoa dawa kwa mujibu wa hali ya mgonjwa. lakini pia kabla ya mgonjwa kupewa dawa huchunguzwa kama ana aleji au tatizo lolote kama vidonda vya tumbo nk. lkn hilo halipo kwa babu. kikombe hicho hakijali uzito wa ugonjwa wala afya yake. hakijali presha ya mgonjwa wala lishe yake. iwe ameshakula au ananjaa kikombe ni kimoja tu. hii ni hatari kwa jamii. hata katika mambo ya kawaida ya binaadamu hali haipo hivyo. gari la tani 3 litabeba mzigo wa tani 3 na la tani 10 litabeba mzigo wa tani 10. huwezi kusemwa magari yote yabebe tani 10 wakati yana uwezo tofauti.
sikutaka kutumia hoja za kisayansi kuwa dawa hii haijathibitishwa kwa kuwa watu wengi wanajidanganya kuwa dini ni zaidi ya sayansi. kwa maoni yangu dini na sayansi havipingani hata siku moja. ukiona hivyo kuna tatizo pahala.
mbali na hali niliyotaja hapo juu, kuna madaktari na wataalamu wa afya huko arusha ambao walishuhudia wagonjwa wakitolewa hospitali na kupelekwa kwa babu wamethibitisha kuwa baadhi yao pamoja na kupata kikombe hicho na kujidanganya kwa siku chache kuwa wamepona wamejikuta wapo hoi na kurudi tena hospitali. huu ndio ukweli ambao utajulikana siku si nyingi kwa kuwa maji hayo yaliyochemshwa hayana dawa yoyote na hayasaidii kuondoa ugonjwa.
kwa bahati mbaya pamoja na ukweli huu baadhi ya watu hudai kuwa wagonjwa hao waliojiona kuwa hawajapona eti walikwepa foleni au kutofuata utaratibu wa babu!!! huu sasa ni ujinga mwengine. wengine wanadai kuwa madaktari hao wanamuonea wivu babu eti kwa sababu kawanyanganya wateja wao!!! wakati watu wanawatahadharisha wao kuepuka kanyaboya wao bado wamo katika usingizi mzito wa kulewa kikombe cha babu...
kwa ufupi wafuasi wa babu wanataka kusema kuwa ni lazima watu wote waliopata kikombe hicho kumsifu babu na anayekwenda kinyume kwa kudai kuwa hajapona huonekana ndio mkorofi. kuna haja ya watanzania kutafakari na kuchukua hatua. tukumbuke kauli ya mhe rais KIKWETE kuwa AKILI YA KUAMBIWA CHANGANYA NA YA KWAKO....
Wakatabahuuu,
mdau
ughaibuni...
Saturday, March 26, 2011
Tiba ya Loliondo - Msimamo wa Mjengwa Blog
(Pichani) Baadhi ya waliofanikiwa kupata kikombe cha 'Dawa ya Babu' huko Sumange Village LoliondoNimesikia habari za watu kupona magonjwa yao baada ya kunywa dawa, pia nimesikia habari za watu amabo walizidiwa baada ya kunywa hiyo dawa na kuacha kutumia madawa waliopewa mahospitalini. Pia nimesikia habari za watu kufariki wakiwa wanasubiri kupata dawa ya ya babu. Ningependa kusikia kutoka kwa watu waliokunywa daw ya babu kabla ya kuaamua kama inafanya kazi au la. Mungu yu Mwema na kweli kama ametupa dawa ya kuponyesha magonjwa yasiyo na dawa basi ingekuwa vizuri dunia nzima wajue habari hiyo.
******************************************************************************
Hii ni tamko rasmi kutoka Mjengwa Blog:
Ndugu Zangu,
Hii ni nchi yetu. Tunayaandika haya kwa mapenzi ya nchi yetu. Yanayotokea Loliondo yanaanza kubeba sura ya kashfa. Taratibu, Loliondo inaonekana kuwa ni aibu ya kitaifa kwenye masuala ya kimsingi ya afya ya watu wake.
Si kawaida, na yawezekana ni mara ya kwanza kutokea, kwa blogu ya jamii kutoa msimamo juu ya jambo la kitaifa. Tunauona umuhimu huo, tunafanya hivyo. Ndio, Hali ni mbaya Loliondo. Kuna Watanzania wenzetu wanakufa kila siku. Wanakufa wakiwa kwenye foleni ya kupata kikombe cha Babu au baada ya kunywa kikombe hicho na kuacha kutumia dawa zao walizokuwa wakitumia kabla.
Asubuhi hii nimepokea simu kutoka Dodoma. Kuna mganga aliyenielezea hali mbaya zinazowapata wagonjwa wake wa kisukari mara baada ya kupata tiba ya Babu na kuacha kutumia dawa zao. Anasema ni mbaya zaidi kwa wagonjwa wa kisukari, maana, kisukari kinapanda haraka. Anasema kuna wagonjwa waliokufa baada ya kuacha kutumia dawa zao.
Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele katika kupigia debe tiba ya Babu bila kufanya uchunguzi yakinifu. Ndio, duniani kuna fikra dhanifu na fikra yakinifu. Ya ‘ Babu’ wa Loliondo ni dhania iliyopaswa kuhojiwa kabla ya kupigiwa debe.
Hivi, wanahabari wetu wanashindwaje mpaka hii leo, kuwahoji madaktari bingwa kwenye maradhi kama UKIMWI, kisukari, na mengineyo. Madaktari hawa wako Agha Khan, wako Bugando, Mount Meru na kwengineko. Hivi, Watanzania wenzetu hawa, katika kazi zao, mpaka hii leo hawana cha kusema, cha kitaalam juu ya Tiba ya Babu? Au media imechagua kuficha ukweli?
Tunajua, kuwa habari za ‘ Babu wa Loliondo’ zinauza magazeti kwa sasa. Lakini, ni dhambi na kutoitendea haki nchi yetu kama tutaamua kufanya biashara na afya za watu wetu. Ni laana kubwa.
Ona sasa, Watanzania kwa maelfu wanakwenda gizani bila kuhoji, au kusaidiwa kuhoji. Katika dunia ya sasa ya Sayansi na Teknolojia hatuwezi kwenda mbele kwa kuendekeza ‘ Abrakadabra’ kama hizi za Loliondo.
Huu ni wakati, kwa Wizara na waziri mwenye dhamana, kutoa tamko rasmi juu ya ukweli kuhusu tiba hiyo ya Babu. Na kama ‘ Babu’ ataruhusiwa aendelee na tiba yake kwa wenye imani, basi, Babu huyu asaidiwe kuhamishia shughuli zake Arusha mjini. Lifanyike hilo ili tunusuru maisha ya Watanzania wenzetu walio katika hatari ya kupata maradhi mapya katika mazingira ya sasa ya Loliondo.
Tunayasema haya kwa mapenzi ya nchi yetu, basi.
Maggid,
Iringa,
Ijumaa, Machi, 25,2011
http://mjengwa.blogspot.com
Friday, March 25, 2011
Dawa ya Babu Sasa Habari ya Kimataifa
Watu Wanaaapa Inafanya Kazi! Nasikia hata wazungu wanakwenda Loliondo sasa!
Kwenye Part 2 msikie Babu akisema mwenyewe kuwa dawa yake inatibu, HIV/AIDS (UKIMWI), Diabetes (Kisukari), Cancer (Saratani), Asthma (Pumu), Kifafa (Epilepsy). Anasema kuwa mtu anahitaji kikombe kimoja tu cha dawa. Mungu ameweka dawa kwenye. Anaseme kuwa lazima unywepale Loliondo, huwezi kupeleka nje ya pale la sivyo haitafanya kazi. Anasema kuwa Mungu amemwambia kuwa watu watatoka mbali hadi Ulaya, Asia kuifuata.
Kwa UKIWMI anasema mwenye UKIMWI atapona baada ya siku saba.
Thursday, March 24, 2011
Mh. Lukuvi na Rosemary Nyerere Nao Wapata Kikombe cha Babu
Dawa ya babu OYEEEEE!
Waziri wa Nchi Ofisi ya Wazri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi (wa pili kulia) na Rosemary Nyerere (kulia) wakipata 'kikombe cha babu' kutoka kwa mchungaji mstaafu wa KKKT , Ambilikile Mwasapila (kushoto) waliopkwenda Loliondo. (Picha kwa Hisani ya Michuzi Blog)Friday, March 18, 2011
Lowassa Naye Apata Dawa ya Babu Loliondo
*****************************************************************************
Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile aka. BABU akipima dozi

Msongamano wa wangonjwa na wananchi wakienda kupata dosi. Dozi ilikuwa shs 500/- tu. Sijui kwa sasa ni bei gani.
Picha na Habari kutoka Michuzi blog:
Lowassa apata kikombe Loliondo, huduma zaimarishwa, bei ya mabasi Ubungo zapanda
Source: Gazeti la Mwananchi
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa juzi alipata tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile katika Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale, Loliondo, mkoani Arusha.
Lowassa alifika katika eneo hilo mchana akiwa na viongozi kadhaa wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Serikali kisha kupata kikombe kimoja chenye dawa kinachotolewa na mchungaji huyo kwa ajili ya tiba.
Tofauti na viongozi wengine, Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), Jimbo linalopakana na Kijiji cha Samunge, alikwenda huko akiwa na viongozi mbalimbali wakiwamo viongozi wa dini na baadhi ya wapigakura wake.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Lowassa alithibitisha kwenda Loliondo na kuwataja viongozi wa dini alioambatana nao katika msafara wake kuwa ni Askofu Msaidizi wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini, Dk Frederick Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Dayosisi ya Kaskazini Kati (Arusha), Mchungaji John Nangole.
Katika ramani ya utendaji kazi ya KKKT, Jimbo la Masai Kaskazini ndipo kilipo Kijiji cha Samunge ambako ni makazi ya Mchungaji Mwasapile.
“Ni kweli, nimekwenda pale na wapigakura wangu pamoja na viongozi wa dini, Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Dk Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Mchungaji Nangole,” alisema Lowassa na kuuliza: “Kwani hiyo nayo ni habari jamani?”
Baada ya Lowassa kufika katika kijiji hicho akiwa na ujumbe wake, aliongoza moja kwa moja hadi kwa Mchungaji Mwasapile na kuzungumza naye kisha akapata kikombe cha tiba na kuondoka.
Kabla ya Lowassa kwenda kupata tiba, amekuwa akitoa msaada wa nauli kwa wagonjwa mbalimbali wa jimbo lake kwenda kwa mchungaji huyo ambaye dawa yake inadaiwa kutibu magonjwa ya saratani, kisukari, pumu, shinikizo la damu na Ukimwi.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:








































