Showing posts with label Shelter. Show all posts
Showing posts with label Shelter. Show all posts

Wednesday, June 10, 2009

Walipa Kodi Marekani Hebu Chekini!

Walio Marekani wataelewa. Unakuta mtu eti maskini anaishi kwenye projects, hafanyi kazi anapokea welfare check lakini ana gari, anavaa nguo na viatu vya bei mbaya na kuwa na simu latest! Huko wewe unasota minimum wage na huna kitu cha maana cha kuonyesha!

*****************************************
This is classic. Our TAX Dollars at work!

Recently Michelle Obama went to serve food to the homeless at a government funded soup kitchen .

Cost of a bowl of soup at homeless shelter $0.00 dollars

Having Michelle Obama serve your soup $0.00 dollars

A homeless person who is receiving government funded meals while taking a picture of the first lady using his $300 Black Berry cell phone $$$$ Priceless
********************************************************************


Friday, February 29, 2008

Casting Call ya ajabu yasababisha serikali iingilie!

Hillbillies

Hapa Marekani kuna jimbo inaitwa West Virginia. Hiyo jimbo inajulikana kwa watu washamba sana (hillibiilies). Wanavyosema kwenye milima ya kule ni jambo la kawaida mtu kufunga ndoa na ndugu yake, hatimaye watoto wanakuwa na nyuso za ajabu na hawana akili sana.

Sasa kuna sinema ambayo inaanza kutengenezwa mwezi ujao, inaitwa Shelter. Stelingi wake ni Julianne Moore. Sasa katika kutafuta extras, mtu aliyekabidhiwa hiyo kazi alitangaza casting call ya ajabu.

Donna Belajac Casting iliyoko Pennsylvania ilitangaza kuwa inatafuta, watu warefu mno, watu wafupi, watu wenye shepu za ajabu na uso za ajabu. Walisema pia kuwa wanatafuta watu wenye kasoro kwenye miili yao hasa macho. Pia walikuwa wanatafuta viwete wasiohitaja msaada maalum.

Haya hiyo siyo mbaya, lakini aliharibu aliposema anatafuta watu ambao wanafanana na 'inbred' yaani waliozaliana wenyewe kwa wenyewe. Tena waliongeza watu wanafanana na 'holler people' ni kabila fulani ya ya wazungu wanaokaa kwenye milima ya West Virginia.

Hapo huyo Donna Belajac kawasha moto! Viongozi wa West Virginia walichachamaa maana walisema kuwa ni stereotype kuamini kuwa watu wa West Virginia ni inbreds na washamba! Gavana Joe Manchin wa West Virginia alilaani hiyo sinema na hiyo casting call vikali! Pia viongozi wengine waliingilia.


Mwisho watengeneza sinema ya Shelter, waliomba msamaha kwa watu wa West Virginia na pia walifukuza kazi kwenye hiyo sinema, hiyo kampuni ya Donna Belajac! Duh!

Kwa habari zaidi za mkasa huo someni: