Showing posts with label Homeless. Show all posts
Showing posts with label Homeless. Show all posts

Saturday, January 30, 2016

Shamba la Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye Mabwepande Imevamiwa!

 Nimepata kwa E-Mail:

WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe. Fredrick Sumaye,ameiangukia serikali na kuomba msaada baada ya wananchi kuchukua sheria mkononi na kuvamia eneo lake la ekari 33 lililopo Mabwepande katika Manispaa ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Serikali imemuahikikishia Mhe. Sumaye kuwa haina mpango wa kumkandamiza mtu mnyonge wala tajiri hivyo itahakikiha inatoa haki kwa kila mmoja baada ya wiki mbili kwa kua imesikiliza pande zote mbili katika mgogoro huo.

Akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya wananchi wa kitongoji cha Kimondo mtaa wa mji mpya Kata ya Mabwepande na Mhe.Sumaye Dar es Salaam leo asubuhi, Mkuu waWilaya ya Kinondoni Paul Makonda alisema ili kumaliza mgogoro huo ambao Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye ameiomba serikali kuingilia kati ni lazima busara kutumika. Alizitaka pande hizo mbili kuiachia serikali kwa wiki mbili ili kutafuta njia bora ya kumaliza tatizo hilo huku wananchi wakitakiwa kuache kuendelea na ujenzi na kugaiana maeneo katika shamba hilo.

“Serikali ya Rais Magufuli ni sikivu na ndio maana ilikuwa tayari kumsikiliza Waziri Mkuu wetu Mstaafu Sumaye na kusikiliza wananchi ili kutenda haki tunatambua migogoro ya ardhi ilivyokuwa na athari kwa jamii hatuna mpango wa kumkandamiza tajiri wala mnyonge,”alisema. Alisema katika eneo hilo anajua jinsi wananchi walivyotumia nguvu katika kuwekeza ujenzi na rasilimali zao lakini kwa sasa wasitishe shughuli hizo na kuendelea kugawana maeneo na Sumaye pia kuacha uwekezaji ili kutafuta suluhu.

Zipo njia nyingi tutazitumia kumaliza mgogoro huu ikiwemo kufuata sheria kwa kuangalia iwapo mzee wetu alikiuka taratibu kweli za kumiliki ardhi kama ilivyodaiwa na wananchi hatua gani serikali tuchukue,”alisema. Alisema pia wanaweza kukaa na Sumaye na kuzungumza naye ili kukubali hasara kwa kutoa eneo kidogo na kuwapatia wananchi hao ambao hawana makazi au Manispaa kutafuta eneo mbadala na kuwauzia kwa bei nafuu.

Alizitaka pande hizo mbili kutambua umuhimu wa kulinda amani katika mgogoro huo kwa changamoto zilizopo kutatuliwa bila kutumia nguvu.Makonda pia aliagiza serikali ya kijiji kufanya utambuzi wa wananchi hao wenye makazi katika shamba la Sumaye. Awali katika mkutano huo Mhe. Sumaye alimueleza Mhe. Makonda jinsi serikali ilivyo na kazi ngumu ya kushughulikia migogoro ya ardhi na kuomba kutumia busara zake kumpatia eneo hilo analomiliki kihalali.

“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kama nilivyokueleza awali serikali yetu inakazi ngumu sana hasa kutokana na viongozi wa chini kutokuwa wasikivu na wakweli eneo hili namiliki kihalali nina nyaraka zote na ninalipia kila mwaka na nilikuwa katika mpango wa kutafuta wafadhili ili kuliendeleza kwa kujenga Chuo Kikuu,”alisema. Alisema yeye na familia yake waliuziwa eneo hilo toka mwaka 1997 na anaamini serikali itatenda haki.

Diwani wa kata hiyo Suzan Masawe alisema anauthibitisho kuwa eneo hilo lilikuwa pori na Sumaye alilitelekeza kwa muda mrefu na kusababisha uhalifu ikiwemo wanawake kubakwa,mali za wizi kufichwa na uhalifu mbalimbali. Alisema kutokana na hatua hiyo walimtafuta Sumaye lakini hakuwa na ushirikiano kwakuwa hata alipofanya uwekezaji kwa kuchimba kisima cha maji alikataa kuwapa wananchi .

Suzan alisema kutokana na hasira za wananchi hao kwa kukosa huduma za kijamii kwa muda mrefu ikiwemo eneo hilo kutokuwa na shule,Zahanati wala kituo cha polisi waliamua kuvamia na kujigaia maeneo. Mmoja wa wananchi hao Athuman Mnubi alikiri kweli hawana umiliki halali wa eneo hilo na katika hatua ya kutafuta makazi walivamia msitu huo uliotelekezwa na Sumaye.

Alisema wanaamini kutokana na ahadi ya serikali ya Rais Magufuli katika kupora maeneo yaliyotelekezwa na wawekezaji watasaidiwa. WAKATI huo huo Makonda alisimamisha na kukamata baadhi ya malori ya kokoto na mchanga, wafanyakazi na Mwekezaji wa kigeni kutoka India Sules Waljan wanaochimba mchanga,kokoto na kifusi katika eneo la Mabwepande. Hatua hiyo imekuja baada ya kuona uharibifu mkubwa wa mazingira na alipowahoji wafanyakazi na Mwekezaji huyo kama wanavibali walisema hawana.
Makonda amewafikisha watuhumiwa hao kituo cha polisi cha Wazo Hill ili kutoa maelezo ya kina na kusema kuwa serikali inatumia gharama kubwa kwa uhalibifu huo wa mazingira ambao pia unafanywa katika vyanzo vya maji na matengenezo ya madaraja yanayoharibiwa ni makubwa.

Monday, June 02, 2014

Ubaguzi Marekani!

Mzungu Mbaguzi akilaani weusi kwa kutokupata msaada wa Serikali
Wadau, hapa Marekani watu weusi wana pambana na ubaguzi kila siku.  Hebu ona, huyo mzungu kaenda kuomba Welfare (Yaani hela ya kujikumu kutoka Serikali), kanyimwa halafu ana laani weusi. Huenda walimwona ni mtu mzima ambaye anaweza kufanya kazi ndo maana walimnyima! Au waligundua kaficha hela mahala.  Yaani hapa USA mzungu mchafu kama huyo akienda, akioga na kuvaa vizuri, halafu aende interview atapata kazi kulikwa wewe mweusi uliyesoma na una sifa zote za hiyo kazi!  Halau ana pochi ya bei mbaya! Khaa si aeuze hiyo pochi apate hela ya chakula!

Halafu wengine ni matapeli tu! Hawataki kufanya kazi, kazi kukaa barabarani na kuomba hela! Na hasa wazungu wanapata hela nyingi kwa kuomba! Tena hizo pesa wanazopata haitozwi kodi kama za mtu ambaye anafanya kazi.

Wednesday, June 10, 2009

Walipa Kodi Marekani Hebu Chekini!

Walio Marekani wataelewa. Unakuta mtu eti maskini anaishi kwenye projects, hafanyi kazi anapokea welfare check lakini ana gari, anavaa nguo na viatu vya bei mbaya na kuwa na simu latest! Huko wewe unasota minimum wage na huna kitu cha maana cha kuonyesha!

*****************************************
This is classic. Our TAX Dollars at work!

Recently Michelle Obama went to serve food to the homeless at a government funded soup kitchen .

Cost of a bowl of soup at homeless shelter $0.00 dollars

Having Michelle Obama serve your soup $0.00 dollars

A homeless person who is receiving government funded meals while taking a picture of the first lady using his $300 Black Berry cell phone $$$$ Priceless
********************************************************************