Showing posts with label SuperBowl. Show all posts
Showing posts with label SuperBowl. Show all posts
Sunday, February 03, 2008
Patriots walia! Kumbe siyo PERFECT!
Doh! Yaani jioni hii nimeona watu wanalia kwa masikitiko utadhani wamefiwa! Wanalia, wanatapika, wanasema miii yao imekufa ganzi! Yaani! Kisa cha masikitiko....Patriots wameshindwa katika SuperBowl. New York Giants wamewashinda 17-14 tena katika sekunde za mwisho wa mchezo!
Kama Patriots wangeshinda ingekuwa historia maana msimu wote hawakuwahi kushindwa.
Mimi nasema kushindwa kwao ni laana ya Bridget Monahan! Kwa wasiojua Quarterback wa timu ya New England Patriots, Tom Brady, alimtupa mpenzi wake mwenye mimba, mcheza sinema maarufu, Bridget Moynahan kwa ajili ya Supermodel Gisele Bundchen.
Moynahan alijifungua mtoto wa kiume na kwa hasira kamnyima mtoto jina la baba yake.
Na walivyoanza kucheza SuperBowl walionyesha huyo Gisele yuko pale stadium kumshabikia mpenzi wake! Haya, watu bado wanfutamachozi lakini naamini siku zijazo tutasikia watu wanavyomlaani huyo Gisele na Bridget kwa kushindwa kwa Patriots kuwa timu bora katika historia ya American football!
Na sasa wanamlaumu kocha wao Bill Belichick kwa kuvaa sweata nyekundu.
Leo wanacheza Superbowl aka The Stupid Bowl!

Leo timu yetu maarufu ya Football, The New England Patriots watacheza katika SuperBowl. Wapinzani wao ni timu ya New York Giants. Wanacheza huko Glendale, Arizona.
Timu yetu haijashindwa katika mchezo hata moja msimu huu. Wakishinda Superbowl watukuwa wamevunja rekodi katika mchezo huu.
Mchezo wa football siipendi. Si ule mpira wa miguu wanaocheza Tanzania, Soccer, hii inafanana zaidi na rugby, kazi kuumizana! Wanaume wanakuwa vichaa kipindi hiki. Leo kuna Superbowl party nyingi tu.
Huwezi kupata tiketi kwenda kuona Superbowl laivu kwa chini ya dola $2,000! Na watu wako tayari kulipa hizo pesa kwa jinisi walivyo washabiki! Wako tayari kuingia katika madeni ili waende.
Katika msimu wa football kuna kuwa na 'football widows', yaani wajane wa Football. Kwa maana hiyo wanaume wao walivyo na ushabiki na mchezo hawajali wake zao.
Akina dada wanaotaka wachumba wanashauriwa wajifunze lugha ya football, Touchdown, field goal penalty. Halafu wajidai kuwa wanapenda huo mchezo. Hapo utampata mwanaume!
Haya tutaona nani atashinda hiyo SuperBowl. Wengi waniita The Stupid Bowl kwa jinis watu wanavuoingiliwa na kiwewe! LOH!
Kwa habari zaidi za SuperBowl soma:
http://www.nfl.com/superbowl
Subscribe to:
Posts (Atom)



