Sunday, February 03, 2008

Patriots walia! Kumbe siyo PERFECT!

Tom Brady na wanawake wake (Bridget(shoto), Tom (Katikati), Gisele(Kulia)


Doh! Yaani jioni hii nimeona watu wanalia kwa masikitiko utadhani wamefiwa! Wanalia, wanatapika, wanasema miii yao imekufa ganzi! Yaani! Kisa cha masikitiko....Patriots wameshindwa katika SuperBowl. New York Giants wamewashinda 17-14 tena katika sekunde za mwisho wa mchezo!

Kama Patriots wangeshinda ingekuwa historia maana msimu wote hawakuwahi kushindwa.

Mimi nasema kushindwa kwao ni laana ya Bridget Monahan! Kwa wasiojua Quarterback wa timu ya New England Patriots, Tom Brady, alimtupa mpenzi wake mwenye mimba, mcheza sinema maarufu, Bridget Moynahan kwa ajili ya Supermodel Gisele Bundchen.

Moynahan alijifungua mtoto wa kiume na kwa hasira kamnyima mtoto jina la baba yake.

Na walivyoanza kucheza SuperBowl walionyesha huyo Gisele yuko pale stadium kumshabikia mpenzi wake! Haya, watu bado wanfutamachozi lakini naamini siku zijazo tutasikia watu wanavyomlaani huyo Gisele na Bridget kwa kushindwa kwa Patriots kuwa timu bora katika historia ya American football!

Na sasa wanamlaumu kocha wao Bill Belichick kwa kuvaa sweata nyekundu.

1 comment:

Anonymous said...

Hii ni kawaida ya wanaume! Wanatupa mwanamke mzuri kwa ajili ya mwanamke mbaya! Mbona huyo Bridget baby mama ni mzuri kuliko Gisele.