Sunday, February 03, 2008

Leo wanacheza Superbowl aka The Stupid Bowl!


Leo timu yetu maarufu ya Football, The New England Patriots watacheza katika SuperBowl. Wapinzani wao ni timu ya New York Giants. Wanacheza huko Glendale, Arizona.

Timu yetu haijashindwa katika mchezo hata moja msimu huu. Wakishinda Superbowl watukuwa wamevunja rekodi katika mchezo huu.

Mchezo wa football siipendi. Si ule mpira wa miguu wanaocheza Tanzania, Soccer, hii inafanana zaidi na rugby, kazi kuumizana! Wanaume wanakuwa vichaa kipindi hiki. Leo kuna Superbowl party nyingi tu.

Huwezi kupata tiketi kwenda kuona Superbowl laivu kwa chini ya dola $2,000! Na watu wako tayari kulipa hizo pesa kwa jinisi walivyo washabiki! Wako tayari kuingia katika madeni ili waende.

Katika msimu wa football kuna kuwa na 'football widows', yaani wajane wa Football. Kwa maana hiyo wanaume wao walivyo na ushabiki na mchezo hawajali wake zao.

Akina dada wanaotaka wachumba wanashauriwa wajifunze lugha ya football, Touchdown, field goal penalty. Halafu wajidai kuwa wanapenda huo mchezo. Hapo utampata mwanaume!

Haya tutaona nani atashinda hiyo SuperBowl. Wengi waniita The Stupid Bowl kwa jinis watu wanavuoingiliwa na kiwewe! LOH!

Kwa habari zaidi za SuperBowl soma:

http://www.nfl.com/superbowl

1 comment:

Anonymous said...

Nilijua New York Giants watashinda. Hao New England Patriots walizidi kuringa eti unbeaten! Now they are beaten! LOL!