Saturday, May 26, 2007

Bongowood





Katika dunia ya sinema, mfalme na wa kuiga ni Hollywood. Maelfu ya sinema zimetengenezwa na Hollywood tokea miaka ya 1910's. Lakini siku kila kona ya dunia sinema zinatengeneawa. Wahindi wana Bollywood na waNigeria wana Nollywood. Sasa sisi waTanzania tuna Bongowood.

Ndiyo, tuna BONGOWOOD! Sinema zinaanza kutengenezwa kwa wingi Tanzania, na watu wana hamu ya kujifunza namna ya kuzitengeneza. Si muda mrefu iliyopita, enzi Ujamaa utengenezaji sinema ilikuwa si kitu muhimu kwetu. Wakati huo kutenegeza sinema ilikuwa ghali na serikali ya Ujamaa ilikuwa na kazi muhimu kama kuwapatia wananchi maji safi, elimu na huduma ya afya.

Lakini ziku hizi asante 'digital technology' bei ya kutengeneza sinema imeshuka sana.

Kama makao makuu ya Hollywood iko Los Angeles, California USA, ninapendekeza studio kubwa iwe Bagamoyo. Bagamoyo ni penyewe kwa mambo ya usanii. Kuna Chuo cha wasanii huko Bagamoyo, na mambo mengi.

Baadhi ya Sinema za KiTanzania, zilizotengenezwa Tanzania ni:


1. Simu ya Kifo (2007)
2. Tusamehe (2005) http://www.kibirafilms.com/tusamehe
3. Bongoland (2003) http://www.kibirafilms.com/bongoland
4. Maangamizi the Ancient One (2001) http://www.grisgrisfilms.com/html/maangamizi_-the_ancient_one.html
5.Arusi ya Mariamu (1985) http://www.grisgrisfilms.com/html/marriage_of_mariamu.html
6. Mama Tumaini (1987)
7. Mogambo (1953) http://www.imdb.com/title/tt0046085/
8. YombaYomba (1985)
9. Darwin’s Nightmare (2005) http://www.imdb.com/title/tt0424024/
10. Surrender (2000) http://www.newsreel.org/nav/title.asp?tc=CN0132&s
10. These Hands (1992)
11. Gubu la Wifi
12. Four Weeks in Tanzania (2004) http://www.studentfilms.com/film/get.do?id=978
13. These Hands (1992)13. Girlfriend (2004)
14. Fimbo ya Mnyonge (1974)
15. Tumaini -Childhood Robbed (2005) http://www.abantuvisions.com/StoryPage.php?StoryID=3

3 comments:

Anonymous said...

Dada Chemi, napenda kukuarifu kuwa siku hizi hapa tulipo Bongo sinema zetu ni za kumwaga (nyingi mno) na zinaburudisha kweli kweli. Baadhi ya waigizaji mahili wahapa ni akina Ray, Blandina, Kanumba,n.k.
Huyu kanumba hivi karibuni alishirikiana na Wanaijeria kutoa sinema ya Dar to Lagos waliyoigiza hapa Dar na Lagos.Nakuunga mkono kuwa huenda hii imefanikiwa kwa kasi kutokana na Digital Technology
kurahisisha gharama za utengenezaji.

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 4:18PM, ni kweli sinema ziko nyingi Bongo siku hizi. Niliziona nilivyokuwa huko na za waNigeria ndo usiseme. Nollywood hiyo!

Akina Ray, Kanumba na Blandina nimewasikia pia.

Anonymous said...

HEMED MSHAMU MANYINJA tumeona maendeleo ya technologia asa ktk mfumo digital lkn ninge waomba wasanii watunge stor zenye mantik ilikuvuta soko la filamu watanzania wanahamu ya kuona maigizo yanayo wagusa ningesema watunge filamu kama ya mzee yomba yomba ambayo ipo ktk maadili ya kitanzania sio ili mradi mkono huende kinywani wakifanya hivyo naamini soko la bongo movies litakuwa na kuleta tija na maendeleo ktkt jamii ya kitanzania