Friday, May 18, 2007

Mheshimiwa Sumaye akipokea DVD za Bongoland na Tusamehe



Wiki hii nilibahatika kumkabidhi aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania enzi za Rais Mkapa, Mheshimiwa Frederick Sumaye, DVD za sinema ya Tusamehe na Bongoland. Yeye ni jirani yangu hapa Cambridge, Massachusetts. Anasoma Harvard University.

Mheshimiwa Sumaye alifurahi sana kuona DVD hizo na alisema ingekuwa vizuri vijana wote Tanzania wazione kwani zina ujumbe nzito sana.

Katika sinema ya Tusamehe waTanzania waliofanikiwa kimaisha Marekani wanakumbwa na ugonjwa wa UKIMWI, na katika Bongoland, MTanzania anapambana na maisha Marekani.

Sinema hizo zimetengenezwa na mwanafilamu wa kiTanzania aishio huko Minnesota, Josiah Kibira. Kwa habari zaidi za sinema hizo na hata kununua DVD zake, tembelea....
http://www.kibirafilms.com/index.html

8 comments:

Anonymous said...

Nimepata wasaa wa kuangalia both DVDs zina maudhui mazuri and its a very good start for upcoming producer bwana Josiah. If there is anything he needs to change ni kujaribu kuepuka ku-hire the same cast kwa kila movie kwa sababu hiyo inaondoa maana ya sinema na kugeuza kuwa kama mchezo wa kuigiza wa Mzee Jongo na mama Tamasha maana kila kukicha waigizaji ni hao hao. Kuna waigizaji ambao hawakuwa confortable kwenye camera kama Salome ambaye alionyesha kuwa ni mgeni ukimsikiliza utagundua kuwa alikuwa amekariri script bila kuchanganya na kipaji ambapo for her case she didn't have anything to add. Mama kurusumu, I think this movie didn't help u either kwa kuwa hukuonyesha kama una uzoefu hata pale kwenye ufunguzi wa awali ulionyesha wazi unafuata camera ili uonekane.. you need to be bigger than that to succeed. My best actor was Bwana Bilantanya.. he was very comfortable kama mtu ambaye amekuwa aki-act for life.. keep it up naamini you can do it for living.. Just my two cents

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 6:50pm, asante sana kwa maoni yako, nina shukuru. Ila kwenye casting naona mtu moja tu ka-acti kwenye sinema zote mbili, naye ni Robert Kataraia.

Anonymous said...

Huyo anonymous wa juu hapo hajaona hizo sinema. Kama Da Chemi alivyosema ni mtu moja ambaye unamwona katika sinema zote mbili. Lakini mbona kwenye sinema nyingi kuna cast recycling. Haina tatizo.Bi Blandina alijitahidi sana for first time acting na Bilantanya kajitahidi sana na mbona sijaona kama Chemi anafuata camera. Camera ilimfuata yeye. Keep it up Bwana Kibira.

Africa360 said...

Huyu jamma youko wapi sikuhizi?

Chemi Che-Mponda said...

africa360, kama unaulizia kuhusu Mheshimiw Sumaye, anasoma Harvard University. Karibu anamaliza masomo yake.

Anonymous said...

Wewe Chemi kwa nini umefuta posti yangu niliyoandika kuhusu ubadhirifu aliofanya Sumaye alipokuwa madarakani?

Unknown said...

Hi Dada Chemi je kwa walio bongo wawezaje kuzipata? kwa sasa niko Berlin je zapatikana kwa hapa? waweza pia kujibu pitia blog za www.bernardrwebangira.blogspot.com

Chemi Che-Mponda said...

Bongo pix, Kibira Films bado wanafanya mipango ya distribution kusudi mweze kuzipata Bongo. Ila kama uko Berlin unaweza kuagiza hapa:

http://www.kibirafilms.com/tusamehe/store.html