Sunday, December 07, 2014

Mama Bishanga Ampongeza Diamond Platinum

MAMA BISHANGA AMPONGEZA DIAMOND
Nimeona nisikae na duku duku la pongezi zangu kwa kijana wetu Diamond kwa kutwaa tunzo tatu kwa mpigo wiki iliopitai huko South Africa, huo ni ushindi mkubwa sana kwa Diamond, mama yake na sisi sote kama taifa la Tanzania. Mimi kwa niaba ya wazazi wenzangu bwana mdogo nakupongeza sana na ninampongeza sana mama yako Sandra kwa kukuandaa katika fani ya muziki, nguvu yake ndio mafanikio yako. Hii inanikumbusha hata mimi nilivyokuwa ninaandaa kazi zangu za sanaa wakati nafundisha Chuo cha Uhazili Tabora nilimtumia mwanangu Kenny (Hery) kuigiza nae na kucheza nae ili kumuelekeza mkondo uigizaji. Na hata Natasha alifanya hivyo kwa mwanae Monalisa, nz wengineo wengi, kumbe ni jambo zuri kwa wazazi kufanya hivyo kwa watoto wao kwa fani, elimu na ujuzi mbalimbali ili kuwapa msingi bora.
 Mimi niakukubali sana kimuziki na kimaadili na upendo na heshima unayompa mama yako na jamii nzima, na hii ngololo, ngololo, ngoololooo hii kibko hata sisi wazazi wako hii tunaisakata kama kazi!

Keep it up young boy from Tanzania! Home , sweet home Tanzania!

Mama Bishanga/ Mrs Marolen
Ohio/ USA

Mama Bishanga aka. Mrs. Christina Marolen

No comments: