Saturday, December 06, 2014

Kifo cha Eric Garner - Aluyeuawa na Polisi Mjini New York

Wadau, nina uchungu sana na kifo cha Mmarekani mwesui, Eric Garner (42). Aliuwawa na polisi wabaguzi. Walisema alikuwa anauza sigara kwa senti 50 kila moja, bila kulipa kodi.  Yaani hiyo ni kosa ya wao kuu mtu! Na siku hiyo walivyomwua hakuwa anauza sigara! Basi tu, walikuwa wanawinda weusi!


Wadau, marehemu nilikuwa namfahamu. Nilimwona mara kadhaa huko Staten Island, New York.  Pale alipouwawa kuna duka la vipodozi na mahitaji mengine. Mara nyingi ilikuwa nikimwona anatabasamu, alikuwa na umbo kama marehemu mume wangu ila mrefu zaidi.  Bora alikuwa anauza hizo sigara kuliko kuwaibia watu au kuwa jambazi. Mara la mwisho kumwona Eric akiwa hai ni hiyo hiyo Julai, alikuwa na mke wake na watoto.

Wiki hii polisi aliyemwua, mzungu, yule aliyemkaba kaachiwa bila hatia.  Yule polisi mshenzi anaitwa Daniel Pantaleo. Ukiona video unaona kabisa jinsi Panataleo anavyomwua, na utalia ukimsika ukisikia anasema, "I Can't Breathe!" (Siwezi kupumua).  Na ni wazi kuwa Pantaleo alikuwa na chuki ya siku nyingi na marehemu.  Yule kijana aliyepiga video ya mauaji ya Eric kafungwa!  Jamani!

Watu wanaandama kwa  wingi sasa karibu kila mji mkuu hapa Marekani! Watu weusi wameuawa na polisi waliowaua wanaachiwa. Ni kama vile maisha ya mtu mweusi haina thamani!  Ni maajabu, weusi na wazungu wanaandana pamoja kudai haki kwa watu weusi! Wana hasira maana wengi wameuawa na hakuna anayedhibitiwa. Tusiwasahau, Michael Brown, Sean Bell, Trayvon Martin, Amadou Diallo, Tamir Rice, na wengine wengi!

Mwenyezi Mungu atulinde hapa Marekani!

Mauaji ya Eric Garner, Staten Island, New York
Kwa habari zaidi na Video ya Mauaji ! BOFYA HAPA:

1 comment:

Anonymous said...

Very very sad that this kind of thing still keeps happening in this day and age. Rest in Peace Eric. What happened to the land of the free?