Saturday, December 20, 2014

Mbunge Ishungisa Afariki na Mjukuu Wake

MBUNGE ISHUNGISA AFARIKI NA MJUKUU WAKE

Na Happiness Katabazi

ALIYEKUWA Mbunge wa Pili , wa Jimbo la Karagwe ambaye alifariki Jana jioni, Laurent Ishungisa , mjukuu wake ambaye ni Mfanyakazi wa Kampuni ya Simu ya TIGO, Gody Tibyampasha naye amefariki alfajiri ya kuamkia Leo  Katika eneo la Skansaka karibu na Mitambo ya IPTL Wilaya ya Kinondoni  kwa ajali ya Gari.

Kwa mujibu wa Msemaji wa msiba wa Inshungisa, Medard Birusya  alisema Gody alikutwa na umauti huo wakati akiendesha gari lake wakati akitokea kwenye msiba wa Babu yake Mabibo Hosteli kurudi nyumbani wake Tegeta kupumzika.Miili ya marehemu wote imeifadhiwa Katika Hospitali ya Mwananyamala.

Birusya akitangaza Ratiba ya misiba hiyo miwili jinsi watakavyoiendesha hivi punde nyumbani kwa Mtoto wa marehemu Ishungisa, Grace Byampanju eneo la Mabibo Hosteli, alisema msiba wa mbunge Ishungisa uliokuwa ukifanyika Mabibo Hosteli kuanzia Kesho asubuhi utaamishiwa nyumbani kwa wazazi wa marehemu Gody eneo la Tegeta kwasababu Mama Mzazi wa Gody ni Mtoto pia wa marehemu Ishungisa.Baba wa Gody ni Daktari Mstaafu  Dk. Dominic  Tibyampasha.

Birusya alisema , Jumatatu miili ya marehemu ambao ni Babu na Mjukuu wake itaagwa Tegeta na Kisha itasafirishwa kupelekwa Wilayani Karagwe kwa ajili ya kuzikwa.

Birusya alisema Mbunge Ishungisa atazikwa Disemba 24 Mwaka huu ,Katika Kijiji Cha Nyakaiga na mjukuu wake marehemu Gody ambaye ameacha Mke na Mtoto wa Miezi mitatu atazikwa Disemba 25 Mwaka huu  Katika Kijiji Cha Kiruruma. Ni masikitiko makubwa.Mungu tunaomba utupe moyo wa subira na uvumilivu maana huyu Israel Mtoa roho za watu anafanyakazi yake bila huruma.

Ishungisa alifariki Disemba 19 mwaka huu, nyumbani kwa mwanae Grace, Mabibo Hosteli baada ya kuugua kwa muda mrefu.Miili ya marehemu wote imeifadhiwa Katika Hospitali ya Mwananyamala Dar Es Salaam.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Disemba 20 Mwaka 2014.

No comments: