Thursday, January 14, 2016

Maombi ya Kumombea Rais Magufuli na Serikali Yaka Mjini Mwanza

Viongozi mbalimbali wa dini wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (wa pili kushoto walioshikilia bendera), katika Maombi ya Kumuombea Rais Magufuli na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo @Binagi Media Group (BMG)
Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza kwa kushirikiana na Umoja wa Maaskofu kutoka Jijini Dar es salaam jana January 13,2015 ulifanya Mamombu Maalumu ya Kumuombea Rais wa wa awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Wasaidizi wake.

Maombi hayo yalifanyika katika Uwanja wa Furahisha Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali na Dini huku pia wananchi wakijumuika pamoja na waumini wa dini mbalimbali katika maombi hayo.

Mgeni Rasmi katika maombi hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae katika hotuba yake, aliwasihi Watanzania wote kuendelea kuliombea Taifa ili kuondokana na vikwazo mbalimbali ambapo alidokeza kuwa kupitia maombi kama yaliyofanyika jana, migogoro mbalimbali ikiwemo ya kisiasa kama iliyopo Zanzibar itamalizika.

Viongozi mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza Askofu Charles Sekelwa, Makamu wake Zenobius Issaya pamoja na Kiongozi wa Kundi la Maaskofu kutoka Jijini Dar es salaam la Good News For all Ministry Askofu Dr.Charles Gadi pamoja na viongozi wengine wa dini kutoka mikoa mbalimbali nchini waliliombea Taifa na kuhimiza utuliza nchini.

Wasaidizi wa wa Rais Maguguli ambao ni pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu, Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu Mhe.Othman Chande, Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai, Mawaziri pamoja na viongozi wengine wa Serikali wa awamu ya tano waliombewa ili kuliongoza vema taifa kwa kuendana na kasi ya Rais Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, ia maombi hayo yalijumuisha toba kwa taifa, kumuomba Mungu kukomesha mauaji ya Vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na kuombea taifa mvua zisizo na madhara. 
Viongozi mbalimbali wa dini wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (Wa tatu kushoto) katika Maombi ya Kumuombea Rais Magufuli na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wa dini
Maombi ya kuliombea Taifa yaliyofanyika Jijini Mwanza jana
Viongozi mbalimbali wa dini wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Kulia ni Mwenyekiti Msaidizi wa Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza Zenobius Isaya akiwa katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Mwenyekiti Msaidizi wa Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza Zenobius Isaya akiwa katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Mmoja wa Viongozi wa dini akiwa katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza Askofu Charles Sekelwa  akiwa katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Kiongozi wa Kundi la Maaskofu kutoka Jijini Dar es salaam Askofu Dr.Charles Gadi akiwa katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Viongozi wa dini
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akizungumza katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akizungumza katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Kwaya ya EAGT Mabatini Jijini Mwanza ikitumbuiza katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Wanahabari katika kunasa habari kwenye Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Meneja wa HHC Alive Fm Radio ya Jijini Mwanza (Kulia) akiwa pamoja na GB Pazzo (Kushoto) katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.

No comments: