Friday, January 15, 2016

Taswira Mbovu ya Barabara ya Market Street Mjini Mwanza

Hii ni barabara inayotegemewa na daladala za Bwiru-Kisesa, Airtport- Kishiri pamoja na Ilemela-Kishiri hii ikiwa ni kwa upande wa daladala. Lakini pia ikitegemewa na watumiaji wengine wa vyombo vya moto vya binafsi.
Ni barabara iliyotumika pia na wakazi wengi wa Jiji la Mwanza wakiwa wanatoka katika mizunguko yako ikiwemo kutoka Soko Kuu la Jiji la Mwanza. Kama inavyoonekana katika picha inahitaji msaada maana wakati huu wa mvua imeharibika sana.

"Hii barabara inaharibika mara kwa mara kutokana na mitaro iliyopo hapa kuziba mara kwa mara kutokana na wafanyabiashara katika maeneo haya kuwa na tabia ya kutupa makopo mitaroni na hivyo kusababisha mitaro kuziba na hivyo mvua ikinyesha maji yanajaa katika barabara hii na hatimae kusababisha hali hii unayoiona". Binagi Media Group imeeleezwa na baadhi ya wafanyabiashara waliopo jirani na barabara hiyo.

Watumiaji wa barabara hiyo wameiomba halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana kushughulikia ukarabati wa barabara hiyo pamoja na kusimamia suala la usafi ili kuzuia uchafu kutupwa katika mitaro iliyo katika barabara hiyo ili kuzuia kuziba na hatimae kusababisha uharibifu katika barabara hiyo.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG

No comments: