Saturday, November 26, 2016

Aliyekuwa Rais wa Cuba , Fidel Castro Afariki Dunia

Rais Castro na Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1977
Aliyekuwa Rais wa Cuba, Fidel Castro, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90.  Castro alifariki usiku wa kuamkia leo.  Mdogo wake, Rais Raoul Castro aliwatangazia waCuba kuwa Castro amefariki saa nne na nusu usiku.  Alisema kuwa maiti ya kaka yake itachomwa moto leo (cremation) huko Cuba. Kutakuwa na Misa ya kumkumbuka  Taifa la Cuba itakuwa na siku kadhaa za kuomboleza.
Rais Raoul Castro alivyowantangazia wananchi:
The commander in chief of the Cuban revolution died at 22:29 hours this evening (03:29 GMT Saturday)," he said. "Towards victory, always!" he added, using a revolutionary slogan.
Marehemu Castro anakumbukwa kwa kuwa Dikteta. Alipindua serikali ya Cuba mwaka 1959, na hakutoka madarakani hadi mwaka 2006.  Alimwachia madaraka mdoo wake Raoul.  Castro alifanya mengi kusaidi nchi za Afrika ikiwemo Tanzania. Nchi ya Marekani waliweka vizuizi vingi juu ya Cuba ili kujaribu kumkomesha Castro lakini walishindwa.
Video ya Ziara ya Rais Castro nchini Tanzania kwa hisani ya APNo comments: