Saturday, December 17, 2016

Naibu Katibu Mkuu Mpya wa CCM Akagua Mali za Chama Dodoma

MPOGOLO AKAGUA MALI ZA CHAMA LEO MJINI DODOMA, LUHWAVI AMKABIDHI KILA KITU HADI MSAIDIZI
 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, kuhusu jengo la mikutano la CCM, lililopo Kilimani mjini Dodoma wakati Naibu Katibu Mkuu huyo mpya alipotembelea jengo hilo akiwa katika ziara ya kukagua mali za CCM, leo. Kushoto ni Mkuu wa Utawala Makao Makuu ya CCM, Innocent Msena na kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utumishi na Uendeshaji Makao Makuu ya CCM Filbert Mdaki.
 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, kuhusu jengo la mikutano la CCM, lililopo Kilimani mjini Dodoma wakati Naibu Katibu Mkuu huyo mpya alipotembelea jengo hilo akiwa katika ziara ya kukagua mali za CCM, leo. kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utumishi na Uendeshaji Makao Makuu ya CCM Filbert Mdaki.
 Mafara wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo ukiwa mbele ya jengo hilo la mikutano la CCM
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo, akimoji jambo, Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara Rajabu Luhwavi baada ya kukagua jengo hilo, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma.
KIWANJA
🔻
 Meneja wa Miliki wa Makao Makuu ya CCM, Abdallah (kulia) Msangi akimpatia maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (wapili kushoto), alipoenda kukagua kiwanja cha CCM kilichopo eneo la Kilimani mjini Dodoma, akiwa katikaziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi.
 Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utumishi na Uendeshaji Makao Makuu ya CCM Filbert Mdaki akiongeza maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo alipoenda kukagua kiwanja cha CCM kilichopo eneo la Kilimani mjini Dodoma, akiwa katikaziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi, akimuonyesha mwisho wa shamba la CCM, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (wapili kulia), Naibu Katibu Mkuu huyo alipoenda kukagua kiwanja hicho kilichopo eneo la Kilimani mjini Dodoma, akiwa katikaziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma, leo.

NYUMBA YA CCM YA NAIBU KATIBU MKUU-BARA
🔻
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akiwasili kukagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama, mkoani Dodoma, leo
 Mkuu wa Utawala Makao Makuu ya CCM, Innocent Msena akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, aliyefika kukagua nyumba ya Chama atakayoishi, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo
 Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utumishi na Uenedeshaji Filbert Mdaki akionyesha sehemu ya jikoni, wakati Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo alipokagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama leo mjini Dodoma. Kushoto ni Luhwavi
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akikagua meza kwenye jiko, alipokuwa akikagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma leo. Kulia ni Msaidizi Msaidizi wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mbwana Kambangwa.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akikagua kabati la jikoni, alipokuwa akikagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma leo
 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo wakati wakiizunguka kuikagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mpogolo alipokuwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo.
 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo baada ya kuikagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mpogolo alipokuwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo.

KUKAGUA MAGARI WHITE HOUSE
🔻
 Msafara wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo na Rajabu Luhwavi, ukiwa umepumzika kwa mda katika jengo la White House la Makao Makuu ya CCM kabla ya kuanza kazi ya kukagua magari, Mpogolo alipokuwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rodrick Mpogolo (wapili kushoto), akipatiwa maelezo na Fundi wa magari, Ramadhani Mbelwa (kushoto), kuhusu hali ya magari yaliyoharibika, Mpogolo alipokuwa akikagua magari hayo akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo amhoji jambo Fundi wa magari ya Chama, Ramadhani Mbelwa (kushoto), alipokuwa akikagua magari mabovu ya Chama, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo. Kulia ni Luhwavi.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akionyeshwa gari lililofunguliwa boneti, kupata uthibisho wa gari tatizo la gari, alipokuwa akikagua magari mabovu ya Chama, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akimshukuru Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi baada ya kumalizika kazi ya kukagua baadhi ya mali za Chama, mjini Dodoma leo.
KUNZIA SASA HUYU NDIYO BOSS WAKO, SIYO MIMI TENA: Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimtambulisha aliyekuwa Msaidizi wake, Mbwana Kambangwa(kulia), kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo kabla ya kuagana, mwishoni mwa ziara ya Mpogolo kukagua mali za Chama, mjini Dodoma, leo. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

No comments: