Showing posts with label Kichaa. Show all posts
Showing posts with label Kichaa. Show all posts

Tuesday, August 12, 2008

Kichaa aua wagonjwa Muhimbili!

Hayo ni mazito. Hivi hakuna usimamizi katika wodi ya wagonjwa wa akili kweli. Huyo jamaa aliweza kupiga wagonjwa saba na kuua wawili. Na si inabidi wagonjwa 'hatari' watengwe na wengine. Au inakuaje huko siku hizi?

**************************************************************************
Kutoka ippmedia.com

Hospitali Muhimbili: Ni kilio...!

2008-08-12

Na Mwanaidi Swedi na Sharon Sauwa, Jijini

Saa chache tu baada ya madaktari walio mafunzoni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kusitisha mgomo wao na kuamua kurejea kazini kwa masharti, mauaji ya kutisha yametokea ndani ya wodi mojawapo na kuzusha kilio cha aina yake.

Mauaji hayo yametokea jana usiku, ndani ya wodi mojawapo baada ya mgonjwa mmoja kuwatembezea kipigo wenzake na kusababisha vifo vya wawili, huku wengine watano wakijeruhiwa vibaya na wanne kati yao kulazimika kukimbiziwa katika chumba cha upasuaji kwa ajili ya matibabu zaidi.

Tukio hilo la kusikitisha na la aina yake, limetokea jana mishale ya saa 1:30 usiku, wakati mgonjwa huyo wa akili aliyelazwa tangu Julai 28 mwaka huu, alipodaiwa kutwaa chuma moja la stendi ya kuwekea dripu ya maji ya kumtundikia mgonjwa na kuanza kuwatwanga wenzake waliokuwa wamelazwa wote wodini.

Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amemtaja mgonjwa anayedaiwa kufanya tukio hilo baya la kusikitisha kuwa ni Daudi Denge, 24, mgonjwa ambaye aliokotwa toka Mwananyamala tangu tarehe 28 na kufikishwa Hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.

Akasema mtu huyo, aliamka ghafla toka kitandani alikolazwa na kuchukua stendi ya dripu kabla ya kuwapiga wenzake. Amesema kuwa katika tukio hilo, watu wagonjwa wawili ambao ni Bw. Paul Maganga, 30 na Abdul Kadri Abeid, 27, walifariki dunia kwa kuumia vibaya sehemu za kichwani.

Aidha, amesema kuwa mlinzi aliyekuwa zamu, Bw. Mohamedi Hassan, aliweza kupambana na mgonjwa huyo na kufanikiwa kumdhibiti kwa kumnyanga'nya stendi hiyo na kisha kumfunga kamba, hivyo kuzuia maafa zaidi kwa wagonjwa wengine.

Akasema hadi sasa, Polisi wanamshikilia mtu huyo kwa tuhuma zinazomkabili huku uchunguzi wa kina ukiendelea kuhusiana na tukio hilo. Naye Mkurungezi Mtandaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Leonard Lema, amesema kuwa wagonjwa wanne waliojeruhiwa wamepelekwa chumba cha upasuaji kwa majeraha waliyoyapata na mmoja wa tano yungali akiendelea na matibabu wodini.

Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Prof. Lema amesema kuwa uongozi wa Hospitali hiyo unawasiliana na viongozi wa Wizara ya Afya kwa hatua zaidi kuhusu tukio hilo. Amesema kuwa taarifa zaidi zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika kuhusiana na tukio hilo.

Aidha, Prof.lema ameomba radhi kwa jamii na familia zilizopoteza wapendwa wao na pia, wale ambao wagonjwa wao wamejeruhiwa. Hadi sasa, miili ya marehemu wote wawili imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali hiyo ya Muhimbili.

SOURCE: Alasiri

Saturday, April 26, 2008

Update - Mtoto Kichaa akutwa na kichwa cha mtoto


UPDATE - April 29, 2008

Mama mzazi wa mtoto salome yohana aliyechinjwa majuzi akilia kwa uchungu wakati akisaidiwa kuweka udongo kwenye kaburi la binti yake wakati wa mazishi tabata segerea jioni hii.

Picha kwa hisani ya issamichuzi.blogspot.com

**********************************************************


KUTOKA MICHUZI BLOG:

Katika kufuatilia tukio la huyu kijana pichani kukutwa na kichwa cha msichana leo asubuhi kule muhimbili, globu yenu imethibitishiwa kwamba jana usiku msichana mdogo alipotea nyumbani kwao tabata.

Inasemekana leo asubuhi ndugu wa marehemu walikuta kiwiliwili kitupu cha msichana huyo karibu na nyumbani kwao na wakaita polisi ambao wakaupeleka hospitali ya taifa ya muhimbili kwa uchunguzi. huko ndiko kichwa kinachosadikiwa kuwa cha kwake kikakutwa na huyu kijana kwenye geti la chuo kikuu cha tiba cha muhimbili ambapo mlinzi alimkamata.

Afande charles mkumbo, mkuu wa upelelezi kanda ya ilala, amethibitisha yote hayo usiku huu na kwamba kichwa hicho ni cha mtoto salome yohana mwenye umri wa miaka kati ya miaka 3 na 4 na kijana huyu ametambulwa kama ramadhani mussa na anashikiliwa na polisi yeye na mama yake kwa kutuma za kukutwa na kichwa cha mtu kwa kile kilichosemwa kuwa ni mambo ya kishirikina.

Kijana mussa mwenye umri wa miaka 12 inasemekana pia amewahi kukumbwa na mikasa mingine, ikiwa ni pamoja na kuanguka toka paa la kanisa la assemblie of God la msasaani analoongoza mh. getrude rwakatare. inasemekana baada ya mkasa huo ambapo alikuwa na mwenzie wa umri kama yeye walipelekekwa kupimwa akili muhimbili na kuachiwa baada ya kuonekana wana akili timamu.

Mtoto Kichaa Muhimbili - Onyo Picha Zinatisha!





Nimepokea haabri hii ya kusikitisha. Inaelekea ni habari ya kweli. Naomba mlioko Dar mthinitishe kama ni kweli. Je, huyo mtoto kichaa anaitwa nani? Huyo mtoto marehemu ni nani?

Kama ni kweli ni lazima wakubwa walihusika! Wakamatwe wahusika wote na wapewe adhabu ya kifo!
******************************************

On 4/26/08, Dr. M Wrote

Dakika chache zilizopita kumetokea tukio la kusikitisha hapa MPL Muhimbili. Askari mmoja alimsimamisha mtoto wa miaka kama 9 hadi 11 akiwa amebeba kichwa cha mtoto mzuri kama wa miaka mitatu. Kijana yule akatoa kichwa mfukoni na kuanza kula live. Nikifika home nitawatumia picha. Ajabu sana



Kijana mla kichwa cha mtoto alisema kuwa anapeleka zawadi kwa shangazi yake yuko IPPM (siyo psychiatry). Ni kweli tukio hili la kusikitisha sana limetokea.Kichwa ni cha mtoto wa kike mzuri (binadamu), it seemed to be fresh.


Alidai anapeleka zawadi hiyo kwa shangazi yake yuko psychiatry!Mara baada ya kukamatwa, alianza kula kile kichwa live !!! !!! Hata hivyo baadhi ya mashuhuda wanasema aliyekamatwa aliwahi kulazwa psychatry unit.Kwa kuaangalia umbo lake, naye ni mtoto pia; hivyo nina walakini kuwa ni psychiatric patient (unless ana childhood neuropsychiatric/ neurodevelopmental disorders).



Mbona amekuja Muhimbili na si kwingineko. Mfano, angekamatwa maeneo ya Ubungo ama kwingineko; akataja Muhimbili psychiatry tungesikuwa na maswali mengi sana. Kwa upande mwingine, kula kichwa LIVE mbele ya kada mnasi inatia walakini kwa binadamu wa kawaida mwenye akili timamu.



Wazazi/ walezi wa watoto hao (aliyetafunwa na aliyetafuna) wako wapi?Wana maelezo yapi?Pamoja na hayo, kiwiliwili kiko wapi? Kikipatikana chote (kuanzia shingoni hadi miguuni) kitatoa baadhi ya majibu.Polisi wa kutosha (magari mawili) wameondoka na kijana huyo uchunguzi (forensic investigation) unaendelea.



AMINI USIAMINI, NI KWELI YAMETOKEA.