Tuesday, August 12, 2008

Kichaa aua wagonjwa Muhimbili!

Hayo ni mazito. Hivi hakuna usimamizi katika wodi ya wagonjwa wa akili kweli. Huyo jamaa aliweza kupiga wagonjwa saba na kuua wawili. Na si inabidi wagonjwa 'hatari' watengwe na wengine. Au inakuaje huko siku hizi?

**************************************************************************
Kutoka ippmedia.com

Hospitali Muhimbili: Ni kilio...!

2008-08-12

Na Mwanaidi Swedi na Sharon Sauwa, Jijini

Saa chache tu baada ya madaktari walio mafunzoni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kusitisha mgomo wao na kuamua kurejea kazini kwa masharti, mauaji ya kutisha yametokea ndani ya wodi mojawapo na kuzusha kilio cha aina yake.

Mauaji hayo yametokea jana usiku, ndani ya wodi mojawapo baada ya mgonjwa mmoja kuwatembezea kipigo wenzake na kusababisha vifo vya wawili, huku wengine watano wakijeruhiwa vibaya na wanne kati yao kulazimika kukimbiziwa katika chumba cha upasuaji kwa ajili ya matibabu zaidi.

Tukio hilo la kusikitisha na la aina yake, limetokea jana mishale ya saa 1:30 usiku, wakati mgonjwa huyo wa akili aliyelazwa tangu Julai 28 mwaka huu, alipodaiwa kutwaa chuma moja la stendi ya kuwekea dripu ya maji ya kumtundikia mgonjwa na kuanza kuwatwanga wenzake waliokuwa wamelazwa wote wodini.

Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amemtaja mgonjwa anayedaiwa kufanya tukio hilo baya la kusikitisha kuwa ni Daudi Denge, 24, mgonjwa ambaye aliokotwa toka Mwananyamala tangu tarehe 28 na kufikishwa Hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.

Akasema mtu huyo, aliamka ghafla toka kitandani alikolazwa na kuchukua stendi ya dripu kabla ya kuwapiga wenzake. Amesema kuwa katika tukio hilo, watu wagonjwa wawili ambao ni Bw. Paul Maganga, 30 na Abdul Kadri Abeid, 27, walifariki dunia kwa kuumia vibaya sehemu za kichwani.

Aidha, amesema kuwa mlinzi aliyekuwa zamu, Bw. Mohamedi Hassan, aliweza kupambana na mgonjwa huyo na kufanikiwa kumdhibiti kwa kumnyanga'nya stendi hiyo na kisha kumfunga kamba, hivyo kuzuia maafa zaidi kwa wagonjwa wengine.

Akasema hadi sasa, Polisi wanamshikilia mtu huyo kwa tuhuma zinazomkabili huku uchunguzi wa kina ukiendelea kuhusiana na tukio hilo. Naye Mkurungezi Mtandaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Leonard Lema, amesema kuwa wagonjwa wanne waliojeruhiwa wamepelekwa chumba cha upasuaji kwa majeraha waliyoyapata na mmoja wa tano yungali akiendelea na matibabu wodini.

Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Prof. Lema amesema kuwa uongozi wa Hospitali hiyo unawasiliana na viongozi wa Wizara ya Afya kwa hatua zaidi kuhusu tukio hilo. Amesema kuwa taarifa zaidi zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika kuhusiana na tukio hilo.

Aidha, Prof.lema ameomba radhi kwa jamii na familia zilizopoteza wapendwa wao na pia, wale ambao wagonjwa wao wamejeruhiwa. Hadi sasa, miili ya marehemu wote wawili imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali hiyo ya Muhimbili.

SOURCE: Alasiri

5 comments:

Anonymous said...

I am gonna repeat this again.Chemi be original.We have seen this on ippmedia already.There was no reason for you to put it here again.Come on now,you are a journalist,aren't you?Journalists are not supposed to do copy and paste!

Anonymous said...

Sasa Da chemi hujaisoma habari au ndo na wewe niwale watu wakupiga kelele tu! Mbona habari inajieleza kwamba yametokea hayo kipindi ambacho madakatari na wauguzi wako kwenye mgomo! Sasa kama wauguza wako kwenye mgomo kutakuwa na mwangalizi wodini?! Au yupi huyo atakae watenga wagonjwa wa akili, wakati wafanyakazi hawapo (wamegoma)? Nadhani hukuwa na haja ya kujiuliza maswali lukuki wakati habari inajieleza!

Anonymous said...

Hao wakuu wa Muhimbili walikuwa na wajibu wa kulinda hao wagonjwa. Hata ingebidi wakodi askari kutoka kwenye yake makampuni ya kizungu. Washukuru wako Bongo wangekuwa Malekani wangepigwa na lawsuit ile mbaya, na huko Japan/China ingebidi viongozi wajiue kwa aibu.

Anonymous said...

Asante Dada Chemi kwa kuweka hii katika Blog yako, maana mimi na wengine hapa New York tumeina kwenye Blog yako; naliongea na madaktari kwenye psychiatric ward hapa Mount Sinai Hospital -NY, kwanza ni tukio la kusikitisha; bila shaka mgonjwa huyo akuwa kwenye uangalizi wa kutosha, hivyo hakupata madawa tosha ya kuweza kumweka sawa katika tatizo lake, na pia tunajua Intern-doctor ambao kwa Muhimbili wapo karibu sana na wagonjwa walikuwa kwenye mgomo: Pia naomba magazenti na waandishi wake wajifunze lugha za utaalam katika nyanja mbali mbali; Huyo ni MGONJWA WA AKILI na si KICHAA, maana lugha ya kichaa ni kudhalalisha mgonjwa na pia kujeanga hisia ya unyanyapaa (Stigma). Prof. Lema , MD yeye na uongozi wawajibike kwa hili na serikali ibebe mzigo wa kuwalipa ndugu waliopoteza maisha ya ndugu zao wakiwa chini ya ungalizi wa hospitali, pili na mgonjwa aliyesababisha madhara naye akipata nafuu haishtakia hospitali kwa kumpatia huduma duni.
Dada chemi asante kwa kutujuza ya ya nyumbani. Fr. ngirwa A. New York.

Anonymous said...

Da chemi aksante. Ni haki kucondemn hawa waangalizi nawauguzi. Kugoma kwao si haki kwa maisha ya binadamu wagonjwa na pia si ethical kwa kazi yao. Hapa tunawatetea tu kuwa hawawajibiki kwa hili wa kuwa walikuwa mgomoni lakini si sawa. Je wafu na majeruhi wangekuwa ni ngugu zako wadhani ungesema positively juu ya mgomo wao?... watafute njia nzuri za kuwasilisha madeni yao au hata wawagomee kuwatibu hao hao wakubwa na si kuhatarisha maisha ya watanzania wanaowaamini katika afya zao.
Stupid