Showing posts with label Kinondoni Cemetery. Show all posts
Showing posts with label Kinondoni Cemetery. Show all posts

Saturday, July 02, 2016

Kumbukumbu - Steven Kanumba (1984 -2012)

Kaka Selles Mapunda akisafisha kaburi la rafiki yake, marehemu msanii Steven Kanumba, huko katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Kusoma Historia ya Marehemu Steven Kanumba BOFYA HAPA:

Marehemu Steven Kanumba (1984 -2012)

Saturday, May 17, 2014

Private Brian Salvatory Rweyemamu Azikwa Leo Mjini Dar es Salaam

 Private Brian Salvatory Rweyemamu -JWTZ  (1987-2014) amezikwa leo mjini Dar es Salaam katika makaburi ya Kinondoni. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.

The Late  Private Brian Rweyemamu 1987-2014


Picha kwa hisani ya Ikulu:





Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Bw. Salva Rweyemamu na mkewe Isabella wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wao Private Brian Salva Rweyemamu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2014




Dada wa Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu wakiweka shada la maua wakati wa mazishi katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2014



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salva Kikwete wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Private Brian Salva Rweyemamuwakati wa mazishi  katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2014

Tuesday, April 10, 2012

Mliozika Ndugu Kinondoni Mkacheki Hali ya Kaburi Zao!!!

Wadau, nilijua itatokea!  Makaburi mengi huko katika makaburi ya Kinondoni yameharibiwa leo na umati walioenda kuhudhuria mazishi ya marehemu Bongo Superstar Steven Kanumba.  Kweli watu hawana heshima kwa wafu! 



Pole sana Profesa Msuya!




KUONA PICHA ZAIDI ZA UHARIBIFU KATIKA MAKABURI YA KINONDONI  NA MAZISHI YA STEVEN KANUMBA BOFYA HAPA:

Wednesday, September 12, 2007

Wizi hata kwenye Mazishi

Jamani, sijui ni njaa au nini inafanya watu wawe na roho ngumu hivyo! Watu wanaiba kwenye mazishi. Lakini nishangae nini, maana hata mfiwa mume wa marehemu Amina Chifupa aliibiwa simu kwenye mazishi ya mke wake!

Someni habari hizi kutoka ippmedia.com

***************************************************************
Aliyejaribu kuiba msibani Dar nusra auawe
2007-09-12

Na Job Ndomba, Mikocheni

Kijana mmoja aliyejaribu kuiba mali wakati wa maombolezo ya msiba amekiona chamoto baada ya waombolezaji kumpa kisago kikali kabla ya Polisi kumuokoa. Mtu huyo amenusurika kupata madhara zaidi baada ya waombolezaji wenye hasira kutaka kuendelea kumpa kichapo zaidi baada ya kumnasa akiwa kwenye harakati za kunyofoa vifaa vya gari moja la waombolezaji hao na kuondoka navyo.

Tukio hilo linadaiwa kutokea jana, mishale ya saa 9:30 na saa 10:00 jioni pale kwenye makaburi ya Kinondoni. Inaelezwa kuwa wakati huo, waombolezaji walikuwa wakiendelea na shughuli za kuuzika mwili wa mpendwa wao.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, ni kwamba kibaka huyo akiwa na wenzake wawili, walitinga makaburini hapo wakati waombolozeji hao wakiwa `bize` na shughuli za mazishi.

Akizungumza na Alasiri mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Bw. Peter, amesema watu hao walitinga eneo hilo wakiwa katika taxi yenye namba T 500 AEF. Msimuliaji huyo amesema wakati shughuli za maombezi zikiendelea, wakasikika watu waliokuwa wakiitilia wezi karibu yao.

Akasema muda si mrefu wakawaona vibaka hao waliokuwa wakinyofoa vifaa kadhaa toka katika shangingi la mmoja wa waombolezaji wakaanza kutimua mbio na hapo baadhi ya watu hawakukubali na kuanza kuwatimua.

``Walikuwa zaidi ya wawili? kwa bahati, mmoja akakamtawa na ndipo watu walipoanza kumpa kipigo,`` akasema msimuliaji huyo.

Aidha, ikasimuliwa kuwa muda si mrefu Polisi wakafika eneo hilo na kumuokoa kibaka aliyenaswa ambaye pengine, kama angeendelea kupigwa angeweza kuuawa kwa mawe.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa tayari kibaka huyo alishakuwa taabani kutokana na kipigo alichopewa. Inaelezwa zaidi kuwa baadaye, lilifika `breakdown` na kuivuta teksi waliyokuwa nayo vibaka hao.

Alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Jamal Rwambow, amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo.

SOURCE: Alasiri

Monday, August 06, 2007

Makaburi ya Kinondoni


Makaburi ya Kinondoni yamejaa lakini naona watu bado wanazikwa huko. Je, wanazikwa juu ya wengine? Au wanatupa mifupa ya watu nje kusudi mwingine apewe nafasi? (Nilishuhudia tukio kama hiyo Tabora). Na pia nilisikia eti kuna watu ambao wamenunua viwanja vya kuzika huko kwa ajili ya familia zao. Makubwa maana Kinondoni si makaburi ya umma (public)! Na kuna watu walisema siku hizi Kinondoni wanazikwa watu wazito na wenye uwezo tu, maskini haingii. Duh! Jamani wote si wamekufa, kuna mtu anondoka na hela yake dunia hii?
Nakumbuka miaka ya 80 walifungua Kinondoni Cemetery part II na penyewe sasa pamejaa!
Lakini pamoja na makaburi ya Kinondoni kujaa naona watu bado wanataka ndugu zao wazikwe huko. Mwisho itakuwa kama yale makuburi ya Kinshasa ambako kuzikwa huko mpaka kutoa donge nono!
Na baada ya kuulizia ziaidi niliambiwa hata makaburi ya Sinza, Magomeni na Temeke yamejaa lakini watu bado wanazika tu! Wanasema hata wakichimba na kukuta mifupa wanaendelea kuchimba. Itabidi halmashauri ya jiji watenge sehemu zingine kwa ajili ya kuzika.
Sasa tukikosa sehemu za kuzika itabidi maiti zichomwe moto kama wanavyofanya wahindi (cremation).