Showing posts with label Steven Kanumba. Show all posts
Showing posts with label Steven Kanumba. Show all posts

Saturday, March 27, 2021

Concussion Awareness - Habari Zaidi - Ubongo ukiumia




Wangapi mmeanguka na kupoteza fahamu kwa muda?  Au baada ya kuanguka unajiona unazimia zimia

Ni kutokana na kitu kinaitwa Concusssion. Yaani ubongo  unapata shot vile.  Mara nyingi wana michezo waanaathirika, na wanaopata ajali wanaathirika.

Mnaweza kusoma kuhusu Concussion  KWA KUBOFYA HAPA:

Snowboarding Concussion (Everything You Need to Know) (snowboardhow.com)



Kumbuka msanii Steven Kanumba alikufa kwa Concussion baada ya kuanguka na kugonga kichwa nyumbani kwake.  Mnaweza kusoma kuhusu kifo cha Kanumba  KWA KUBOFYA HAPA:

http://swahilitime.blogspot.com/2012/04/kanumba-alikufa-kwa-brain-concussion.html


Saturday, July 02, 2016

Kumbukumbu - Steven Kanumba (1984 -2012)

Kaka Selles Mapunda akisafisha kaburi la rafiki yake, marehemu msanii Steven Kanumba, huko katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Kusoma Historia ya Marehemu Steven Kanumba BOFYA HAPA:

Marehemu Steven Kanumba (1984 -2012)

Sunday, April 07, 2013

Ni Mwaka Moja Tangu Steven Kanumba Aage Dunia!

 
The late Steven Charles Kanumba (1984-2012


Leo ni Mwaka moja tangu Steven Kanumba afariki dunia baada ya kuumia katika ugomvi na mpenzi wake msanii, Lulu. Lulu yuko nje kwa dhamana sasa lakini kesi yake ya mauaji unaendelea. Leo Lulu na Mama yake mzazi walitembelea kaburi la marehemu Kanumba. Kutokana na picha nilizoona inaelekea kulikuwa na sinema ya bure huko:

Lulu akiweka Shada la Maua kwenye kaburi la Steven Kanumba huko Kinondoni Cemetery



Kuona picha zaidi tembelea Paradise Entertainment & Promotion:

http://nellykivuyo.blogspot.com/2013/04/picha-za-matukio-lulu-atembelea-kaburi.html

Tuesday, January 29, 2013

Hatimaye Lulu Apata Dhamana

Mcheza sinema, Elizabeth Michael, aka. Lulu amepata dhamana leo. Lulu alikaa rumande siku 274 kwa tuhumu za kumwua mpenzi wake, mcheza sinema maarufu, Steven Kanumba.



 Picha hizi zimetoka Millardayo.com

Lulu akilia machozi ya furaha baada ya kuaachiwa huru kwa dhamana

Lulu na mama yake mzazi wakilia baada ya kukutana nje ya Mahakama, Lulu amechiwa huru na Mahakama leo january 29 2013 mchana, pembeni ni mwigizaji Dr. Cheni ambae amekua karibu na familia ya Lulu kwa muda mrefu sana.


Taarifa ya habari ya saa saba machana ( Jumatatu 28/1/13)  kupitia TBC imesema:


Msanii wa filamu Elizabeth Michel, maaruf kama Lulu, anayekabiliwa na shitaka la tuhuma za mauaji ya aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba, leo amepewa dhamana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam.

Masharti ya dhamana hiyo ni pamoja na:

- Kuwa na wadhamini wawili kwa dhamana ya Shilingi milioni 20 kila mmoja

- Kukabidhi pasi yake ya kusafiria kwa Msajili wa Mahakama

- Kuripoti Mahakamani kila tarehe Mosi ya kila mwezi.

- Marufuku kusafiri nje ya nchi.

Taarifa kwa kina kama ilivyowandikwa na Happiness Katabazi Happiness Katabazi

HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imempatia masharti matano ya kupata dhamana kwa msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael ‘Lulu’, anayekabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.

Masharti hayo yaliyolewa jana na Jaji Zainabu Mruke muda mfupi baada ya mawakili wa Lulu, Peter Kibatara, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe kuiomba mahakama hiyo impatie dhamana mshtakiwa huyo ambaye anasota rumande tangu April mwaka jana ambapo walieleza kuwa ombi la dhamana wameliwasilisha chini ya kifungu cha 148(1) ,(2) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 .

Jaji Mruke alisema ili mahakama impatie dhamana ni lazima asalimishe kwa Msajili wa mahakama hiyo hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya mahakama, kuripoti kwa msajili kila mwezi, kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali ambao watasaini bondi ya Sh. milioni 20 kila mmoja.

Baada ya jaji huyo kutangaza masharti hayo Lulu na wakili wake walitoka nje ya ukumbi uliokuwa ukiendeshwa kwa shauri hilo kwa ajili ya kwenda kwa msajili kutimiza masharti hayo lakini kwa bahati mbaya Msajili hakuwepo ofisini na hivyo kufanya Lulu kurudishwa rumande hadi leo atakapoletwa kwa ajili ya kujatimiza masharti hayo mbele ya Msajili wa mahakama hiyo.

Kufuatia mahakama hiyo kumpatia masharti ya dhamana Lulu kutoka na ombi lake Na.125/2012 la kuomba mahakama hiyo impatie dhamana, bado kesi ya msingi inayomkabili Lulu ambayo ni ya kuua bila kukusudia haijapangiwa jaji wala tarehe ya kuanza kusikilizwa.

Desemba 21 mwaka jana, Hakimu Mkazi Christine Mbando wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu aliifunga kesi ya kuua bila kukusudia Lulu na kuiamishia rasmi kesi hiyo katika Mahakama Kuu, na uamuzi huo wa mahakama ulitokana na upande wa Jamhuri kumsomea maelezo ya kesi yake kwa kina mshtakiwa huyo na kuieleza mahakama kuwa wanakusudia kuleta jumla ya mashahidi tisa.

Monday, January 07, 2013

Tanzania Yapoteza Wasanii wengi katika Kipindi Kifupi

Katika kipindi kifupi tuepoteza wasanii wengi, wengine vijana wengine wazee.  Mungu apumzishe roho zao mahala pema mbinguni. Amen.

Juma Salum Kilowoko a.k.a Sajuki (1986-2013)

John Stephano Maganga  (1988- 2012)

Hussein Ramadhani Mkieti  aka.Sharo Milonea (1985 -2012)
Steven Kanumba  (1984 -2012)

 Fundi Saidi aka. Mzee Kipara (192? -2012)

Rose Thomas (1980 -2012)

Saturday, July 28, 2012

Mama Kanumba Alazwa!!

Ugua pole Mama Kanumba!
 




 KUTOKA GLOBAL PUBLISHERS:

Na Shakoor Jongo
MAMA mzazi wa marehemu Steven Charles Kanumba, Flora Mtegoa juzi alilazwa katika Zahanati ya Kilimani, Manzese jijini Dar kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu pamoja na Malaria.
Chanzo chetu kilichopo hospitalini hapo kilisema kuwa, mama huyo alifikishwa katika zahanati hiyo usiku wa Julai 9, mwaka huu huku akiwa hoi.
“Mama Kanumba hakutaka kwenda kwenye hospitali nyingine yoyote zaidi ya kwenda kwa daktari aliyekuwa akimtibia mwanaye maarufu kwa jina la Kidume ambaye anafanya kazi katika zahanati ya Kilimani,” kiliendelea kusema chanzo hicho.
Baada ya kupata taarifa hizo, paparazi wetu alitinga katika zahanati hiyo ili kuhakikisha kama kweli mama huyo alikuwa amelazwa, alipofika nje aliliona gari la marehemu Kanumba na alipoingia ndani alimuona mama huyo.
Hata hivyo, jitahada za kupata picha yake akiwa kitandani zilishindikana kutokana na mazingira kutoruhusu.
Aidha, Ijumaa liliongea na mdogo wa marehemu Kanumba, Seth Bosco ambaye alikiri mama yake kulazwa katika zahanati hiyo.
“Ni kweli mama amelazwa na anasumbuliwa na malaria pamoja na presha, anaendelea kupata matibabu,” alisema Seth.Chanzo:www.globalpublishers.info ************************* MAMA KANUMBA AMVAA MAMA LULU!!! Na Hamida Hassan na Gladness Mallya CHOKOCHOKO zimeanza! Huku kesi ya kifo cha mwanaye ikiendelea na Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ akisota nyuma ya nondo za mahabusu ya Segerea, mama mzazi wa marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’, Flora Mtegoa amemvaa mama Lulu, Lucresia Karugila, Ijumaa linafunguka. MANENO MAZITO YA AIBU Kwenye mahojiano maalum na gazeti hili nyumbani kwake Kimara-Temboni, Dar es Salaam, mapema Jumanne wiki hii, mama Kanumba alimtolea mama Lulu maneno mazito huku akimshangaa kwa kushindwa kumpa pole na kumfariji tangu mwanaye afikwe na umauti Aprili 7, mwaka huu. Mama Kanumba alisema anaongea kwa uchungu kwani hakutegemea kama mama Lulu anaweza kuwa kimya mpaka leo hii bila hata kumpa pole wakati matatizo yamewakuta watoto wao wote. TUPATE SAUTI YA MAMA KANUMBA Ijumaa: Ili kupata kile alichokisema mzazi huyo mbele ya gazeti hili, tujiunge naye akiwa nyumbani kwake Kimara-Temboni. Kwako mama Kanumba: Namshangaa sana mama Lulu kwani namuona kama siyo mzazi mwenzangu. Huwezi amini mpaka leo hii hajawahi hata kunipa pole wala kunitumia ujumbe wa watu kunifariji, hivi anategemea mimi nimfuate? Yeye mwanaye yupo hai wangu ndiyo ametangulia. Nimeona niseme kabisa nimpe habari yake. Ijumaa: Kwani wewe uliwahi kufanya jitihada za kukutana na kufarijiana naye akakataa? Mama Kanumba: Mama Lulu siyo kabisa. Aliwahi kufuatwa na kuombwa ushirikiano wakati kesi imefunguliwa akakataa. Ijumaa: Mbona kuna madai kuwa baada ya kifo cha Kanumba upande wa Lulu ulikufuata ukakataa kutoa ushirikiano? Mama Kanumba: Sijawahi kuongea na mtu yeyote wa upande wa Lulu. Huyo anayedai alikuja kuniomba ushirikiano nikamfukuza ananisingizia kwani simfahamu Lulu na mama yake zaidi ya kuwaona kwenye vyombo vya habari na filamu (Lulu). Ijumaa: Je, akikufuata utamkubalia aje kukufariji? Mama Kanumba: Mimi sina nia mbaya na mama Lulu, kibinadamu namuona kakosea kwani kama yeye alikuwa akiogopa, angetuma watu waje kwa niaba yake. Nilidhani alikuwa akiogopa kuja Sinza (Vatican kwa Kanumba) kwa sababu ya waandishi lakini hata nilipohamia huku (Temboni) hajaja. Ukweli ni kwamba akija nitampokea tu ila sidhani kama ipo siku atakuja, nawashangaa hata washauri wake. Ijumaa: Unaizungumziaje filamu ya Foolish Age ya Lulu ambayo Kanumba aliipeleka Steps? Mama Kanumba: Ni kweli filamu hiyo ipo Steps, Kanumba ndiye aliipeleka kwa nia ya kumuinua Lulu lakini kabla haijalipwa mauti yakamkuta. Ingekuwa ya Kanumba ningefuatilia. Baada ya mahojiano hayo, Ijumaa lilitafuta mzani upande wa pili wa mama Lulu ambapo mahojiano yalikuwa hivi: TUJIUNGE NA MAMA LULU AKIWA TABATA Ijumaa: Mama Lulu gazeti la Ijumaa limezungumza na mama Kanumba anakulaumu kwa kushindwa kumfariji baada ya kifo cha mwanaye Kanumba aliyekutwa na umauti akiwa na Lulu. Je, unalizungumziaje suala hili? Mama Lulu: Eehee unasemaje? Wewe ni nani? Mwandishi? Nimeshawaambia mniache kabisa kwani bila habari ya Lulu na Kanumba hamuuzi? Ijumaa: Katika maadili ya kazi yetu mtu mmoja akiongea lolote juu ya mwenzake lazima pande zote zisikilizwe hivyo hii ndiyo nafasi yako. Unalizungumziaje suala hilo la mama Kanumba? Mama Lulu: Sitaki kushauriwa na wewe mwandishi, nina washauri wazuri tu tena ni watu wazima, tafadhali naomba mniache nipumzike. KIFUATACHO Bado kesi ya Lulu ni mbichi ambapo itaendelea kuunguruma baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kumaliza utata wa umri na jina la Lulu Julai 23, mwaka huu. KALAMU YA IJUMAA Wazazi hawa wanapaswa kuwa na staha kwa sababu kila upande una machungu. Kanumba hatunaye na Lulu yupo nyuma ya nondo. Ni vyema wakakaa chini bila kukorogana ili kupunguza machungu waliyonayo.Chanzo:www.globalpublishers.info

Wednesday, June 13, 2012

Mahakama Waendelea Kujadili Umri wa Lulu!

Wadau, Cheti cha Kuzaliwa Kinatosha kuthibiti umri wa mtu. Ila katika kesi hii, Lulu alikwishafanya party ya kutimiza 18, na pia alikuwa anawaambia wanahabari katika mahojiano kuwa yeye ni 18. Ndo matokeo ya kutaka kuwa mkubwa kabla ya siku zako!  Ukubwa amepata!

******************************************************


Elizabeth Michael Kimemeta aka. Lulu ana miaka mingapi? 17 au 18?
 Kutoka The Citizen

Court orders Lulu’s lawyers to Provide proof on her Age


Monday, 11 June 2012
By Rosina John

The Citizen Correspondent

Dar es Salaam. The High Court in Dar es Salaam yesterday ordered defence lawyers of movie actress Elizabeth Michael alias Lulu to present documents supporting their claim she is under the age of 18.Judge Fauz Twaibu ordered the defence lawyers to present the evidence and supporting documents by way of affidavit on June 13.

Lulu is charged at the Kisutu Resident Magistrate’s Court with murdering local movie star Steven Kanumba on April 7, this year, at Sinza Vatican.

Defence counsel led by advocate Peter Kibatala filed the application at the High Court seeking the determination of the accused’s age. The lawyers stated that Lulu has not attained the age of 18 years to merit prosecution in an adult court.

The application by Mr Kibatara followed a decision by the lower court to turn down their request to transfer the murder case to a juvenile court on the ground that the lower court lacked jurisdiction to entertain the matter. However, in his ruling yesterday, Judge Twaib quashed and set aside the decision by the resident magistrate’s court to refuse to entertain the application, saying it was an error in law and an abdication of duty.

“Consequently, I hold that the lower court was wrong to refuse to entertain the application, thinking that such an enquiry could only be done by this court.

I quash and set aside the decision of the Kisutu Court,” the judge ruled.

The judge said that, considering the seriousness of the charge facing the applicant and the urgency of determining whether or not the applicant is entitled to the benefits of the Child Act and in the interest of justice, the court is invoking its supervisory powers under Section 44 of the Magistrate’s Court Act and shall proceed to determine the correct age of the applicant in terms of Section 113 of the Child Act.

The judge said that the nature and seriousness of the charge facing the applicant, the lack of any possibility for securing bail, during the pendency of the charge and undisputed urgency of the matter require that the controversy about her age be determined the soonest.

He further ruled that, in the meantime, the proceedings of the murder case at the lower court should stay, pending determination of the applicant’s age in the High Court. The judge ordered the applicant’s counsel to produce evidence on their client’s age on June 13 while prosecution required submitting their reply on June 20 while the hearing would be on June 25.

Wednesday, June 06, 2012

Hivi Lulu Ana Miaka Mingapi?

Wadau,  jumatatu ijayo mahakama itasikiliza kesi kujadili umri wa Lulu Michael Kimemeta.  Lulu anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumwua Bongo Superstar, Steven Kanumba.

Hayo ndio matokeo ya kutaka kukua haraka. Mwaka jana Lulu alifanyiwa Birthday Party kubwa ya kusherekea Birthday yake ya 18. Mwenyewe Lulu katika mahojiano na waandihi wa habari kasema ana miaka 18. Kakbiliwa na shitaka la kuua na sasa ana miaka  16 mara 17! Duh!  Msipende kukua haraka wadau!

********************************************


Elizabeth 'Lulu' Michael Kimemeta
 Court ruling on Lulu’s age set for early June


Monday, 28 May 2012

By Rosina John

The Citizen Correspondent

Dar es Salaam. The High Court will on June 11 rule on an application by lawyers of actress Elizabeth Michael alias Lulu seeking a court order to determine her age.

Judge Faud Twaib will give the ruling after both parties concluded their submissions yesterday whereby the prosecution asked the court to dismiss the application because it was filed contrary to the law.

Lulu is charged at Kisutu Resident Magistrate’s Court with murdering local movie star Steven Kanumba on April 7, this year, at Sinza Vatican.

Advocate Peter Kibatara filed the application at the High Court seeking an order to the lower court to determine the age of the accused.Mr Kibatara is requesting for the court to transfer the murder case to juvenile court because the suspect is underage.

According to the lawyers, the accused has not attained the age of 18 years to merit prosecution in the adult court.

However, the lower court said it has no jurisdiction to entertain any application because the charge before it involves murder.

In the application, advocate Kibatala said the lower court has power to investigate the age of the accused according to section 113 of the Child Act.

“But the High Court, seeing that the lower court cannot make an investigation, should do so to satisfy itself that the accused is a child,” said Kibatala.

For their part, prosecution led by State Attorney Shadrack Kimaro asked the court to dismiss the application for lack of merit.Kimaro said that the law cited by the defence counsel in the application does not give authority to High Court to give the order.

According to Kimaro, the defence is required to appeal or seek review on the lower court’s decision instead of filing the application.But if they decided to file the application they should cite a section of the law that gives the High Court authority to give the order.

Tuesday, June 05, 2012

Lulu Mahakamani Jana!

Lulu mahakamani Kisutu jana:


Lulu akisindikizwa na Askari magereza

Kutoka The Citizen:


Lulu Case Adjourned to June 18
Monday, 04 June 2012 22:17
By Rosina John
The Citizen Correspondent
Dar es Salaam. The Kisutu Resident Magistrate’s Court adjourned a murder case facing local film actress Elizabeth Michael alias Lulu to June 18, this year.Lulu is charged with murdering local movie star Steven Kanumba on April 7, this year, at Sinza Vatican.

The case was yesterday brought before Resident Magistrate Augustina Mmbando for mention, with the prosecution informing the court that investigations were still going on.“The case is before the court today for mention because the investigations are not complete,” said State Attorney Peter Sekwao.

Sekwao asked the court to set another date for mentioning the case and magistrate Mmbado adjourned it to June 18, this year.While the case continues at the Kisutu Court, the High Court will on June 11 this year rule on an application by the accused seeking the court’s order to determine her age.Advocate Peter Kibatala filed the application after a lower court turned down their request to transfer the case to a juvenile court.

According to the lawyers for the accused, she has not attained the age of 18 years to merit prosecution in an adults’ court. However, the lower court said that it lacked jurisdiction to entertain any application because the charge before it involved murder.

But in his application Mr Kibatala stated that the lower court has power to investigate the age of the accused according to section 113 of the Child Act.The advocate wants the court to take consideration of her age to maintain Lulu’s basic rights as a child, according to section 4(2) of the Child Act.

***********************************************************

Global Publishers wanasema Mimba ya Lulu Imetoka!
 

Kutoka Global Publishers:
 
Na Shakoor Jongo
ULE ujauzito wa miezi mitatu wa mwigizaji nyota wa sinema Bongo ambaye kwa sasa yuko nyuma ya nondo za Gereza la Segerea, Dar es Salaam kwa kesi ya kifo cha Steven Kanumba, Elizabeth Michael 'Lulu' umedaiwa kuchoropoka, Ijumaa Wikienda lina cha kushika mkononi.
CHANZO CHAFUNGUKA
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika ambacho ni makini, sababu kubwa ya mimba hiyo kutoka ni kutunga nje ya mfuko wa uzazi hali ambayo ingemletea matatizo Lulu.
“Nikwambie kitu, unajua wengi wanaamini Lulu ana mimba na hivi karibuini iliandikwa imefikisha miezi mitatu, ilikuwa sahihi, lakini ukweli ni kwamba kwa sasa imetoka.
“Sababu kubwa ni kwamba afya yake ilidorora, ukiachia ule ugonjwa wa U.T.I alioripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba anao, lakini kingine ni kuwa iligundulika ujazuito wake ulitunga nje ya mfuko wa uzazi ikawa haina jinsi, ikabidi kutolewa na kusafishwa,” kilisema chanzo hicho bila kuainisha tukio hilo lilitokea lini.
ETI NI MIMBA YA TATU
Kikiendelea kuzungumza kwa umakini mkubwa, chanzo chetu kilidai kuwa eti ujauzito huo ni wa tatu kuchoropoka kwa msanii huyo.
“Unajua huu unakuwa ujauzito wa tatu kwa Lulu kutoka. Kwa kweli kama si hivyo angekuwa na mtoto,” kilisema chanzo bila kuweka wazi nyingine mbili zilitoka kwa matatizo gani.
“Kuna wakati Lulu alikwenda China, aliporudi alikuwa na ujauzito, lakini nao ulitoka, inaonekana ana matatizo kidogo kwenye upande wa kizazi,” kilidai chanzo hicho.
Kikaendelea: “Baada ya hapo, haukupita muda mrefu, akanasa nyingine ya mwanamuziki mmoja wa Bongo Fleva, pia hiyo nayo ikaja kutoka ya tatu ni hii ya Kanumba.”
MAMA LULU
Katika kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa Wikienda lilimsaka mama Lulu, Lucresia Karugila ili kusikia kutoka kwake lakini hakupatikana hewani kutokana na kuzima simu.
USHUSHUSHU GEREZANI
Ijumaa Wikienda lilituma ‘mpelelezi’ wake kwenye Gereza la Segerea ili kukutana na Lulu na kuzungumza naye kuhusu madai ya mimba yake kuchoropoka.
Ilikuwa kazi kubwa kumpata ‘laivu’ nyota huyo kutokana na ukweli kwamba kuna watu maalum watatu ambao ndiyo wenye ruhusa ya kumwona mtuhumiwa huyo, mbali na hao marufuku kwa wengine.
Hata hivyo, ‘shushushu’ huyo alifanikiwa kupata fursa ya kumjulia hali mahabusu mwingine aliyepo kwenye gereza hilo na ndipo akapata bahati ya kuonana na Lulu ambaye alionekana kuwa mnyonge.
Baada ya salamu, shushushu wetu alimuuliza Lulu kuhusu afya yake na ya ujauzito alionao ambapo alijibu kwa mkato.
“Nani amekwambia mimi nina mimba?”
MASTAA WA BONGO WANENA
Baadhi ya mastaa wa sinema Bongo ambao hawakuwa tayari majina yao kuchorwa gazetini, walipozungumza na gazeti hili kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa ujauzito wa Lulu walipishana ‘kiswahili’.
Wapo waliodai ujauzito huo ulitoka akiwa gerezani, wengine walidai ulitoka wiki moja kabla ya kifo cha Kanumba lakini wapo waliodai bado anao.
Staa wa kiume: “Lulu hana ujauzito, ulitoka. Ninavyojua mimi, wiki moja kabla ya kifo cha marehemu (Kanumba) ndiyo ulitoka, kwa hiyo hana.”
Staa wa kike: “Lulu bado ana mimba ila ni siri sana. Lakini hata nyiye wenyewe si mmeona tumbo lile, anao.”
Staa wa kike: Lulu mpaka anaingia kwenye matatizo kwa kifo cha Kanumba alikuwa na kibendi, hawezi kukitoa kwa sasa, maana yuko gerezani.”
Lulu anatarajiwa kufikishwa Mahakama Kuu ya Tanzania Mei 28, mwaka huu ili kujibu tuhuma zinazomkabili juu ya kifo cha Kanumba.
Lulu ana Mimba? Is Lulu Pregnant

Former Tanzanian film star Steven Kanumba's girlfriend Lulu Michaels is rumoured to be pregnant. Lulu who was charged with his murder is now three months pregnant. According to Tanzanian tabloids, Lulu, 17, is reportedly carrying the late actor's baby. She has however not commented on the pregnancy. Lulu is rumoured to have  previously dated Tanzanian Ali Kiba. They remained friends after they broke up. Kanumba’s  sudden death devastated his fans from both within and outside the country.
According to the police, Kanumba and Lulu were fighting over calls that were coming on her phone while she was at his home. He demanded to see the calls and the girl wasn't ready to surrender it. While he was taking it by force, she pushed him and he fell, hitting his head hard. She is still in police custody as the investigations are still underway.

Monday, April 23, 2012

Lulu Mahakamani Kisutu Leo

 Mcheza sinema Elizabeth 'Lulu' Michael alifikishwa katika mahakama leo kuhusiana na kesi yake kuhusiana na mauji ya Bongo Star Steven Kanumba.  Kesi leo ilikuwa ni kutajwa tu yaani Mention.
Mcheza Sinema, Elizbeth 'Lulu' Michael, katika Mahakama ya Kisutu leo hii 23/4/12 (Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)  Kuona picha zaidi Mtembelee Kaka Michuzi


Katika hii picha ya Global Publishers Lulu anaonekana kuwa na kakitambi!   (picha kwa hisani ya Global Publishers)

MAELEZO KUTOKA GLOBAL PUBLISHERS

Mwigizaji Maarufu wa filamu za Kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo majira ya saa nne asubuhi amepandishwa kizimbani kwa mara ya pili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shitaka la kumuua Steven Kanumba. Baada ya kusomewa shitaka hilo na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama hiyo Elizabeth Kaganda mbele ya Hakimu Rita Tarimo hakutakiwa kujibu lolote. Mwendesha Mashitaka huyo alisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamailika hivyo kesi hiyo iliahirishwa mpaka Mei 7 mwaka huu.


Friday, April 13, 2012

Baraza la Habari Tanzania Yaja Juu! - Kifo Cha Steven Kanumba

Baraza la Habari Tanzania: Acheni Mahakama Ifanye Kazi Yake Juu Ya Kifo Cha Steven Kanumba

Kutoka kulia ni Katibu wa MCT Kajubi Mukajanga katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Baraza la Habari MCT Jaji Thomas B. Mihayo, na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili pia Mjumbe wa Bodi Rose Haji.
(Picha na Blasio Kachuchu)





KAMATI ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) leo mchana imetangaza imesikitishwa na ukiukwaji mkubwa wa maadili uliojitokeza hivi karibuni kwa baadhi ya vyombo vya Habari ambavyo wakati vikiripoti kuhusu kifo cha Msanii Steven Charles Kanumba, vimemhukumu msichana Elizabeth Michael Kimemeta maarufu kama Lulu, kuwa amemuua msanii huyo.

Ukiukwaji huo umejitokeza hasa baada ya msichana huyo kufikishwa Mahakamani, ambapo baadhi ya magazeti yanayoheshimika katika jamii jana Alhamisi, Aprili 12, 2012 yaliandika vichwa vikubwa vilivyosomeka: Lulu Kortini kwa kumuua Kanumba na Lulu Kizimbani kwa mauaji ya Kanumba.

Kwa mujibu wa sheria na maadili ya Uandishi wa Habari mtu yeyote anayekamatwa kwa tuhuma yoyote ile ni mtuhumiwa mpaka atiwe hatiani na mahakama.

Kanuni hii ya siku nyingi katika fani ya uandishi wa habari inafahamika na waandishi na wahariri wote wanaoheshimu kazi yao.

Baraza pia limeshatoa matamko mara kadhaa kuwakumbusha wanahabari kujiepusha na uandishi wa habari au vichwa vya habari vinavyohukumu.

Baraza linafahamu fika kuwa kesi zilizoko Mahakamani ni kivutio kwa umaa kutaka kujua kinachoendelea ili kuona haki ikitendeka na pia wanahabari wana haki ya kujua na kuripoti yanayojiri huko na katika vyombo vingine vya sheria.

Lakini lazima ifahamike kuwa wakati wakitumia fursa na haki hiyo Wanahabari wanapaswa kuzingatia kanuni, miongozo na sheria zinazolinda haki za msingi zxa watuhumiwa na uhuru wa Mahakama.

Ni wazi kuwa vichwa vya habari vilivyoitajwa hapo juu vimeliingilia uhuru wa Mahakama kwa kuchapisha habari ambazo zinaonekana kushawishi au kushinikiza uamuzi wa Mahakama.

Wanahabari ni lazima watambue kuwa kuna taratibu na makubaliano ya kijamii juu ya namna gani taarifa zinavyopaswa kuripotiwa ili kutowadhuru watu wengine.

Hivyo basi , Baraza la Habari Tanzania linapenda kuwakumbusha tena wahariri kuhakikisha kuwa wanafanya kazi yao kwa kuzingatia maadili na weledi katika kuripoti mkasa huu unaogusa hisia za watu.

Imesainiwa na


Jaji Thomas B. Mihayo
Mwenyekiti
Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania.

Thursday, April 12, 2012

Baba Lulu Aongea na Waandishi wa Habari

KWA HISANI YA BLOGU YA JAMII:

Mzee Michael Edward Kimemeta (picha na Dixon Busagaga)

Imeandikwa n Dixon Busagaga  - Globu ya Jamii Moshi


Baba mzazi wa Muigizaji wa kike wa filami nchini maarufu kama Lulu, ambaye anahusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba, ameibuka na kueleza kushtushwa sana na taarifa za kifo hicho pamoja na habari kuwa bintiye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo nguli na kuwa anahusika na kifo chake.

 Baba Lulu, ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimemeta(49) mzaliwa wa Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro, kaiambia Globu ya Jamii leo huko Moshi kuwa alimtambua Steven Kanumba kama mwalimu wa mtoto wake Lulu,lakini hakuamini masikio yake baada ya kupata taarifa za kifo hicho, huku bintiye, anayedaiwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu, anahusika.


Lulu alifikishwa mahakamani jana April 11, 2012 akikabiriwa na mashtaka ya mauaji ya Marehemu Steven Kanumba, ikiwa ni siku nne baada ya kifo cha msanii huyo. Alisema kuwa Elizabeth ama Lulu alizaliwa tarehe April 17,1995 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, na kwamba alimaliza elimu ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Midway mwaka jana na kamba hivi sasa ana umri wa miaka 17.

Bw Kimemeta alisema kuwa ni vyema polisi kuwa makini katika uchunguzi wao kwa kuzingatia kuwa tukio hilo limejenga chuki na uhasama baina ya Lulu na ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wa marehemu Steven Kanumba. Alisema kuwa kilichomshtusha zaidi ni taarifa za polisi kusema kuwa kulitokea ugomvi kati ya Marehemu Steve Kanumba na Lulu,huku ikitajwa kuwa walikuwa wapenzi.

“Hatukutegemea kama Marehemu Kanumba angeweza kuwa na mahusiano y kimapenzi na binti yetu; kwanza ndiye tuliyekuwa tukimtegemea kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza na kukikuza kipaji alichokuwa nacho Elizabeth”, alisema baba mtu. “Ninaomba Wanasheria na wanaharakati wa haki za kibinadamu kuingilia suala hili na kusaidia katika kupatikana kwa haki dhidi ya shtaka la mauaji linalomkabili binti yangu Elizabeth na pia naomba swala hili lisichukuliwe kishabiki ama kwa hisia bali haki ichukue mkondo wake”alisema.

Kanumba na Lulu mwaka jana.  Picha kwa hisani ya  Mpeli Jr Ngonywike
 Alisisitiza kuwa jamii inatakiwa kutambua mazingira ya tukio hilo,ambapo chanzo kinasemekana ni ugomvi uliopelekea tafrani kwa Lulu kutuhumiwa kumsukuma Marehemu Kanumba kwa kile kinachodaiwa kuwa ulikuwa wivu wa kimapepenzi na haiyumkini hakukusidua kumuua hivyo yeye anashangaa bintiye kuhusishwa moja kwa moja na mauaji.

“Ushiriki wa mwanangu kuhusu mambo ya sanaa nilikwishapata wasiwasi na mama yake mzazi alikuwa akiwasiliana na Marehemu Kanumba enzi za uihai wake ambaye alikuwa anamhakikishia usalama wa Lulu na kusema kuwa ataendele kubaki kama mwalimu…..lakini leo nasikia alikuwa ni mpenzi - nilishtushwa” alisema Kimemeta.

Baba Lulu pia ameelezea kusikitishwa kwake kwa kushindwa kuhudhuria mazishi marehemu Steven Kanumba kuhofia usalama wake, na kusema mazingira yatakaporuhusu hata sita kufika nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba na kutoa pole. Bw Kimemeta amesema kuwa anaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia ya Marehemu Steven Kanumba na kutoa mkono wa pole kwa msiba huo mkubwa ambao haukutarajiwa.Kasema kuwa Kanumba alikuwa bado ni kijana mdogo aliyeonyesha umahiri kwenye sanaa na kwamba amecha pengo kwa familia yake na Tanzania kwa ujumla.

Lulu na Mama yake Mzazi, Bi Lucrecia Kalugila

Wednesday, April 11, 2012

LULU: That Girl! Kasichana Kale!

Gazeti la Global Publishers

Gazeti la Global Publishers Mwaka Jana

LULU: That Girl! Kasichana Kale!


By Jacqueline Mgumia

Dear TGNP members, young feminists and those in support of our sisters, I think we have a role to play in understanding Lulu's case, its context and her future charges in relation to Kanumba’s death. This portrays a classic relationship between private and public life.

I think it is a platform for expanding and demanding for women’s right issues in our current context - the media space. We should follow up the tragedy to understand what is at stake in relation to women’s rights, images and representations on the media and legal spaces, specifically how domestic spaces make life so vulnerable.

Thus far, Lulu is in rumande, accused, suspected, or associated with Kanumba's death. Unfortunately, public opinion is against Lulu as she is condemned and demonized for her loose sexual conducts, a fact which could easily forge her rights in regard to the accusations or, if found innocent, her security in the public domain will be threatened.

I am not saying she is innocent, but I always wonder why only young superstar women are labeled as loose or malaya! And, yes, if she has been malaya or bad, so what? Is this only bounded/confined to a moral question? Is this about good girls and bad girls? Does this mean she deserves to be accused without being listened too? Does this justify one being declared guilty without a fair trial or being understood?

Some people say YES! Kaache kasote rumande ama kaende jela, maana, asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu! I say NO, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!

This is not a claim for being guiltless, rather it is a call to allow police and medical practices as well as procedures to rule the investigations, not the hyped media opinion of kale kasichana.

Justice is for everyone, those good and bad, those present and absent. If the investigation finds any association or relation of her conducts to be incriminating that will be a different question of the law and lawyers will choose positions.

Human right activists, feminists and the media, how do we associate ourselves with those labeled bad or indeed bad on culture lenses? Do we choose to remain in silence on whose lenses we are trading?

I speak not because she is a woman and young, as that could be doing injustice to our late Kanumba and being biased on a purely gender stance, rather it is to engage with the notion of good and bad girls in the media and its implication on women representation in general, and especially in our digital generation.

Lulu is still in rumande, maybe a quick and quiet visit will help us understand what is happening to her and perhaps make a decision if it is a case we might want to follow. We should start by getting facts right by acknowledging that Lulu is prejudged because of her character, and that can never be right or fair.

This is not about Lulu, it is about Wema, Ray C, Yasinta, and many young women like her in the movie and music industry; the platform is rough and tough, providing different experiences to female artists, of which we know very little about.

We need to start engaging with these spaces, as these young women define the good and bad girls in subtle but very important ways!

This is not about that girl! It is about understanding what is happening in domestic spaces, where both men and women rights could easily be abused in silence. It is about engaging with misunderstood women using our lenses to make sense of their stories and realities so as to inform ourselves on diverse issues facing women. It is about understanding the perceptions and cultures that influence practices and outcomes of laws.

I pray for Kanumba the Great that he may rest in peace and, at this point, I should declare that he was one of the Tanzanian actors that I gave respect to for his achievements; however, his latest movie MOSES, which is centered on hate on women, left me wishing to meet him and chat about impacts of such contents on women. Indeed he has left us very young. He will be greatly missed.

As he rest in peace tomorrow and justice is found for his sudden death, let Lulu - before the law and public - be judged and treated with fairness regardless of being that girl - kasichana kale!

Lulu Mahakamani Kisutu Leo!

Lulu Akijiandaa kuacti Sinema
Hayati Steve Kanumba ni miongoni mwa wasanii maarufu wa Tanzania wenye nyota za umaarufu (Tanzania Walk of Fame) ndani ya ukumbi wa Dar Live jijini Dar Es salaam ambapo mara baada ya kifo chake wafanyakazi wa ukumbi huo na mashabiki wake wameweka mashada ya maua,kadi na kuwasha mishumaa kama ishara ya kuomboleza kifo chake.
 (Picha kw Hisani ya Abdallah Mrisho Blog)
MAELEZO KUTOKA MICHUZI BLOG:

Muigizaji wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie, Marehemu Steven Kanumba,Elizabeth Michael a.k.a Lulu amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana na kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.


Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko sinza vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.

Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.

Muigizaji huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.

********************************************************************

Lulu kortini kwa kumuua Kanumba

Polisi wamficha, wakwepa waandishi
Ajifunika ushungi, avaa kandambili

Msanii wa uigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael Kimemeta (18), maarufu kama Lulu, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba (28).

Tukio la msanii huyo kufikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka lilikuwa kama mchezo wa filamu baada ya polisi kufanya siri na hata kugombana na baadhi ya waandishi wa habari waliotaka kuingia katika chumba cha mahakama kufuatilia kesi hiyo.

Kesi hiyo ilisomwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Augustina Mmbando.

Kabla ya kusomewa mashtaka hayo, hakimu alimtaka Lulu kutojibu chochote kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda, alidai kuwa Aprili 7, mwaka huu katika eneo la Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alimuua Kanumba.

Kwa mujibu wa Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA), Lulu hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Hata hivyo, mara upelelezi utakapokamilika, kesi hiyo itahamishiwa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusikilizwa.

Kaganda alidai upelelezi bado haujakamilika, hivyo akaiomba mahakama kupanga tarehe ya kuitajwa kwa kesi hiyo.

Hakimu Mmbando alisema mshtakiwa atakaa mahabusu hadi Aprili 23, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa.

Wakati mshtakiwa huyo akisomewa hati ya mashtaka alidai mahakamani hapo kwamba, umri wake sio miaka (18) kama ilivyoandikwa kwenye hati ya mashtaka bali ana miaka (17).

Pia wakati mashtaka yanasomwa hali mahakamani hapo ilikuwa shwari, huku watu wengine wakinong’ona bila kuwa na uhakika kuhusu msanii huyo kufikishwa mahakamani kutokana na kutoonekana kwa wanafamilia wake na watu wa karibu.

Mazingira ya Lulu kufikishwa mahakamani hapo yalikuwa kama mchezo wa kuigiza kutokana na jeshi la polisi kufanya kuwa siri kubwa.

Gari aina ya Suzuki Vitara liliingia katika viunga vya mahakama hiyo muda ambao haukufahamika likiwa na makachero wa Jeshi la Polisi wanne, wanawake wawili na wanaume wawili na mshtakiwa.

Lilifuatiwa na gari lingine aina ya Toyota Land Cruiser lililokuwa na askari polisi saba waliovaa sare za jeshi hilo wakiwa na silaha.

Hata hivyo, baada ya muda NIPASHE kupitia chanzo chake ilipata taarifa ya msanii huyo kufikishwa katika viunga vya mahakama hiyo na kwamba jalada la kesi yake lilikuwa limeshapangiwa hakimu.

Hatua hiyo ilisababisha waandishi wa habari za mahakama kujipanga na kuweka lindo katika kila kona ya jengo la mahakama hiyo huku wengine wakiwa kwenye mlango wa kutokea mahabusu, kwenye korido za milango ya kuingia katika ofisi za mahakimu.

Hata hivyo, kundi la waandishi waliokaa katika korido ya ghorofa ya kwanza kuelekea kwenye ofisi za mahakimu, ghafla saa 5:20 asubuhi walifanikiwa kumuona mshtakiwa huyo akiwa katikati ya makachero wanawake wawili na nyuma wanaume wawili akiwa amejifunika ushungi wa rangi ya udhurungi, gauni kubwa maarufu kama ‘dira’ la rangi ya njano na kandambili za rangi nyekundu.

Waandishi hao walikimbilia msafara huo uliokuwa na askari wanne pamoja na mshtakiwa, lakini kabla ya kuingia chumba cha hakimu, askari aliyekuwa ameshika simu ya upepo mkononi aliwazuia waandishi kuingia.

Hali hiyo ilisababisha majibishano ya muda na mwishowe alibadili nia ya kuzuia wanahabari hao kufanya kazi yao.

Mshtakiwa alisomewa mashtaka yake na baadaye alipitishwa njia ya mlango wa nyuma hadi kwenye gari aina ya Suzuki Vitara yenye namba za usajili T848 BNV yenye vioo visivyoonyesha ndani (tinted).

Ingawa gari hilo lilikuwa na namba za kirais, kwenye vioo liliandikwa namba PT 2565, na iliondoka mahakamani hapo kwa kasi kumpeleka mshtakiwa mahabusu ya Segerea kusubiri upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.

Mapema jana saa 3:35 asubuhi, NIPASHE ilizungumza kwa njia ya simu na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Charles Kenyela kuhusu hatima ya kufikishwa mahakamani kwa msanii huyo, mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo:

NIPASHE: Shikamoo afande.

Kamanda Kenyela: Marahaba. Nipigie baadaye niko kwenye kikao.

NIPASHE: Sawa afande. Lakini nilitaka kujua kama Lulu atapelekwa mahakamani leo (jana) na itakuwa mahakama gani Kinondoni au Kisutu?

Kamanda Kenyela: Mmmh! Kwa kweli bado uchunguzi unaendelea. Hivyo, jalada liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP).

NIPASHE: Ahsante afande. Shida yangu ilikuwa hiyo tu endelea na ujenzi wa Taifa.

Kamanda Kenyela: Nashukuru sana mwandishi.

Kanumba alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumamosi Aprili 7, mwaka huu, baada ya kudaiwa kutokea ugomvi kati yake na Lulu.

Maelfu ya watu, wakiwamo mawaziri, wabunge, viongozi wa siasa, vyama vya kiraia, wasanii wenzake na wananchi wa kawaida, walijitokeza katika msiba huo nyumbani kwake, Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam na kwenye shughuli za kumuaga viwanja wa Leaders Club na kuuzika mwili wake katika makaburi ya Kinondoni.

Mazishi hayo yaliongozwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.


CHANZO: NIPASHE

Maelezo ya Lulu - Kifo Cha Steven Kanumba

KUTOKA THE CITIZEN:

Lulu’s Side of the story as Kanumba is Buried



Elizabeth Michael aka Lulu Akistarehe (Picha kwa hisani ya Global Publishers)
 Tuesday, 10 April 2012 
By Mkinga Mkinga

The Citizen Reporter

Dar es Salaam. The prime suspect in the death on Saturday of local film star Steven Kanumba spoke out on the tragedy for the first time just a day before tens of thousands of people gathered for his funeral yesterday.Elizabeth Michael, alias Lulu, broke her silence on Monday—two days after she was arrested. Investigators at Oysterbay police station had to engage a crime psychologist to get her to open up on the events leading up to the death of the star who had just been invited to Hollywood in the United States.

Highly placed police sources told The Citizen in an exclusive interview yesterday that Lulu, girlfriend of the deceased, started narrating what had transpired on the night the 28-year-old died after meeting the psychologist.

“The suspect, who had refused to cooperate with police detectives from the Kinondoni regional police office, has now managed to speak for three hours with the psychologist,” the sources said on condition of anonymity since they are not official spokespersons of the Tanzania Police Force.

The psychologist from the Criminal Investigation Department (CID) headquarters in Dar es Salaam chatted candidly with the suspect for three hours on Monday, a day before Kanumba was buried.

Lulu reportedly told the investigators that Kanumba phoned her on the fateful night asking her to join him for an outing. She went to his home but told him she did not really want to go out and that she preferred to return home.

Kanumba allegedly wanted Lulu to accompany him to a Mashujaa Band show at Vingunguti, and became furious when she refused to accompany him.

According to the sources, the misunderstanding between the two developed into a quarrel, with Kanumba demanding to know what it was that she had left at her home.“According to Lulu, the deceased locked the door to his room,” said the sources. “In a panic, she unlocked the door and fled.”

Lulu is quoted as saying that she managed to escape after he fell and had no idea what transpired after her departure.

The sources said police have also interrogated another suspect, a Bongo Flava musician (name withheld), who gave Lulu a lift when she left Kanumba’s Sinza residence. “I am sorry, brother, I cannot comment on that issue,” he told The Citizen before he hang up.

According to detectives, other suspects have also been lined up for questioning. The sources could not say how long the interrogations would take.

In another development, the sources said heavyweight politicians related to Lulu have been sending her consolation text messages pledging to assist her. “Their involvement with the suspect could complicate our investigations,” said the sources.

Yesterday, this paper reported that Kanumba died of a brain injury caused by a sudden blow to the head.

One of the doctors who examined Kanumba’s body at Muhimbili National Hospital hinted that the actor died on the spot after suffering such severe brain damage that he collapsed and stopped breathing.

His sudden death sent shockwaves across the country, East Africa and West Africa—particularly Ghana and Nigeria—where he had achieved prominence in the continent’s leading film industry, Nollywood. He had returned home from a trip to Ghana just a few days before his death.

President Jakaya Kikwete joined mourners on Sunday, calling the fallen star a brilliant ambassador who sold Tanzania far and wide through the screen.

Maggid Mjengwa Aomba Jamii Imsamehe Lulu - Kifo cha Steven Kanumba



Lulu, alivyokuwa na maskendo (scandals) sijui kama itakuwa rahisi kwa jamii kumsamehe katika jambo la kifo cha Steven Kanumba!

**************************************************************


KUTOKA MAGGID MJENGWA BLOG:
Neno La Leo: Jamii Ya Walo Wema Imsamehe Elizabeth ' Lulu' Michael

Ndugu zangu,

Jana amezikwa Steven Kanumba , kipenzi cha wengi.

Mauti ya Steven Kanumba yanatukumbusha wanadamu ukweli huu; kuwa maisha yetu hapa duniani ni mafupi sana. Hivyo, lililo jema kwetu wanadamu ni kuishi kwa kutenda yalo mema. Kuwatendea mema hata tunaodhani wametukosea, maana, tutawasaidia kujifunza kutenda mema. Na ni mwanadamu gani asiyekosea?

Na moja ya adhabu kubwa mwanadamu unaweza kuipata humu duniani kutoka kwa wanadamu wenzako ni adhabu ya kutengwa na wanadamu wenzako.

Msichana Lulu ameshapata na anaendelea kuipata sasa, adhabu kubwa sana kutoka kwa wanajamii. Adhabu ya kupewa hukumu ya mauaji na kutengwa na wengine. Lulu , ambaye ni mmoja wa waliokuwa karibu na marehemu Kanumba hata katika dakika zake za mwisho maishani, na ambaye alikuwa mpenzi wa Kanumba, hakuweza kushiriki mazishi ya mpenzi wake. Hiyo nayo ni adhabu kubwa kwa Lulu kupewa na wanadamu wenzake.

Yumkini Lulu ana mapungufu yake kama mwanadamu, lakini, kwa sasa hastahili adhabu kali hiyo kutoka kwa wanajamii. Kwa kosa ambalo hakuna aliye na hakika leo kuwa amelitenda. Ndio, Lulu aweza kuwa mwanadamu mwenye mapungufu yake mengine, lakini , hayo yasitufanye wanadamu tuwe na haraka ya kumpa hukumu isiyo ya haki. Na kwenye mienendo ya maisha, ni mwanadamu gani asiye na mapungufu?

Maana, tangu mara ile ilipofahamika, kuwa msichana Elizabeth ‘ Lulu' Michael alikuwepo kwenye mazingira ya kutokea kwa kifo cha Kanumba, basi, jamii, huku ikisaidiwa na vyombo vya habari, haraka ikapata wa kumnyoshea kidole. Na hukumu ya Lulu kutoka kwa wanajamii walo wengi ikawa imetolewa hapo. Kwamba Lulu ndiye muuaji. Kwa sasa, hukumu hiyo haiwezi ikawa ya haki mpaka pale wenye mamlaka ya kututhibitishia hilo watakapofanya hivyo.

Na hata kama ugomvi, uliotokana na wivu wa kimapenzi , wa Lulu na mpenzi wake ulipelekea mauti ya Kanumba, bado maelezo tuliyoyasikia hayamwonyeshi Lulu kuwa na dhamira ya kutaka kutenda maovu anayohukumiwa na wanajamii kuwa kayatenda. Hivyo, naye, kama mwanadamu, anastahili msamaha kutoka kwa wanajamii wengi walo wema.

Katika wakati huu mgumu sana kwa msichana Lulu, vyombo vya habari viwe mbele katika kumsaidia Lulu kama mwanadamu mwenzetu, badala ya kutumia balaa lililomkuta kama mtaji wa kuandika na kutangaza udaku wa kuuzia magazeti na kuvutia watazamaji wa runinga na wasikilizaji wa redio.

Maana, kwa adhamiriae kutumia magumu yanayomkabili msichana Lulu kuvuna, basi, hana atakachokivuna zaidi ya kuvuna dhambi.

Badala yake, media isaidie katika kutufanya wanajamii tujitafakari. Kwa vile, habari za matukio ya mahusiano yasiyo na staha na matendo ya kiuhuni yanayofanywa na baadhi ya wanajamii wakiwemo wasanii, huwa yanashabikiwa na vyombo vya habari badala ya vyombo hivyo kushiriki kukemea na kuelimisha jamii. inasikitisha, kuwa katika wakati huu, vyombo hivyo vya habari vyaweza kabisa kuwa kwenye harakati za kuandaa stori zaidi za ‘ kumning’iniza’ zaidi Lulu ambaye tayari ameshaning’inizwa hadharani.

Ndugu zangu,

Kama wanajamii, na wengine kama wazazi. Lulu anabaki kuwa ni msichana mdogo anayehitaji kusaidiwa katika wakati huu mgumu kwa maisha yake. Yumkini vyombo vya dola vinaweza vimtie au visimtie hatiani. Hivyo, kumwachia huru Lulu.

Lakini, bado hukumu ya jamii ikabaki pale pale. Hukumu ya Lulu kutengwa na jamii. Hiyo ni hukumu mbaya zaidi inayoweza kuchangia hata kuyafupisha maisha ya msichana huyu mdogo. Jamii haina faida na hukumu kama hiyo. Ni heri ikamwacha huru aende akapambane na yanayomkabili mbele yake. Ndio, akapambane na maisha haya magumu ya dunia hii bila kujisikia kutengwa na wanajamii wenzake.

Na naamini, leo kuna wengi kama mimi, wenye kufikiri hili, kuwa jamii ya walo wema imsamehe Elizabeth ‘ Lulu’ Michael.

Na hilo ni Neno La Leo.

http://www.mjengwablog.com/

Maggid Mjengwa
Dar es Salaam.

Tuesday, April 10, 2012

Mliozika Ndugu Kinondoni Mkacheki Hali ya Kaburi Zao!!!

Wadau, nilijua itatokea!  Makaburi mengi huko katika makaburi ya Kinondoni yameharibiwa leo na umati walioenda kuhudhuria mazishi ya marehemu Bongo Superstar Steven Kanumba.  Kweli watu hawana heshima kwa wafu! 



Pole sana Profesa Msuya!




KUONA PICHA ZAIDI ZA UHARIBIFU KATIKA MAKABURI YA KINONDONI  NA MAZISHI YA STEVEN KANUMBA BOFYA HAPA:

Mazishi ya Bongo Superstar Steven Kanumba Mjini Dar!

Wadau, ama kweli Steven Kanumba alikuwa Superstar!  Watu kuzimia, kuanguka vilio, si wanawake, si wanaume kwenye kilioni, kwenye mazishi mpaka inabidi wahudumiwa na Red Cross! Duh!  Inanikumbusha nilivyoona documentary kuhusu kifo cha mcheza sinema maarufu wa Marekani, Rudolf Valentino mwaka 1926. Valentino naye alikufa ghafla akiwa na miaka 31 tu!  Alikuwa anapendwa mno, tena mno. Watu walitoka kila kona kwenye msiba wake na kwenye mazishi na ilibidi polisi waingilie.  Habari niliyosoma leo kuhusu kifo cha marehemu Kanumba imenikumbusha msiba wa Valentino.  Wazungu wanaweza kusema, The similarities are eerie.

REST IN ETERNAL PEACE STEVEN KANUMBA!


Misa ya Kumwombea marehemu Steven Kanumba huko Leaders Club, Dar es Salaam


Picha Zote kwa hisani ya Michuzi Blog. Kuona Picha zaidi za mazishi tembelea MICHUZI BLOG:

Monday, April 09, 2012

Kanumba Alikufa Kwa Brain Concussion!

Duh! Kama kweli alipata concussion ina maana Steven Kanumba, alipigwa na kitu kizito kichwani au alianguka kweli.  Polisi wanasemaje?  Madakatari wanasema ubongo wake ulikuwa umevimba.

KUTOKA WEB MD

What is a concussion?
A concussion is a type of traumatic brain injury that is caused by a blow to the head or body, a fall, or another injury that jars or shakes the brain inside the skull. Although there may be cuts or bruises on the head or face, there may be no other visible signs of a brain injury.4


 
******************************************************************************
KUTOKA  GAZETI LA MWANANCHI:

NI BAADA YA JOPO LA MADAKTARI MUHIMBILI KUMFANYIA UCHUNGUZI, BABA YAKE AZUNGUMZA, WABUNGE WAANGUA KILIO

Florence Majani na Suzzy Butondo

MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza.


Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya saa mbili.

“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain Concussion,” alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) “Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka” alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.

“Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na rangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.”

“Mtu aliyepata mtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.”

Daktari mwingine aliyeshiriki katika uchunguzi huo ambaye pia aliomba jina lake lisitajwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo ulikuwa umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.
Alisema sehemu ya maini na majimaji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo.

Baba mzazi azungumza Baba mzazi wa mwigizaji huyo, Charles Musekwa Kanumba alisema kwamba alipata taarifa za kifo cha mwanawe Jumamosi saa 10:00 alfajiri baada ya kupigiwa simu na dada wa marehemu, Sara Kanumba. “Sara aliniuliza: ‘Una taarifa yoyote kuhusu mwanao Kanumba?’ Nikamjibu kuwa sina taarifa yoyote, ndipo aliponieleza habari za kifo hicho. Aliniambia Kanumba hatupo naye tena amefariki kwa kuanguka, amekorofishana na mpenzi wake.” alisema taarifa hizo zilimsababisha aishiwe nguvu kwa kuwa kilikuwa kifo cha ghafla… “Basi kuanzia hapo, nilianza kupigiwa simu za kupewa pole, ndipo nilipoamini kumbe mwanangu amefariki.”

Akizungumzia kuchelewa kufika msibani, alisema kumetokana na tatizo la mawasiliano. Awali, alikuwa amepanga mtoto wake Kanumba akazikiwe Mwanza kwa babu yake ndiyo maana hakufika mapema msibani. “Nilikuwa nimepanga apitishwe hapa kwangu Shinyanga aagwe, halafu tumpeleke Mwanza kwa babu yake kumzika huko lakini alipokuja mama yake alinishauri kuwa huko kutakuwa na nafasi ndogo kwa sababu watu ni wengi pia alikuwa na marafiki wengi, wengine wa kutoka nje ya nchi kwa hiyo alinishawishi na tukakubaliana kumzika Dar es Salaam,” alisema.

Pia alikanusha uvumi kuwa hajafika msibani kwa kuwa walikuwa na ugomvi na marehemu akisema walishamaliza tofauti zao. Alisema anatarajia kufika leo usiku tayari kushiriki mazishi hayo.

Wabunge kilio Jana, baadhi ya wabunge waliofika nyumbani kwa marehemu Kanumba waliangua vilio wakati walipotoa salamu zao za rambirambi.

Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata hakuzungumza na badala yake aliimba kipande cha wimbo uliozungumzia kifo na maneno ya wimbo huo yalionekana kuwagusa wafiwa na kusababisha vilio kuanza upya huku baadhi wakipoteza fahamu.
Mbunge mwingine, Neema Mwinyimgaya aliongeza majonzi masibani hapo alipounganisha msiba huo na wa mama yake… “Mama yangu amefariki miezi mitatu iliyopita, huko uliko mama, nakuomba umpokee kijana mwenzetu,” alisema mbunge huyo na kushindwa kuendelea.

Wabunge wengine waliohudhuria msiba huo ni Ismail Aden Rage (Tabora Mjini), Aboud Juma (Kibaha Vijijini), Mussa Azan Zungu (Ilala), Abbas Mtemvu (Temeke), Peter Serukamba (Kigoma Mjini) na Ritha Kabati (Viti Maalumu).
Kova na mchango wa Kanumba Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema anakumbuka mchango wa Kanumba katika kuzuia uhalifu jijini.

“Tulishirikiana naye pamoja na wasanii wengine kuandaa bonanza maalumu ambalo lilidhamiria kukabiliana na uhalifu hapa jijini na kwa kweli mchakato ule ulifanikiwa kwani uhalifu ulipungua kwa kiasi kikubwa” alisema Kova.
“Kifo chake kimekuwa cha ghafla mno na nafikiri kujiweka tayari (kiimani) ni jambo ambalo kila mmoja anatakiwa kuwa makini nalo katika maisha yake,” alisema Kova.

Ratiba ya mazishi
2:30 - Msafara kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia Barabara ya Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi hadi Viwanja vya Leaders Club.
3:30 - Misa ya kumuombea na salamu mbalimbali.
6:00 – Kuaga
9:00 - Kuelekea Makaburi ya Kinondoni kupitia Barabara ya Tunisia

SAHIHISHO
Rais Jakaya Kikwete jana alilazimika kubadili ratiba yake ya safari za ndani ya nchi ili kwenda kujumuika na waombolezaji wengine katika msiba wa msanii nguli, Steven Kanumba na hakuwa na safari nje ya nchi kama ilivyoripotiwa na gazeti hili jana. Mhariri.

SOMA HABARI ZAIDI HAPA: