Showing posts with label Premiere. Show all posts
Showing posts with label Premiere. Show all posts

Saturday, November 05, 2016

FIlamu na Tamthilia za Kitanzania Zazinduliwa Jijini Dar es Salaam - Zitarushwa na DSTV

Mwenyekiti wa Bodi ya DSTV, Balozi Ali Mpungwe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Filamu na Tamthilia za Kitanzania zitakazorushwa na DSTV kupitia Chaneli yao kuanzia Maisha Magic Bongo Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo akizungumza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Mtendaji Mkuu wa Multchoice, Chande Maharage, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Chaneli ya Maisha  Magic Bongo, Barbara Kambogi akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu MNET, Yalisa Phawe akitoa hutuba fupi katika uzinduzi huo. Kulia ni Mkuu wa Chaneli ya Maisha  Magic Bongo, Barbara Kambogi.
Wadau wa filamu wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Viongozi mbalimbali walioshiriki uzinduzi huo.
Wasanii wa filamu na wadau mbalimbali wakiwa kwenye 
uzinduzi huo.
Taswira katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) na viongozi wengine wakizindua Filamu na Tamthilia za Kitanzania.

Na Dotto Mwaibale

TANZANIA imeingia katika mapinduzi makubwa ya tasnia ya filamu baada ya Maisha Magic Bongo kwa kushirikiana na Multchoice Tanzania pamoja na maprodyusa kuzindua rasmi chaneli yao (160) Maisha Magic Bongo itakayo kuwa ilirusha filamu na tamthilia za kitanzania.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu na Tamthilia za kitanzania kwa niaba ya Waziri  wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi, Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo alisema mpango wa kurusha filamu za kitanzania kupitia mtandao wa DSTV utasaidia sana kutangaza filamu zetu na kuleta ushindani katika ulimwengu wa kimataifa.

"Serikali tunaona hili ni jambo muhimu sana litakalowafanya wadau wa kazi za kitanzania kutabasamu tena kwani sote tunafahamu umaarufu wa chaneli zilizopo DSTV na jinsi zinavyoweza kuwafikia watu wengi duniani" alisema Fissoo.

Aliongeza kuwa uzinduzi huo uliohusisha filamu sita, tamthilia mbili na kazi nyingine mbili DSTV wametoa mtaji wa dola za kimarekani 450,000.

Mkuu wa Chaneli ya Maisha  Magic Bongo, Barbara Kambogi alisema uzinduzi huo umelenga kusherehekea kazi nzito za maprodyusa wa filamu hapa nchini na utambulisho rasmi wa chaneli yetu yenye maudhui ya kitanzania.

Alisema chaneli hiyo imelenga kuburudisha na kuelimisha watamazaji wa kitanzania kupitia filamu, tamthilia na maigizo mbalimbali ya kiswahili.

Aliongeza kuwa chaneli hiyo itapatikana kwenye kifurushi cha huduma za DSTV (160).


Mwenyekiti wa Bodi ya DSTV, Balozi Ali Mpungwe alisema DSTV Tanzania imetoa ajira 80 hivyo kusaidia katika maendeleo ya nchi.

Mtendaji Mkuu wa Multchoice, Chande Maharage alisema mpango huo utasaidia kukuza lugha ya kiswahili kama alivyokuwa akifanya mtunzi wa mashairi hayati marehemu Shabani Robert katika kukuza lugha hiyo.


Wednesday, November 18, 2009

Sinema - Precious (PUSH: Based on the Novel by Sapphire)


Wadau, jana nilienda Loews AMC Boston Common kuona sinema, Precious. Ilikuwa Advance Screening kiingilio bure. Kwa bahati mbaya nilishindwa kuingia kwani nilikuwa kati ya watu zaidi ya 1,000 waliorudishwa kwa vile ukumbi ulikuwa umejaa. Watu walifika pale saa 9 mchana, na screening ilikuwa saa moja. Nilifika pale saa 12 kasorobo na mamia ya watu walikuwa wanarudhishwa! Walisema waliofika hiyo saa 9 walikuwa wengi mno na kujaza ukumbi!
Watu wamekuwa wakingoea kuona hii sinema kwa zaidi ya mwaka moja! Stelingi wake ni Mo'nique na mgeni katika sinema, Gabourey 'Gabby' Sidibe. Inahusu maisha ya msichana mwenye miaka 16 aliyebakwa na baba yake na kuzaa watoto wawili huko Harlem, New York mwaka 1987. Kwa vile ni mweusi tii na mnene anaona kama hana thamani duniani. Gumzo ni kuwa sinema ni nzuri mno na huenda stelingi wake na sinema enyewe itapata tuzo ya Oscar.
Ijumaa wiki hii sinema itaonyeshwa katika sinema kadhaa hapa Marekani. Nitaenda kuangalia na kuwapa maoni yangu.

Friday, April 04, 2008

Bongoland II Premiere - Kesho April 5, 2008



Hii ni kukumbusha kuwa kesho, ndio uzinduzi rasmi wa sinema ya Bongoland II. Hii ni sinema iliyoshutiwa mjini Dar-es-salaam mwaka jana. Ni sinema ambayo iliwahusha wasanii mbali mbali wa kutoka Tanzania. Kama Mzee Kipara, Huyu ni mzee wa zamani sana ambaye alicheza katika michezo ya redio na umaarufu wake katika sana Tanzania bado ni wa hali ya juu.

Pia yumo Bi Chuma Selemani Mzee ambaye huko Afrika Mashariki ameshiriki katika sinema nyingi tu zilizotengenezewa pale Dar-es-Salaam. Kwa upande wa kizazi kipya kuna wasanii chipukizi wengi hasa hasa watu kama Peter Omari ambaye alikuwa mkazi wa Minneapolis na ambaye ndiye msanii mkuu katika sinema hii. Peter alikuwa katika sinema ya Tusamehe kama mchungaji.

Unaweza kusoma habari za wasanii wote waliosiriki katika sinema hii hapaVile vile kuna wasanii chipukizi kama Shafii Abdul ambaye kusema kweli anaonyesha uzoefu mkubwa katika fani hii ya usanii.Mwanamziki maafuku wa bongo BUSHOKE naye yuko katika sinema hii.Katika utengezaji wa sinema hii, Kibira Films ilishirikiana na chuo kikuu cha UCLA kwa vitivyo vya filamu na Kiswahili. Wanafunzi wanane walisaidia kitaalamu katika harakati za Bongoland II pale mjini Dar.Kwa ujumla, hii ni hatua kubwa sana kwa sababu lengo letu ni kuupamba utamaduni wa watu wa Afrika Mashariki na hasa Tanzania.

Pia ni kuvionyesha vipaji vya wasanii katika sehemu za kimataifa.Kwa hiyo sinema hii itaonyeshwa kwa mara ya kwanza hapa Minneapolis saa nane na saa kumi na moja hapa OAK STREET CINEMAUnaweza kuona Trela ya kwanza hapa au ya Trela ya pili hapa.Tunategemea kuwa utaweza kufika. Kwa maelezo zaidi ya uzinduzi unaweza ukayapata hapa.