Friday, April 04, 2008

Bongoland II Premiere - Kesho April 5, 2008



Hii ni kukumbusha kuwa kesho, ndio uzinduzi rasmi wa sinema ya Bongoland II. Hii ni sinema iliyoshutiwa mjini Dar-es-salaam mwaka jana. Ni sinema ambayo iliwahusha wasanii mbali mbali wa kutoka Tanzania. Kama Mzee Kipara, Huyu ni mzee wa zamani sana ambaye alicheza katika michezo ya redio na umaarufu wake katika sana Tanzania bado ni wa hali ya juu.

Pia yumo Bi Chuma Selemani Mzee ambaye huko Afrika Mashariki ameshiriki katika sinema nyingi tu zilizotengenezewa pale Dar-es-Salaam. Kwa upande wa kizazi kipya kuna wasanii chipukizi wengi hasa hasa watu kama Peter Omari ambaye alikuwa mkazi wa Minneapolis na ambaye ndiye msanii mkuu katika sinema hii. Peter alikuwa katika sinema ya Tusamehe kama mchungaji.

Unaweza kusoma habari za wasanii wote waliosiriki katika sinema hii hapaVile vile kuna wasanii chipukizi kama Shafii Abdul ambaye kusema kweli anaonyesha uzoefu mkubwa katika fani hii ya usanii.Mwanamziki maafuku wa bongo BUSHOKE naye yuko katika sinema hii.Katika utengezaji wa sinema hii, Kibira Films ilishirikiana na chuo kikuu cha UCLA kwa vitivyo vya filamu na Kiswahili. Wanafunzi wanane walisaidia kitaalamu katika harakati za Bongoland II pale mjini Dar.Kwa ujumla, hii ni hatua kubwa sana kwa sababu lengo letu ni kuupamba utamaduni wa watu wa Afrika Mashariki na hasa Tanzania.

Pia ni kuvionyesha vipaji vya wasanii katika sehemu za kimataifa.Kwa hiyo sinema hii itaonyeshwa kwa mara ya kwanza hapa Minneapolis saa nane na saa kumi na moja hapa OAK STREET CINEMAUnaweza kuona Trela ya kwanza hapa au ya Trela ya pili hapa.Tunategemea kuwa utaweza kufika. Kwa maelezo zaidi ya uzinduzi unaweza ukayapata hapa.

No comments: