Showing posts with label Filamu. Show all posts
Showing posts with label Filamu. Show all posts

Saturday, January 07, 2017

Bodi ya Filamu Nchini Yawaomba WaTanzania Kuzipigania Kura Filamu za Kitanzania Kwenye Tuzo za AMV

BMGHabari
Bodi ya Filamu nchini imewahamasisha watanzania kuongera ari ya kuzipigia kura filamu za kitanzania zinazowania tuzo za Africa Magic Viewers Awards (AMVA 2017) za nchini Nigeria.

Katibu Mtendaji wa bodi hiyo, Bi Joyce Fissoo (pichani juu) ametoa hamasa hiyo hii leo, wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power Break Fast On Saturday kinachoendeshwa na watangazaji Philip Mwihava na Godfrey Kusolwa.

“Filamu hizo ni Naomba Niseme, Aisha na Home Coming ambazo zinawania tuzo za filamu bora na Siri ya Mtungi ambayo inagombea filamu bora ya lugha ya Kiswahili. Niwaase Wanzania, ushindi wa filamu hizi ni sisi kuwapigia kura hawa vijana wetu ambao wameshika bendera yetu kwenda kutuwakilisha kule Nigeria, niwasihi waweze kuzipigia kura na wahakikishe wanahamasisha marafiki zao pia kuzipigia kura ili nafasi zote tuzo zije Tanzania”. Amesisitiza Fissoo.
Naye Mtayarishaji wa filamu nchini, Staphord Kihole (pichani) ambaye pia alikuwa kwenye kipindi hicho, ametumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kuzipigia kura filamu za kitanzania ili zishinde tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards ikiwemo filamu yake ya "Naomba Niseme" inayowania vipengele viwili, kikiwemo kipendele cha Best East Africa na Best All Africa kinachoamuliwa na majaji.

Ili kuzipigia kura filamu za Tanzania ambazo ni Naomba Niseme, Aisha na Home Coming, unapakua Application ya We Chat, unajisajiri kwenye Africa Magic kwa kutumia nambari ya simu na kisha unatafuta kipengele cha AMVCA na utaweza kupiga kura kadri upendavyo ambapo mtu mmoja anaweza kupiga kura hadi 100 kwenye filamu tofauti tofauti.
Bonyeza Hapa  Au play hapo chini kusikiliza sauti  Credit: Clouds Fm

Saturday, December 17, 2016

Katibu Tawala Moani Mara Ahitimisha Mafunzo kwa Wadau wa Filamu Mkoani Humo

Katibu Tawala mkoa wa Mara, Adoh Mapunda (katikati) akizungumza hii leo kwenye kilele cha mafunzo ya siku tatu kwa wadau wa filamu mkoani humo. Mafunzo hayo yalianza juzi Disemba 14,2016 kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Mara Mjini Msoma.

Yaliandaliwa na Bodi ya Filamu nchini kwa lengo la kuwajengea welezi wanatasinia wa filamu ili kuzalisha kazi zenye ubora na hivyo kukidhi ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi ambapo zaidi ya washiri 200 walionufaika na mafunzo hayo wamepatiwa vyeti. Tayari mafunzo ya aina hiyo yamefanyika mikoa ya Morogoro na Mwanza na yataendelea katika mikoa mingine.
#BMGHabari
Wanatasnia wa filamu mkoani Mara wakimsikiliza Katibu Tawala mkoani humo, Adoh Mapunda, wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia hao. Ameahidi kutoa fulana (Tshirt) 250 kwa ajili ya wanatasnia wa filamu mkoani Mara waliohudhuria mafunzo hayo ambapo zitawasaidia hususani kuwa na sare ya aina moja wakikutana kwa pamoja
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao, amesema sekta ya filamu ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa wanatasnia wake na taifa kwa ujumla hivyo Bodi za filamu mikoani zihakikishe zinasimamia maendeleo ya tasnia hiyo.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso, amebainisha kwamba wadau wa filamu wakiwemo watayarishaji, waongozaji, wahariri pamoja na waigizaji wamefundishwa vyema mafunzo hayo ili kuzalisha kazi bora.
Mgeni rasmi, Katibu Tawala mkoani Mara, Adoh Mapunda (wa pili kulia), akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao, akipokea cheti cha utambuzi
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso
Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Bi.Deograsia Ndunguru, kutoka Chuo Kikuu Dodoma, akipokea cheti cha utambuzi kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, akipokea cheti cha utambuzi kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Mwanahabari Genoveva kutoka Idara ya Habari Serikalini, akipokea cheti cha utambuzi kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Katibu wa Chama cha Waigizaji mkoani Mara, Johnson Ibambai, akipokea cheti cha utambuzi kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Mwakilishi wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Mara, akipokea cheti cha utambuzi kwa niaba yake kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Mwanahabari Amicus Butunga, akipokea cheti cha utambuzi kwa niaba ya TBC kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Mwanahabari George Binagi akipokea cheti cha utambuzi kwa niaba ya 102.5 Lake Fm kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Katibu Tawala mkoa wa Mara, Adoh Mapunda (mwenye suti) na viongozi wengine wakiwa pamoja na washiriki wa mafunzo ya filamu mkoani Mara wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Katibu Tawala mkoa wa Mara, Adoh Mapunda (mwenye suti) na viongozi wengine wakiwa pamoja na washiriki zaidi ya 200 wa mafunzo ya filamu mkoani Mara wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mwigizaji Dan Msimamo kutoka Tarime amesema mafunzo hayo yatawasaidia kuinua ubora wa filamu mkoani Mara na hivyo kukuza soko lake
Mwigizaji Justar Lucas kutoka Tarime amesema mafunzo hayo yamewaongezea weledi na kutambua kwamba filamu ni ajira na ikitumika vyema husaidia kukuza kipato cha wanatasnia wa filamu na taifa kwa ujumla.
Mwigizaji Innocent Mbalwa kutoka Bunda ameishukuru Serikali kupitia Bodi ya Filamu kwa kutoa mafunzo hayo ambapo amesema yatafungua milango mipya kwenye tasnia ya filamu mkoani Mara.
Mwigizaji Jackline James kutoka Musoma amesema mafunzo hayo yamemsaidia kutambua kwamba filamu ni ajira tofauti na alivyokuwa akidhani awali kwamba tasnia hiyo ni sehemu ya burudani.
******************
Katibu Tawala mkoani Mara, Adoh Mapunda, amewahimiza wanatasnia wa filamu mkoani humo kuwa wabunifu katika uzalishaji wa kazi zao ili kupanua soko la filamu ndani na nje ya nchi.

Mapunda ametoa rai hiyo hii leo, wakati akihitimisha mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia wa filamu mkoani Mara, yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini ili kukuza welezi katika uzalishaji wa kazi bora na zenye maudhui yanaykubalika katika jamii.

"Ubunifu ndio unahitajika hivi sasa, watu wengi wanahitaji ubunifu binafsi na siyo "kucopy" na "kupaste" kazi za wengine". Amesisitiza Mapunda na kuongeza kwamba serikali itatoa ushirikiano wa dhati katika kuboresha tasnia hiyo ya filamu kwani hivi sasa hutoa ajira na kukuza uchumi kwa taifa.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Millao, ameziagiza Bodi za Filamu za mikoa kuhakikisha kwamba zinatimiza wajibu wake ipasavyo ili kuboresha zaidi sekta hiyo.

Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fisso, amewahimiza wadau wa filamu mkoani Mara wakiwemo watayarishaji, waongozaji, wahariri pamoja na waigizaji walionufaika na mafunzo hayo, kuyatumia vyema ili kukuza soko lao la filamu.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, amewasisitizia hao kutumia mafunzo hayo ili kuzalisha filamu na vipindi vya luninga vyenye ubora ili kunufaika na uhitaji uliopo.

Akisoma maazimio ya wanatasnia wa filamu mkoani Mara, Katibu wa Chama cha Waigizaji mkoani humo, Johnson Ibambai, ametaja baadhi ya maazimio hayo kuwa ni pamoja na kuiomba serikali kuweka mitaala ya filamu kuanzia shule za msingi na vyuo vya ufundi VETA ili kusadia utoaji wa elimu hiyo ya filamu.
Tazama picha zaidi HAPA

Saturday, November 05, 2016

FIlamu na Tamthilia za Kitanzania Zazinduliwa Jijini Dar es Salaam - Zitarushwa na DSTV

Mwenyekiti wa Bodi ya DSTV, Balozi Ali Mpungwe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Filamu na Tamthilia za Kitanzania zitakazorushwa na DSTV kupitia Chaneli yao kuanzia Maisha Magic Bongo Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo akizungumza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Mtendaji Mkuu wa Multchoice, Chande Maharage, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Chaneli ya Maisha  Magic Bongo, Barbara Kambogi akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu MNET, Yalisa Phawe akitoa hutuba fupi katika uzinduzi huo. Kulia ni Mkuu wa Chaneli ya Maisha  Magic Bongo, Barbara Kambogi.
Wadau wa filamu wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Viongozi mbalimbali walioshiriki uzinduzi huo.
Wasanii wa filamu na wadau mbalimbali wakiwa kwenye 
uzinduzi huo.
Taswira katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) na viongozi wengine wakizindua Filamu na Tamthilia za Kitanzania.

Na Dotto Mwaibale

TANZANIA imeingia katika mapinduzi makubwa ya tasnia ya filamu baada ya Maisha Magic Bongo kwa kushirikiana na Multchoice Tanzania pamoja na maprodyusa kuzindua rasmi chaneli yao (160) Maisha Magic Bongo itakayo kuwa ilirusha filamu na tamthilia za kitanzania.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu na Tamthilia za kitanzania kwa niaba ya Waziri  wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi, Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo alisema mpango wa kurusha filamu za kitanzania kupitia mtandao wa DSTV utasaidia sana kutangaza filamu zetu na kuleta ushindani katika ulimwengu wa kimataifa.

"Serikali tunaona hili ni jambo muhimu sana litakalowafanya wadau wa kazi za kitanzania kutabasamu tena kwani sote tunafahamu umaarufu wa chaneli zilizopo DSTV na jinsi zinavyoweza kuwafikia watu wengi duniani" alisema Fissoo.

Aliongeza kuwa uzinduzi huo uliohusisha filamu sita, tamthilia mbili na kazi nyingine mbili DSTV wametoa mtaji wa dola za kimarekani 450,000.

Mkuu wa Chaneli ya Maisha  Magic Bongo, Barbara Kambogi alisema uzinduzi huo umelenga kusherehekea kazi nzito za maprodyusa wa filamu hapa nchini na utambulisho rasmi wa chaneli yetu yenye maudhui ya kitanzania.

Alisema chaneli hiyo imelenga kuburudisha na kuelimisha watamazaji wa kitanzania kupitia filamu, tamthilia na maigizo mbalimbali ya kiswahili.

Aliongeza kuwa chaneli hiyo itapatikana kwenye kifurushi cha huduma za DSTV (160).


Mwenyekiti wa Bodi ya DSTV, Balozi Ali Mpungwe alisema DSTV Tanzania imetoa ajira 80 hivyo kusaidia katika maendeleo ya nchi.

Mtendaji Mkuu wa Multchoice, Chande Maharage alisema mpango huo utasaidia kukuza lugha ya kiswahili kama alivyokuwa akifanya mtunzi wa mashairi hayati marehemu Shabani Robert katika kukuza lugha hiyo.


Friday, April 18, 2014

Against the Jab - Film Made in Boston by Patrick Jerome

  • MESSAGE FROM BOSTON FILMMAKER PATRICK JEROME
     
    Pat Jerome

    I need your help to support my movie AGAINST THE JAB. We have an important screening this Saturday April 19 at 7:30pm at AMC loews Theater Boston Common. I will have a Q & A after the showing with the audience. The goal for this screening is set up a wider distribution or influence more distribution outlets around the country. I hope you can come and support. The tickets is $12.00 if you cannot make it. Please tells a friend that may be available that day. I would greatly appreciate it. If you have any questions please let me know. https://www.amctheatres.com/movies/session-28b-against-the-jab You may need the set the theater location if you don't live in Boston. It usually say showtime is not available in your area. You need to set the location by enter the theater zip code 02111, MA. Patrick
    Session 28B- Against the Jab
    www.amctheatres.com
    On this installment of AMC Movie Talk (Wednesday April 16th 2014) we discuss: New X-MEN Trailer review Ferrell and Reilly re-team for BORDER GUARDS Walker's brothers join FAST 7 MAGIC MIKE XXL gets...

Saturday, April 07, 2012

Ukiwa mwaminifu wa mapenzi, wewe ni "zoba"... Kifo cha Kanumba

Da Subi anatoa maoni yake juu ya kifo cha msanii maarufu wa Tanzania, Steven Kanumba, aka. Kanumba the Great aka. Denzel Washington wa Tanzania.
****************************************************************
 
Picture
Ikiwa ni kweli kuwa kifo cha Steven C. Kanumba, aliyekuwa mwigizaji maarufu wa filamu na sinema, kimesababishwa na ugomvi wa mapenzi uliotokana na kukosekana uaminifu, basi kauli niliyoitoa hapo juu ambayo nimeinukuu kwenye "zilipendwa", wimbo wa "Kadiri Kasimba" una ukweli na, waliotutangulia si wehu. Waliyaona! Wakatuasa. Tunajifunza?

Juzi hapa msanii "Diamond" kwenye mahojiano na CloudsFM kuhusu Wema Sepetu, aliyatamka maneno haya, "ku-cheat katika mapenzi ni kitu cha kawaida" bofya hapa kusikiliza kiwa huamini.

Si kwamba ninaamini takwimu finyu ya mtu mmoja na kuichukulia ya jamii nzima. Hapana.

Na si kwamba siamini maneno hayo au ni jambo geni sana kwangu, hapana.

Kilichonistusha ni kusema, "ni kitu cha kawaida"... kwamba ni kawaida tu kusalitiana kwenye mapenzi. Kwa vile aliyeyatamka ni msanii kioo katika jamii, sina uhakika kama ndivyo ilivyo kwenye ulimwengu wao wa wasanii au kwa vile anaishi katikati ya jamii na anawasiliana na wanajamii wengi, basi ameyaona hayo kila pahala, kwa hivyo imezoeleka na hakuna haja ya kustuka wala kushangaa usaliti unapotokea kwenye mapenzi.
  1. Tamaa - kushindwa kuzizuia tamaa zako za hali (mwili, muonekano, wasifu n.k.) au tamaa za mali
  2. Vishawishi - kushindwa kuzuia vishawishi vinavyoletwa kwako na wengine kwa njia ya tamaa (tizama namba 1) zao kwako.
Mengine yote yanayoufauta baada ya hapo kwa kweli ni sababu au visingizio vya kabla au baada

Msanii Lulu Anashikiliwa na Polisi!

Msanii, Elizabeth Michael aka. Lulu (18) anashikiliwa na Polisi Oyster Bay, Dar es Salaam, baada ya ugomvi na mpenzi wake marehemu Steven Kanumba.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni Charles Kenyela, amethibitisha kushikiliwa kwa Lulu
Habari zinasema kuwa Kanumba alikuwa anajiandaa kutoka na mpenzi wake usiku wa kuamkia leo, alipokuwa bafuni anaoga akamsikia Lulu akiongea kwenye simu na mwanaume mwingine. Alipotoka bafuni kumwuliza kuhusu simu, Lulu alimsukuma kwenye ukuta, Kanumba kaanguka kufa pao hapo!  Ina maana kuwa kifo cha Kanumba umesabishwa na 'Domestic Violence'!

Mungu ailaze roho ya Steven mahala pema mbinguni.   Ameacha pengo kubwa katika fani ya sinema Tanzania.


pichani - Msanii  Elizaneth Michael aka. Lulu, ambaye alikuwa Mpenzi wa Steven Kanumba

Elizabeth Michael , aka, Lulu,  Julai 1, 2007, alipokuja kwenye audition ya Sinema Bongoland 2, aliigiza katika hiyo sinema kama, Chapati Girl
Lulu akipiga pozi hii karibuni


Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

Kuna picha nyingine ya Lulu HAPA:

Kwa habari za kilio nyumbani kwa KANUMBA MTEMBELEE KAKA MICHUZI KWA KUBOFYA HAPA:

KUSOMA SIMULIZI YA UGOMVI NA MDOGO WAKE KANUMBA ALIYESHUHUDIA BOFYA HAPA:

Friday, April 06, 2012

Bongo Superstar Steven Kanumba Afariki Dunia!

Steven Kanumba
Mwigazaji maarufu wa Tanzania, Steven Kanumba aka. Denzel wa Tanzania, amefariki dunia leo jioni mjini Dar es Salaam.

Habari nilizosikia ni kuwa amefariki ghafla! 

Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.

Nalia, Tanzania imepoteza msanii mwenye kipaji na moyo wa fani yake. Pia ilikuwa ni ndoto yangu kuigiza sinema na Kanumba.

Mwaka 2007 Waaigizaji  Steven Kanumba (kulia) na Emmanuel Myamba (kushoto) walikuja kututembelea kwenye set ya sinema Bongoland 2, wakati tulikuwa Magomeni Mikumi mjini Dar es Salaam.

Friday, February 10, 2012

Warsha ya Uandishi wa Miswaada ya Filamu - UDSM

WARSHA YA UANDISHI WA MISWAADA YA FILAMU/SCREENPLAY WORKSHOP
(Level 1)


Je? Unajua kuwa hadithi za Filamu zozote hujengwa kwa wahusika, wahusika ndiyo wabeba lengo zima la filamu?  Je, wajua jinsi ya kuwa jenga wahusika wako ili waweze kubeba lengo la hadithi ya Filamu kiufasaha? Je,unajua kuwa ukikosea kumjenga mhusika mkuu katika hadithi ya Filamu yako ni vigumu hadithi ya Filamu bora?

Basi ukitaka kuyajua yote haya karibu katika warsha ya uandishi wa miswada ya filamu pale IDARA YA SANAA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM Kuanzia tarehe 13-15 Februari 2012. Kuta kuwa na Warsha ya Uandishi wa Miswaada ya Filamu/Screenplay Workshop (Level 1) Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kila siku kuanzia saa 3 asubuhi hadis aa 8 mchana , Cheti cha Ushiriki kitatolew amwishoni mwa mafunzo.

Warsha itakuwa kwa Kiswahili (na Kiingereza ikibidi)na mshiriki anaweza kuwa mtu yoyote anayependa kuandika miswada ya filamu (amateur scriptwriter) au mwandishi anayechipukia (upcoming scriptwriter)

Hima wadau wote wa Tasnia ya Filamu ,Sanaa, Sanaa za Maonyesho na Uandishi wa ubunifu msikose nafasi hii muhimu ya warsha mafunzo daraja la kwanza ilikujijengea misingi mizuri ya Uandishi wa Miswaada ya Filamu.

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na warsha hii tafadhali wasiliana na IDARA YA SANAA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM , Ndg. John Mwakilama SimuN amba0714 13 22 49, na barua pepe: mwakilamajohn@yahoo.com

Tuesday, December 20, 2011

Matokeo ya Uchaguzi wa Viongozi wa TASA

Taarifa imeletwa na Mdau Emmauel Manase

WALIOCHAGULIWA KWENYE UCHAGUZI NGAZI YA TAIFA WA CHAMA CHA WAANDISHI WA FILAMU/TANZANIA SCREEPTWRITER ASSOCIATION-TASA


1. Abdul Maisala -Mwenyekiti

2. Kimela Billa -Makamu Mwenyekiti

3. Samwel Kitang’ala -Katibu

4. Subira O.Nassor Chuu -Mweka Hazina

5. Mike Sangu -Mjumbe

6. Dimo Debwe -Mjumbe

7. Ramadhani King’aru -Mjumbe

8. Badru Soud -Mjumbe

9. Amos Banzi -Mjumbe

10. Nasir Mohamed -Mjumbe

11. Christian Kauzeni -Mjumbe

12. Pirre Mwinuka Mwakalukwa -Mjumbe

13. Erick Chrispin -Mjumbe

Kwa mujibu wa sharia ya TASA,TASA itakuwa na mikutano mikuu minne kwa mwaka,Mweyekiti ,Makamu Mwenyekiti na Katibu wa TASA Taifa wanapiga kura kwenye uchaguzi w a kuchagua viongozi wa Taifa wa Shirikisho la Filamu/Tanzania Film Federation-TAFF

Tunawapongeza wote waliochaguliwa kama wajumbe na nafasi nyingine za kiutendaji,Tunatarajia kuwa kuchaguliwa kwao kutaleta changamoto za kiutendaji na kusukuma mbele maendeleo ya TASA naTAFF.

Saturday, January 08, 2011

Warsha ya Filamu Tanzania



Habari Wadau wa Tasnia ya Filamu nchini.
Karibuni katika warsha ya kuzungumzia filamu za Kitanzania....
ni Bure kwa kila mtu.
Karibuni wote

Thursday, March 18, 2010

Ray na Vincent Wanatafuta Waigizaji wa Kike Wapya!

Waigizaji wasichana wanahitajika RJ Company

03/18/2010


Kama unajihisi wewe ni mrembo basi kwa sasa tunatafuta wasanii wapya wa kike katika ofisi za RJ COMPANY zilizoko SINZA MORI. Lengo ni kuwapata wasanii wa kike ambao ni wapya katika tasnia ya filam nchini ili waje kushiriki katika filam mpya itakayoandaliwa na kampuni ya RJ. Umri ni kuanzia miaka 18 mpaka 28. Pia unaweza kutuma picha zako kabla hufika ofisini ili tuweze kukuona jinsi ilivyo.Muda wa ofisi ni saa 4 kamili asubuhi mpaka saa 12 jioni kwa siku za Jumatatu mpaka Ijumaa na siku za Jumamosi kuanzia saa 4 kamili asubuhi mpaka saa 8 mchana. HAKUNA GHARAMA ZOZOTE ZILE UTAKAZOLIPISHWA KWANI KAMPUNI INAJITOSHELEZA.

WASILIANA NA VINCENT aka RAY KUPITIA:Tel: +255 714 082729P.O. Box 11347
Email: vincentkigosi@gmail.com
Website: www.rjtanzania.com

*****************************************

Hapo napingana na Ray. Yaani watu zaidi ya miaka 28 hawawezi kuwa warembo? Angesema anatafuta kuanzia 18+. Katika sinema unahitaji waigizaji wa kila umri. Mambo ya vijana kujifanya wazee haipendezi. - Chemi

Sunday, August 30, 2009

Maonyesho ya Filamu Hadharani Marufuku-Mkuchika

Naona wanapunguza milo ya watu! Yaani leo ndo wanarudisha Bodi ya Ukaguzi wa Filamu! Video na DVD zilivyozagaa nchini Bongo mbona watakuwa na kazi ngumu!

**********************************************************
Kutoka ippmedia.com

Na Mwandishi wetu

Serikali imepiga marufuku maonyesho yote ya filamu kwenye hadhara ya watu, majumba yasiyo rasmi, hoteli na maeneo ya baa bila kufuata masharti kwa mujibu wa Sheria.

Agizo hilo limetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu nchini ambayo itakuwa na jukumu la kukagua na kusimamia maonyesho na shughuli za filamu nchini.

Alisema sehemu nyingi zinazotumiwa kuonyesha filamu hazina leseni halali za kuonyeshea na kuongeza kuwa sio salama kwa mali na afya za watu. “Nachukua fursa hii kutoa onyo kwa mtu yeyote atakayeonyesha filamu kwenye hadhara ya watu katika majumba yasiyo rasmi, vibanda, kumbi ndogondogo, hotelini, baa na katika vyombo vya usafiri waache mara moja,” alisisitiza.
Alifafanua kuwa sehemu nyingi zinazotumika kuonyeshea filamu sasa hazikidhi matakwa ya ujenzi wa kumbi za kuonyeshea filamu na ni kinyume cha sheria kwani nyingi zimekuwa chanzo cha maficho ya wahalifu, majambazi, biashara ya dawa za kulevya na kuchochea vitendo vya ngono kwa vijana.

Alisema athari nyingi tayari zimeshajitokeza katika jamii yetu na kuongeza kuwa filamu nyingi zimechangia kubomoa na kudunisha Utamaduni wa taifa letu na hata kuchangia kwa kiasi kikubwa kubomoa misingi ya amani , Upendo , Uadilifu, heshima, uaminifu na utu ambao ni utambulisho wa mtanzania jinsi ulivyokuwa umejijenga na kuenea katika jamii yetu.
Aidha alisema serikali iko makini kuhimiza na kusisitiza matumizi ya sanaa katika masuala mbalimbali ya maendeleo na kuvitambua , kuvikuza na kuviendeleza vipaji vya wasanii katika kukuza taaluma na fani ya filamu nchini.

Awali akizungumza kuhusu majukumu ya Bodi hiyo, alisema kuwa Bodi itakuwa na jukumu la kuweka misingi ya kuimarisha utaratibu wa usimamizi wa utengenezaji wa filamu na pia kutoa vibali vya kutengeneza filamu hapa nchini.

Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bi. Rose Sayore ameihakikishia serikali kuwa Bodi yake itafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha kuwa kanuni, sheria , maadili na taratibu za uonyeshaji na utengenezaji wa filamu zinazingatiwa kwa maslahi ya watanzania na vizazi vijavyo.