Showing posts with label Pres. Levy Mwanawasa. Show all posts
Showing posts with label Pres. Levy Mwanawasa. Show all posts

Wednesday, September 03, 2008

Rais Levy Mwanawasa azikwa Zambia leo

Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma wakitoa salamu za mwisho kwa marehemu Rais wa Zambia, Levy Mwanawasa. (picha na Freddy Maro wa Ikulu)
Rais Robert Mugabe wa Zambia, akimpa pole mjane wa Rais Mwanawasa, Mama Maureen Mwanawasa.


Marehemu Rais Mwanawasa alizikwa leo huko Zambia na heshima zote za kitaifa. Jeneza lake lilitengenezwa na 'copper' ambao ni chuma linaloingiza pesa nyingi za kigeni kwa waZambia. Mzee Mwanawasa alipiga vita ufisadi katika mambo ya machimbo ya copper huko Zambia. Alifariki nchini Ufaransa tarehe 19 Agosti alipokuwa anapata matibabu kutokana na kuugua ugonjwa wa kiharusi (stroke).

Kwa habari zaidi someni:

http://afp.google.com/article/ALeqM5jwNZ3tMG8KG-rFekS9Gn1oy4rAdQ

http://english.aljazeera.net/news/africa/2008/09/200893161946349113.html

Tuesday, August 19, 2008

Rais wa Zambia Afariki


Nilikuwa nasita kuposti habari hizi mpaka kupata thibitisho. Unakumbuka hivi karibuni kulitokea uzushi kuwa Rais Levy Mwanawasa (59) amefariki akiwa kwenye mkutano Misri kumbe ilikuwa si kweli.

Sasa ni kweli amefariki huko Ufaransa alipokuwa anapata matibabu kutokana na kuugua kiharusi/kupooza (stroke).
Poleni wananchi wa Zambia kwa msiba huo mzito.

Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. AMEN.

*******************************************************************************

Zambian president dies after stroke

Mwanawasa won praise for his economic reforms and anti-corruption drive [AFP]
Levy Mwanawasa, the Zambian president, has died in hospital in Paris, where he was receiving treatment following a stroke he suffered earlier in the year.

Rupiah Banda, the country's vice-president, told state media on Tuesday that Mwanawasa had died and that seven days of national mourning had been declared.

"Fellow countrymen, with deep sorrow and grief, I would like to inform the people of Zambia that our president Dr Levy Patrick Mwanawasa died this morning at 10:30 hours [08:30 GMT]," Banda said.

Mwanawasa's health deteriorated after he suffered a stroke while attending an African Union summit in Egypt in June.

He was rushed to a hospital in Paris, the French capital and a statement on Monday night indicated that the president's health had taken a turn for the worse.
Outspoken leader

Mwanawasa was elected president in 2002, Zambia's third president since independence from Britain in 1964.

He won praise for his anti-corruption and economic modernization drive in one of the world's biggest copper producers, but was unable to lift his nation out of poverty.

In recent months, he broke African leader's traditional silence towards the actions of Robert Mugabe, the Zimababwean president, describing Zimbabwe as a "catastrophe" and criticising the the 2008 presidential elections.

Under Zambia's constitution, elections are meant to be held within 90 days of his death.
Vice-president Banda is expected to take over as acting president until then.
Kwa habari zaidi soma:

Tuesday, July 08, 2008

Aliyeanzisha uzushi kuwa Rais Mwanawasa kafa Anatafutwa!

Rais Levy Mwanawasa wa Zambia

Mnakumbuka mwishoni mwa wiki iliyopita, kulikuwa na uzushi kuwa Rais Levy Mwanawasa wa Zambia alifariki hospitalini huko Ufaransa baada ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi akiwa kwenye mkutano huko Misri.

Habari zilienea kwa kasi mpaka Rais Thabo Mbeki, wa Afrika Kusini alitangaza na kuomba watu wakae kimya kwa dakika moja kwa heshima ya Mwanawasa.

Habari zinasema kuwa Rais Mwanawasa anaendelea vizuri na sasa aliyeanzisha huo uzushi anatafutwa ajieleze. Anaitwa Marlone Zaza na eti aliwambia waandishi wa habari Afrika Kusini wa 702 Talk radio, kuwa yeye ni "Chief of Protocol' katika ubalozi wa Zambia huko. WaZambia wanasema kuwa hawana mtu kama huyo huko ubalozini. WaAfrika Kusini wanasema kuwa hata hawana uhakika kama huyo jamaa ni MZambia au ni raia wa nchi gani. Nami nauliza kama hiyo ni jina la huyo jamaa kweli.

Habari zinasema kuwa Zaza amezima simu yake na kajificha.

Kwa sasa tuendelee kumwombea uzima Rais Mwanawasa.
********************************************

Kwa habari zaidi someni: