Tuesday, August 19, 2008

Rais wa Zambia Afariki


Nilikuwa nasita kuposti habari hizi mpaka kupata thibitisho. Unakumbuka hivi karibuni kulitokea uzushi kuwa Rais Levy Mwanawasa (59) amefariki akiwa kwenye mkutano Misri kumbe ilikuwa si kweli.

Sasa ni kweli amefariki huko Ufaransa alipokuwa anapata matibabu kutokana na kuugua kiharusi/kupooza (stroke).
Poleni wananchi wa Zambia kwa msiba huo mzito.

Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. AMEN.

*******************************************************************************

Zambian president dies after stroke

Mwanawasa won praise for his economic reforms and anti-corruption drive [AFP]
Levy Mwanawasa, the Zambian president, has died in hospital in Paris, where he was receiving treatment following a stroke he suffered earlier in the year.

Rupiah Banda, the country's vice-president, told state media on Tuesday that Mwanawasa had died and that seven days of national mourning had been declared.

"Fellow countrymen, with deep sorrow and grief, I would like to inform the people of Zambia that our president Dr Levy Patrick Mwanawasa died this morning at 10:30 hours [08:30 GMT]," Banda said.

Mwanawasa's health deteriorated after he suffered a stroke while attending an African Union summit in Egypt in June.

He was rushed to a hospital in Paris, the French capital and a statement on Monday night indicated that the president's health had taken a turn for the worse.
Outspoken leader

Mwanawasa was elected president in 2002, Zambia's third president since independence from Britain in 1964.

He won praise for his anti-corruption and economic modernization drive in one of the world's biggest copper producers, but was unable to lift his nation out of poverty.

In recent months, he broke African leader's traditional silence towards the actions of Robert Mugabe, the Zimababwean president, describing Zimbabwe as a "catastrophe" and criticising the the 2008 presidential elections.

Under Zambia's constitution, elections are meant to be held within 90 days of his death.
Vice-president Banda is expected to take over as acting president until then.
Kwa habari zaidi soma:

1 comment:

Anonymous said...

Alikuwa Raisi safi sana huyu kuliko karibu maraisi wote wa Afrika kwa kupenda wawekezaji wadogo waafrika ngozi nyeusi..

Kama kuna mtu alipenda wawekezaji waafrika ni huyu.aliwaheshimu hadi wawekezaji wadogo kabisa wa kiwango cha machinga..

Zambia ndiyo nchi pekee Afrika mashariki, kati na kusini ambako kumejaa wawekezaji wadogo wa Afrika weusi kutoka nchi nyingi za Afrika .Ukienda utawakuta Watanzania kibao kuanzia karibu kila kabila la Tanzania liko kule,Warundi,wanyarwanda,wakongo,wazimbabwe,waafrika ya kusini,wanamibia,waswazi n.k wanaendesha biashara zao kihalali bila bughudha kabisa kutoka serikali ya Mwanawasa..

Mwanawasa alitambua kuwa wawekezaji wadogo waafrika weusi kutoka mataifa mengine ni muhimu kwa uchumi jikimu hasa wa Afrika na Zambia.Wafanyabiashara wadogo waafrika toka nchi za Afrika wamejaa sana Zambia.Wana maduka,viwanda,n.k na wanapewa leseni na hawabughudhiwi tofauti na nchi kama Tanzania,Kenya na Uganda ambako watu wanajifanya wazawa sana na wana utaifa sana wakati utaifa wenyewe ni wa kuwakataa waafrika wenzao na kuwakumbatia wahindi na waarabu,wazungu au watu wenye mitaji mikubwa toka nje ya bara la Afrika.


Kama kuna Raisi mfano wa wengine kuiga kuwainua waafrika wengine kwenye eneo la uwekezaji wa watu wadogo wenye mitaji midogo kutoka mataifa mengine ya kiafrika na kuwatambua na kuwaheshimu Mwanawasa ni mfano mzuri tofauti na nchi nyingine ambako wazungu,wahindi na waarabu ndio hasa wanaonekana ndio wawekezaji na wanasiasa wanashindana kujikomba kwao na kuwatambua kama ndio wenyewe kwa uwezekezaji na kuwakimbiza mitaani kwa viboko machinga wao wa kiafrika na kuwatoa vijijini wawekezaji wadogo waafrika ngozi nyeusi wanaochimba dhahabu kwa majembe ya mikono ili wawapishe watu wa nje waje wachimbe na magreda!!!.Hata mchimba dhahabu kwa jembe la mkono ni mwekezaji wa kiwango chake cha mtaji huo wa jembe alichojaliwa na mola wake hicho ndicho nilichojifunza kwa Mwanawasa na siasa zake za kujali waaafrika wawekezaji wadogo.Hata kama Afrika au dunia haitakukumbuka mimi binafsi nitakukumbuka kama shujaa wa Afrika na mheshimu waafrika na mitaji yao midogo.

Na mazishi yako lazima nitahudhuria.

I salute you Mwanawasa.Rest in PEACE

Koloboi@yahoo.com