Tuesday, July 08, 2008

Aliyeanzisha uzushi kuwa Rais Mwanawasa kafa Anatafutwa!

Rais Levy Mwanawasa wa Zambia

Mnakumbuka mwishoni mwa wiki iliyopita, kulikuwa na uzushi kuwa Rais Levy Mwanawasa wa Zambia alifariki hospitalini huko Ufaransa baada ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi akiwa kwenye mkutano huko Misri.

Habari zilienea kwa kasi mpaka Rais Thabo Mbeki, wa Afrika Kusini alitangaza na kuomba watu wakae kimya kwa dakika moja kwa heshima ya Mwanawasa.

Habari zinasema kuwa Rais Mwanawasa anaendelea vizuri na sasa aliyeanzisha huo uzushi anatafutwa ajieleze. Anaitwa Marlone Zaza na eti aliwambia waandishi wa habari Afrika Kusini wa 702 Talk radio, kuwa yeye ni "Chief of Protocol' katika ubalozi wa Zambia huko. WaZambia wanasema kuwa hawana mtu kama huyo huko ubalozini. WaAfrika Kusini wanasema kuwa hata hawana uhakika kama huyo jamaa ni MZambia au ni raia wa nchi gani. Nami nauliza kama hiyo ni jina la huyo jamaa kweli.

Habari zinasema kuwa Zaza amezima simu yake na kajificha.

Kwa sasa tuendelee kumwombea uzima Rais Mwanawasa.
********************************************

Kwa habari zaidi someni:



1 comment:

Anonymous said...

Bora Mzee wetu yu hai!