Showing posts with label Rungu. Show all posts
Showing posts with label Rungu. Show all posts

Sunday, April 05, 2009

Mume Atalakiwa


Mume atalikiwa sababu ya "rungu" kubwa


Dar Es Salaam, Tanzania


Mwanamke mmoja amerudi kwa wazazi wake akilalamika kwamba "jogoo" la mumewe ni kubwa sana. Mwanamke huyo mkazi wa jijini aliwashangaza ndugu zake waliofika nyumbani kwake alipowatobolea kwamba hawezi kuvumilia "kugongwa" na "rungu" hiyo kubwa ya mumewe.

Awali gazeti la "Kasheshe" lilieleza kwamba, mume alilalamika kwa ndugu za mkewe akisema tangu wafunge ndoa miezi minane iliyopita, alifanikiwa kufanya nae tendo la ndoa siku moja pekee. "Mke wangu amenishangaza. Tangu tuoane miezi minane iliyopita alinipa unyumba siku tuliyofunga ndoa tu. tangu hapo amekataa kabisa kunipa haki yangu.


Kila nikimuomba anasema eti mimi si size yake", akalalamika mume. Mkewe alipoulizwa na ndugu zake sababu ya kumnyima mumewe chakula cha ndoa, aliwashangaza zaidi alipowaambia kwamba mumewe ana uume mkubwa sana ambao ameshindwa kuumudu.

"Aliniumiza sana siku ya kwanza na siwezi kuvumilia tena. Anipe talaka yangu nirudi kwetu", akasema mwanamke.Juhudi za ndugu hao za kumsihi dada yao ajaribu tena kufanya tendo la ndoa na mumewe wakimwambia atazoea maumbile yake, hazikufua dafu.

***********************************

Mmmh si aende kwa kungwi wamsaidie basi jinsi ya kuumudu! Huyo mume atampata mke mwingine hasa baada ya hii habari ya rungu kubwa kuenea! LOL!