Showing posts with label Shafii Abdul. Show all posts
Showing posts with label Shafii Abdul. Show all posts

Wednesday, August 13, 2008

Walimu wa sinema 'stunts'



Hao ndo walifundisha akina Peter Omari, Shaffi Abdul na Charles Magali stunts zao kwenye sinema Bongoland II. Nilishangaa waigizaji Bongo walivyoniambia kuwa eti watu wanapigana kweli hadi kuumizana wakiwa kwenye shuti. Hizi sinema za Hollywood hakuna kuumizana ingawa utadhani mtu kapigwa kweli kweli.

Tulivyokuwa Bongo niliwashauri watu wajifunze hizo stunts maana walikuwa wanatoa mafunzo bure. Zaidi ya kipigana aliwaonyesha kidogo defensive driving (yaani kuendesha gari kwa stunt). Hapa Marekani watu wanalipa maelfu ya dola kujifunza.

Mwalimu Jason Hilton alitaka kufundisha wabongo wengi lakini hakuna aliyejitokeza zaidi ya waliokuwa kwenye sinema. Nilivyowauliza vijana fulani kama wanataka kujifunza waliuza eti watalipwa shilingi ngapi. Somo inatolewa bure halafu unataka ulipwe? Si ukachukua huo utalaamu uliyopata na uende ukatengeneza pesa? Au, ni wazo baya kwangu?

Friday, February 15, 2008

Mjue Msanii wa Bongo - Shafii Abdul

Shaffii Abdul in a scene from Bongoland II

Shaffii Abdul (26) ni mwigizaji maarufu nchini Tanzania. Katika sinema ya Bongoland II anacheza kama Hamisi, mdogo wake Juma ambaye ni mhusika mkuu wa sinema. Shaffii amecheza vizuri sana kama mtu mwenye hasira za karibu.

Kusoma habari zake tembelea:

http://bongoland2.blogspot.com/